Mafunzo ya Database MySQL DATABASE somo la 2

Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE

SOMO LA PILI:

LENGO LA MAFUNZO HAYA KWA UJUMLA:

Lengo la mafunzo haya ni kukuwezesha kutumia database kwenye bloga ama website yako. Pia uweze kutumia database kwa ajili ya Android App ama web App. Pia utaweza kutumia database kwa ajili ya kudhibiti taarifa zako.

 

 

Ni nini maana ya DATABASE?

Data base ni neno la kiingereza ambalo ukilileta kwa kiswahili ni mkusanyiko wa taarifa zilizopangiliwa na kuhifadhiwa na huweza kupatikana katika mfumo wa kielectronic. Taarifa hizi zinakuwa katika majedwali (table).

 

SQL ni nini?

SQL ni lugha ya kikompyuta ambayo hutumika katika udhibiti wa database. Lugha hii yenyewe hutumiaka kwenye server. Je unajuwa ni nini maana ya server? Pitia somo la kwanza mafunzo ya PHP.

 

SQL ni kifupisho cha maneno ;- Structured Query Language. Hii ndio lugha ya kikompyuta ambayo inahusika katika kuthibiti database kama kufuta taarifa, kuedit na kuongeza ama kupunguza.

 

 

Ni ni Databae management System (DBMS)

Hizi ni software ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kudhibiti taarifa kwenye database. Mifano ya software hizi ni kama:-

  1. Ms
  2. Sql server
  3. IBM DB2
  4. Oracle
  5. MySQL
  6. Microsoft Access

Software hizi ndizo ambazo zinatumia lugha ya SQL kwa ajili ya kutumia database. Chukulia mfano php ni lugha ya kikompyuta lakini haiwezi kufanya kazi mapaka kuwe na server pamoja na software ya php. Hivi ndivyo na SQL inafanya kazi kwenye server na inahitahi software.

 

 

MySQL

Katika masomo yetu haya tutatumia MySQL, kwa kuwa ni free, pa inatumiaka sana kuliko hizo nyingine. Pia ni rahisi kuitumia. Unaweza kuipata kwa kutumia simu ama kompyuta.

 

SQL inaweza kufanya nini?

  1. Kusoma taarifa kwenye database
  2. Kuweka taarifa kwenye database
  3. Kufuta taarifa kwenye database
  4. Kubadili taarifa kwenye database
  5. Kutengeneza jedwali kwenye database
  6. Kufyta majedwali kwenye database

 

 

Mahusiano ya PHP na SQL

  1. PHP inatumika kwenye website kwa ajili ya kutumia SQL ili kufikia database.
  2. Kwa watumiaji wa blog, post na koment zinakuwa kwenye database, hivyo itatumiaka PHP ili kuweza kutumia SQL ili kuzipata post ambazo zipo kwenye database na kufanya watumiaji wa blog waweze kuziona.
  3. PHP pekee haiwezi kutumia database bila ya kuhitaji SQL
  4. Kwa kutumia SQL unaweza kutumia MYSQL ili kuthibiti database bila hata ya kuhitaji PHP.

 

 

SQL na MySQL

Kwa watumiaji wa kawaida MYySQL inatosha kuitumia hata kama hijui SQL lakini ili kuweza kudhibiti vyema database utahitaji kuzungumza kwa lugha hii ya SQL kwenye MySQL ili kudhibiti database. SQL ni lugha ya kikompyuta kama ilivyo PHP lakini MySQL ni software ambayo hutumia SQL kwa ajili ya kudhibiti database.

 

 

Je wajuwa kuwa:

“Katika siku za mwanzoni mwa facebook ilihitaji PHP, SQL na MySQL kwa ajili ya kudhibiti database yote ya facebook”. kwa mchanganyiko wa HTML, JAVASCRIPT, CSS unaweza kufanya makubwa.

 

 

Tukutane somo la Tatu tutakapoanza kujifunza hasa kuhusu hiii SQL na sheria zake. Na vipi utaweza kuitumia. Hakikisha somo la kwanza umelipitia vyema na umeweza kuandaa kifaa chako vyema.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tehama Main: Jifunze File: Download PDF Views 1472

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Dua za Mitume na Manabii    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 web hosting    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Mafunzo ya DATABASE - MySQL database somo la 8

Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya database MySQL somo la 3

Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya php level 1 somo la tatu (3)

hili ni somo la tatu katika masomo ya php level 1. Hapa utajifunza zaidi kuhusu variable na namna ya kuitengeneza.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya DATABASE - MySQL somo la 7

Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya html level 2 (html full course for beginners)

haya ni mafunzo ya HTML level 2 kwa wenye kuanza. Mafunzo haya ni muendelezo wa level 1 html. Katika course hii utajifunza mengi zaidi lu;iko level1 pia tutazidi kuboresha project yetu.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML level 1 somo la 4 (HTML basic level FOR BEGINNERS)

Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML level 1 somo la 8 (HTML basic level FOR BEGINNERS)

Katika somo hili la 8 mafunzo ya html level 8 utajifunza jinsi ya kuhost project ya html na kuwa live, watu wakaipitia na kusoma maudhui yake.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML level 1 somo la 2 (HTML basic level FOR BEGINNERS)

Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya php level 1 somo la kwanza (1)

Karibu kwenye mafunzo ya PHP level 1 na hili ni somo la kwanza. Hapa utajifunza maana ya php, inavyofanya kazi pamoja na historia yake kwa ufupi

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 8 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 8)

Hili ni somo la mwisho mafunzo ya HTML level 2 (html full course for beginners)

Soma Zaidi...