PHP level 1 somo la tano (5)

Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions.

SOMO LA TANO:
PHP FUNCTIONS:
Katika programming language, php imepata ubora wake kwa kuwa na hiki kipengele cha functions. Katika php kuna functions zaidi ya 1000. pia php inakupa uwezo wa wewe kuandika function yako mwenyewe kulingana na matarajio yako. Hivyo basi zipo funtion ambazo tayari zipo. Hizi zinaitwa built-in PHP functions. Na kuna hizo ambazo unaweka mwenyewe, hizi huitwa user defined functions.


 

Sasa function ni nini hasa?
Function ya kikundi cha maelekezo (block of statement) katika code za php ambazyo huweza kutumika zaidi na zaidi katika program. Tofauti na statement nyingine kama echo na print, ambazo huleta matokea punde tu ukiran code ama ukurasa ukufunguliwa au kurefresh. Function zenyewe mpaka zitu ziitajwe kwenye code yaani (by calling the functions).

Katika somo hili tutaona baadhi ya mifano ya built-in-function na jinsi zinavyofanya kazi kwa mifano. Hapa tutaangalia hasa kwenye string. Kama tulivyojifunzakatika somo lililopita.


 

KANUNI ZA FUNCTION (built-in-php functions)
1.Kwanza ni jina la function ila lisianze na namba mfano salamu
2.Kisha linafatiwa na mabano () mfano salamu()
3.Ndani ya mabano kunawekwa ujumbe ama maudhui ya hiyo function mfano salami(hujamb)
4.Kisha coloni ; mfano salamu salami(hujamb);

Tutajifunza kanuni nyingine za function kwenye somo linalofata kuhusu user defined functions.


 

FUNCTIONS KWENYE STRING:
1.Kujuwa idadi ya character kwenye string
. Kama unataka kujuwa je katika string kuna herufi ngapi ama namba ngapi ama character ngapi, basi tunatumia strlen() function. Neno hili ni ufupisho wa maneno string length.
Mfano:
<?php
echo strlen (“bongoclass”);
?>
Hii itakupa matokeo 10 kumaanisha kuwa kuna character 10.


 

2.Kwa kutumia php functions unaweza kubadili ama ku replace baadhi ya maandishi ndani ya string. Function inayotumika ni str_replace (). Kwa mfano katika mfano ufuatao nita replace neno bongoclass na kwa google.
<?php
echo str_replace ('karibu', 'bongoclass', 'welcome google');
?>
Hii itakupa matokeo welcome google maneno ya kwanza utaona yamebadilishwa kwa maneno ya pili.


 

3.Kuhesabu idadi ya maneno kwenye string
Katika hali ya kawaida unaweza kusema kuwa hii haina haja.lakini chukulia mfano data zipo kwenye database, na huwezi kuhesabu idadi ya maneno, na kwa mfano unatakiwa umlipe mtu kulingana na maneno aliyoandik, hapa utahitaji function ya kuweza kukuhiabia idadi ya maneno kwenye database.

Hivyo kwa namna hii function inayotumika hi hii str_word_count() mfano:-
<?php
echo str_word_count("welcome at bongoclass");
?>
Hii itakupa jibu la 3 yaani katika string iliyotumika kuna maneno matatu.


 

4.Pia unaweza kugeuza maneno, yamomeke mbelenyuma nyuma mbele. Kwa mfabo “welcome at bongoclass “ ukiligeuza litasomeka “ssalcognob ta emoclew”. ili kufanya hivi function inayotumika ni strrev yaani string revise. Mfano

<?php
echo strrev("welcome at bongoclass");
?>


 

5.Pia kwa kutumia strpos() unaweza kutafuta neno fulani kama lipo, kisha kama lipo matokeo utaambiwa position lilipo kwenye string. Yaani kama lipo la tatu kutoka mwanzo ama la nne. Kwa mfano katika string ifuatayo tutaangalia position ya neno bongoclass.

<?php
echo strpos('welcome google,welcome bongoclass,welcome facebook', 'bongoclass');
?>
Hapa utapata jibu 23 yaani neno bongoclass linapatikana kuanzia kwenye string ya 23 kutoka mwanzo. Na katika kuhesabu huku huanzia 0 na sio kwenye 1.


 

6.Kujiwa aina ya data iliyotumika
Ili uweze kujuwa aina ya data iliyotumika huwa tunatumia var_dump(). hii ni function ambayo hutumika katika kuonyesha aina ya data iliyotumika kwenye php. Angalia mifano hapo chini:-


Mfano 1:
<?php
$a = "hello piga *112#";
Var_dump ($a);
?>

Hapa iakuletea: string(16) "hello piga *112#" hii inamaana kuwa data nilizotumia kwenye mfano huu ni string, ambazo ni mkusanyiko wa herufi, namba na alama kama * na #. hiyo 16 hapo ina maanisha kuwa string iliyotumika ina character 16.


Katika somo lijalo tutaona function kwenye tarehe na kalenda na baadhi ya built-in-functions kwenye php. Hakikisha somo hili umelimudu vyema kwa kulifanyia mazoezi kabla ya kuingia somo linalofata.


Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-10-30     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 643


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Kujaa kwa memory au hard disc
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vitu vya kufanya endapo memory au hard disk itajaa Soma Zaidi...

Mafunzo ya Database MySQL DATABASE somo la 2
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE Soma Zaidi...

Tembo
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama tembo Soma Zaidi...

UTI na ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa UTI kwa wajawazito Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 8 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Katika somo hili la 8 mafunzo ya html level 8 utajifunza jinsi ya kuhost project ya html na kuwa live, watu wakaipitia na kusoma maudhui yake. Soma Zaidi...

Niambie mwanya na pengo kwa kiingereza vinaitwaje?
Give inakuwa mwajima unaitwaje kwa kiingereza. Kama hilo haji base niambie pengo linaitwaje kwa kiingereza. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 4 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia. Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamin A
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamin A Soma Zaidi...

Kurudisha mafaili na data zilizopotea
Posti hii inakwenda kukupa elimu ya kurudisha mafaili na data zilizopotea Soma Zaidi...

Cheetah
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama cheetah Soma Zaidi...

Epuka malware (virus,work)ukiwa mtandaoni
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuepuka malware ukiwa mtandaoni Soma Zaidi...

Matatizo katika hard disk
Posti hii inakwenda kukupa baadhi ya matatizo katika hard disk Soma Zaidi...