Huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 10. katika somo hili tutakwenda kuendelea namna ya kupangilia muonekano wa data zako kwenye database.
Katika somo la 9 tuliona namna ya kutumia database yaani kusoma taarifa kwenye database kwa kutumia SQL. Katika somo hili tutajifunza namna ya kupangilia data zako yaani sorting data kulingana na mahitaji yako. Hapa tutakwenda kutumia command kama WHERE, ORDER BY, AND, OR, ASC, DESC, RAND(). pia katika somo hili tutatumia sana SQL kama tulivyofanya katika somo lililopita:-
Katika somo hili tutatumia database yetu yenye jina hotel na table menu. Hivyo tutakwenda kujifunza somo letu kwa kutumia database hii.
1. Kupangilia data kutoka kubwa kwenda ndodo
Katika SQL unapotaka kupangilia data kuwa zionekane kwa mpangilio upi tunatumia ORDER BY kisha unakuja kuweka hiyo column ambayo unataka iangaiwe. Kisha unakuja kuweka huo mpangilio wako, kama ni kuanzia kubwa kuja ndogo hapo tutatumia DESCENGING order ambapo kifupi chake ni DESC. Baada ya hapo unaweza kutumia LIMIT kama tulivyoona katika somo lililopita.
Mfano:
Katika menu yetu tunataka zijipange kutoka chakula chenye gharama kubwa kuja chakula chenye gharama ndogo. Hvyo kama tulivyoona katika somo lililopita utatumia select kama ni coumn zote utaweka * kisha from kisha jina la table kisha ORDER BY hapa sasa tuta zipanga kulingana na price zao, hivyo itakuwa ORDER BY price kisha tutaweka mpangilio tunaotaka kama ni kubwa kja ndogo tutatumia DESC unaweza kuongeza LIMIT 5 kwa mfano ili kuona idadi maalumu Hivyo command yote itaonekana hivi:-
SELECT * FROM `menu` ORDER BY `price` DESC LIMIT 5;
2. Kupangilia data kutoka ndogo kwenda kubwa
Mfano huu haupo tofauti sana na huo wa juu. Hapa tunataka data zijipange kulungana na gharama zao lakini zianze ndogo zije kubwa. Pia tutataka kuoan 5 tu za mwanzo. Ili kuweza kupanga ndogo kwenda kubwa tunatumia ASCENDING ORDER ambayo kifupi chake ni ASC. Hivyo command nzima itakuwa hivi
SELECT * FROM `menu` ORDER BY `price` ASC LIMIT 5;
3. Kupangilia data random (yaani bila mpangilio maalumu)
Yaani tunataka taarifa zijipango kwa mchanganyiko bila kujali kubwa ama ndogo. Yaani hovyohovyo. Kufanya hivi tutatumia ORDER BY RAND(). Yaani random. Hivyo command itakuwa hivi
SELECT * FROM `menu` ORDER BY RAND() LIMIT 5
4. Kupanga kutoka A kwenda Z ama kutoka Z kwenda A.
Sasa menu yetu tunataka kuzisoma data kwa majina yake kutoka A kwenda Z. kitu cha kwanza ni kujuwa column yenye majina ni ipi. Katika table yetu majina yapo kwenye column yenye jina name. Kupanga tutoka A kwenda Z tutatumia ASC kama tulivyoona kwenye mfano uliotangaulia. Na kupanda kutoka Z kwenda A tutatumia DESC kama tulvyoona huko juu.
Kikubwa hapa tumebadili column. Hapo mwanzo tulitumia column ya price kwani tulikuwa tunazipanga kulingana na price zao. Sasa tutatumia column ya name kwani tunapanga kulingana na majina yao.
A. Hivyo kupanga A to Z tutatumia
SELECT * FROM `menu` ORDER BY name ASC LIMIT 5
Hapo data zako zitajipanga kwa majina yao kutoka A to Z
B. Kupanga Z to A
SELECT * FROM `menu` ORDER BY name DESC LIMIT 5
Hapodata zako zitajipanga kutoka Z to A kulingana na majina (name)
5. Pia unaweza kuchaguwa column za kuona kama tulivyoona somo la tisa. Yaani namaanisha unataka kuosma majina na gharama tu, ila zijipange kulingana na gharama zake kutoka kubwa kwenda ndogo mathalan. Utofauti wa mfano huu na ulotangulia ni kuwa hapo mwanzo umezisoma data zote kuanzia id, name, description na price. (rejea matumizi ya nyota * kwenye somo la tisa)
Hivyo kwa mfano huo comand itakuwa hivi:
SELECT name, price FROM `menu`ORDER BY price DESC LIMIT 8;
Hapo utaona column mbili tua mbayo ni ya name na price na zitajipanga kutoka yenye gharama kubwa kwenda ndogo na itaonyesha row 8 tu.
Endelea nami kwenye somo la 11 ambapo tutajifunza namna ya kutumia where, and, or . kwa sasa endelea kufanyia mazoezi ya kutosha database hii.
Mafunzo haya yamekujia kwa Ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email: mafunzo@bongoclass.com
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
haya ni mafunzo ya HTML level 2 kwa wenye kuanza. Mafunzo haya ni muendelezo wa level 1 html. Katika course hii utajifunza mengi zaidi lu;iko level1 pia tutazidi kuboresha project yetu.
Soma Zaidi...Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE
Soma Zaidi...Hapa utajifunza utofauti kati ya php constant na variable. Na hili ni somo la nane katika mfululizo wa masomo haya ya php level 1.
Soma Zaidi...Ktika somo hili la 7 utajifunza namna ya kuandaa na kujiandaa kutengeneza website ama blog. Pia utajifunza maandalizi ya kuhost
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions.
Soma Zaidi...Hili n somo la tatu katka muendelezo wa mafunzo ya HTML LEVEL 2 kwa lugha ya kiswahili. Mafunzo haya yanakujia kwa Ihsani ya bongoclass
Soma Zaidi...Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza.
Soma Zaidi...Somo la 10 mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza kuhusu condition statement.
Soma Zaidi...haya ni mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 9. katika soo hili utajifunza namna ya kusoma ama kutumia taarifa zilizomo kwenye DATABASE.
Soma Zaidi...Hii ni tafiti ambayo itakushangaza, kwa namna ambavyo matumizi ya AI yalivyo na athari kwenye uwezo wa kufikiri
Soma Zaidi...