Haya ni mafunzo ya HTML kwa wanaoanza level ya kwanza, na hili ni somo la kwanza katika masomo 8 yatakayokujia katika mtiririko wa course hii.
HTML SOMO LA KWANZA
HTML ni ufupisho wa maneno yanayosomeka kama:-
Hypertext
Markup
Language
Ni lugha ya komputa inayotumika katika kutengenezea kurasa za tovuti (website) ama blog.Inaungana na lugha nyingine katika kuboresha kurrasa za tovuti ama blog na kuzifanya ziweze kufanya kazi iliyokusudiwa vyema. Unaweza kutumia HTML tu ukatengeneza website yako bila ya lugha nyingine. Hata hivyo muonekano wake hautakuwa vyema sana kama hutatumia nyinggine.
Je na wewe una ndoto za kuwa na blog ama website uliyoitengeneza wewe mwenyewe. Mafunzo haya ni kwa ajili yako. Katika mafunzo haya utajifunza namna ya kutengeneza website yako kupitia kiganja chako yaani simu yako ya mkononi. Kama utakuwa na kompyuta hatutakuacha pia.
Somo hili la kwanza utajifunza namna ya kuandaa simu yako ama kompyuta yako kwa ajili ya kutengeneza website, ama kwa ajili ya kutumia HTML. Kama tutaenda vyema na mafunzo haya hadi mwisho nakuhakikishia kama Mwenyezi Mungu akitujaalia nguvu, uwezo na uhai, utaweza kutengeneza website yako na kuiweka live.
Muda wa masomo haya kwa hatuwa za Awali (Basics) itakuwa na wiki moja. Kisha baada ya hapo hatuwa ya pili ya mafunzo itaendelea. Tafadhali kuwa tayari kujifunza, kuwa muulizaji na mchangiaji:
VIGEZO VYA KUJIFUNZA:
1.Kuwa na simu ya smartphone au kompyuta
2.Uwe unajuwa kusoma na kuandika
3.Kuwa tayari kujifunza
4.Kuwa mjanja
5.Uwe mwenye kufanyi akazi (fanya mazoezi)
NAMNA YA KUANDAA SIMU YAKO:
1.Download App inayoitwa TrebEdit. Tumia link hii https://play.google.com/store/apps/details?id=com.teejay.trebedit
2.Funguwa App yako kisha bofya Menu
3.Bofya palipoandikwa Workplace
4.Bofya kitufe chenye alama ya kujumlisha chini
5.Kisha bofya palipandikwa New Project
6.Andika jina la Project (mimi natumia HTML) kisha bofya save.
7.Ingia kwenye project uliotengeneza kwa kubofya jina lake, ukurasa mpya utafunguka
8.Bofya tena kitufe cha alama ya kujumlisha
9.Bofya palipoandikwa new folder (hapa tunatengeneza folda la kuweka picha tutakazokuja kuzitumia kwenye tovutu tutakayotengeneza)
10.Andika jina la folda tumia image kisha bofya save.
11.Baada ya hapo rudi nyuma hatuwa moja kwenye project yako.
12.Bofya tena jina la project yako
13.Bofya kitufe cha alama ya kujumlisha
14.Bofya palipandika New file (hapa ndipo tutakapoanzia kuweka code za kutengeneza tovuti yetu)
15.Utatkiwa kuandika jina la file hapo andika index.html (hili ndio faili letu la kwanza la tovuti yetu.
16.Bofya faili hilo ulilolitengeneza, utaona limeandika index.html
17.Baada ya kufunguka kuna maneno chini yameandika html snippet, bofya hayo maneno
18.Ukursa wako sasa utaona una code HONGERA SANA KWA KUFIKA HATUWA HII
19.Juu ya ukurasa kuna kibatani cha kusave, kimefanana na kile cha kwenye microsoft office. Bofya hicho kibatani, hapo utakuwa umesave code zilizopo hapo.
20.Kuna kibatani kingni cha kuplay kimefana na kile tunachotumia kwenye media player. Bofya hicho kupreview code zako.
21.Utaona ukurasa mtupu. Vyema sasa fanya hivi rudi nyuma kisha:-
22.Tafuta haya maneno
Page title
kisha yabadilishe yasomeka
Home Page
23.Chini ya maneno haya
weka maneno haya
Haya ni mafunzo ya HTML kwa kutumia simu
NAMNA YA KUANDAA KOMPYUTA YAKO
Kwa watumiaji wa kompyuta funguwa notepad, ama notepadplus ama sublimetext3. unaweza kudowload bure ila kwa notepad haina haja ya kudownload ipo kwenye kompyuta yako. Kwanza tengeneza folder lipe jina website.kisha ndani ya folder hilo tengeneza folda jingine lipe jina imae. Rudi kwenye folda la website Tengeneza faili jipya kisha pest code hizo hapo chini kwenye faili lako.save as andika jina index.html. Lifunguwe faili lako la index.html kwakutumia browser kama chrome litafungukakama website. Angalia video itakusaidia. Unaweza kudownload notepadplus hapa https://notepad-plus-plus.org/downloads/v8.1.4/
My First Webpage
Welcome to my brand new website.
Somo la pili tutaanza kujifunza hizo code ulizoziweka kazi yake na vipi zinafanya kazi. Kama umefanikiwa hatuwa zote hizo tupe maoni yako, ama tutumie screenshot yako.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia.
Soma Zaidi...Katika somo hili la 8 mafunzo ya html level 8 utajifunza jinsi ya kuhost project ya html na kuwa live, watu wakaipitia na kusoma maudhui yake.
Soma Zaidi...hili ni somo la tatu katika masomo ya php level 1. Hapa utajifunza zaidi kuhusu variable na namna ya kuitengeneza.
Soma Zaidi...haya ni mafunzo ya HTML level 2 kwa wenye kuanza. Mafunzo haya ni muendelezo wa level 1 html. Katika course hii utajifunza mengi zaidi lu;iko level1 pia tutazidi kuboresha project yetu.
Soma Zaidi...Karibu tena katika mafunzo haya ya html level 2 na hili ni somo la 5. Katika somo hili utajifunza zaidi kuhusu kuweka style kwenye html file.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 6. Katika somo hili tutakwenda kuona jinsi ya kutengeneza table kwa kutumia MySQL na kwa kutuma SQL.
Soma Zaidi...Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database
Soma Zaidi...Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia.
Soma Zaidi...