haya ni mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 9. katika soo hili utajifunza namna ya kusoma ama kutumia taarifa zilizomo kwenye DATABASE.
SOMO LA TISA.
Katika somo hili la tisa tutakqenda kuona namna ya kutumia database. Somo hili tutajifunza jinsi ya kusoma data kwenye database. Hapa tutaona jinsi ya kutumia command kama:-
Somo hili ni msingi mzuri sana kwa masomo yajayo. Somo hili tutakwenda kutumia sana uwanja wa SQL tofauti na masomo yaliyotangalia ambapo tulikuwa tukitumia MySQL interface na SQL .
Maandalizi ya somo la tisa:
tengeneza database yemye jina hoteli kisha tengeneza table yennye jina menu ama pest code hizi kwenye uwanja wa sql:-
CREATE TABLE IF NOT EXISTS `menu` (
`id` int(100) NOT NULL,
`name` varchar(255) NOT NULL,
`description` varchar(255) NOT NULL,
`price` int(100) NOT NULL
) ENGINE=InnoDB DEFAULT CHARSET=utf8mb4;
Kisha jaza data kwenye table yako. Unaweza kupest data hizi kwenye uwanja wa sql:-
INSERT INTO `menu` (`id`, `name`, `description`, `price`) VALUES
(1, 'ugali', 'Pata ugali na mchuzi, ama ugali na nyama ama ugali na samaki. Ugali wa mahindi na muhogo', 1500),
(2, 'Wali', 'Pata waki na mchuzi, ama wali na nyama ama wali na samaki.', 2000),
(3, 'chai', 'Pata chai maandazi, chapati, ndizi, na supu', 3000),
(4, 'internet', 'Pata huduma za internet free huku ukijipatia chakula hapa, utalipia kila nusu saa utakalotuia', 700),
(5, 'simu', 'Pata huduma za simu bre huku ukijipatia chakula hapa, utalipia kila nusu saa utakalotuia', 1200),
(6, 'ushauri', 'Tunatowa huduma za ushauri nasaha, utalipia kwa kila nusu saa utakaloluwa unapewa ushauri', 1000),
(7, 'huduma za Afya', 'Hapa utapata huduma za afya za awali kama bipimo vya uti, malaria, mimba na vinginevyo. utalipia kwa kila kipimo', 5000),
(8, 'Mapishi', 'pia tunatowa mafunzo ya mapishi kwa gharama nafuu. Utalipia kwa kila nusu saa utakalokuwa unafundishwa.', 9500),
(9, 'matanazo', 'Pia tunatowa matangazo mbalimbali kuwapatia waeja wetu. utalipia kwa kila tangazo litakapotagazwa', 25000),
(10, 'maji ya kunywa', 'huduma hii itatoka kwa gharama nafuu. utajipatia maji ya kunywa baridi. Utalipia kwa kila glasi', 300);
Baada yahapo utakuwa upo tayari pamoja nami katika somo hili la tisa katika mafunzo ya database kwa kutumia software ya MySQl.
1. Kusoma taarifa (data) zilizopo kwenye database
Hapa tunatumia command ya SELECT. Lakini pia tunaweza kutumia MySQL interface kufanya hili. Hapa nitaanza kukuonyesha namna ya kutumia MySQL intrface.
2. Kusoma taarifa kwenye database kwa kutumia SQl
Kwa kutumia mfano huo hapo tumechaguwa data zote. Sasa chukulia mfano unataka kuona majina tu ya menu na si gharama na maelezo meengi. Kufanya hivi utahitajika kutaja hivyo unachotaka kukiona pale tulipoweka nota: Mfano:-
Table yetu inaitwa menu. Na ina column kama name, descriptions, na price. Sasa hapa ninataka kusoma column ya name tu. Hapa tutatumia command hii
SELECT name FROM `menu`;
Utaona hapo pale kwenye nyota ambapo ilimaanisha All data tumeitowa na kuweka name kwa maana tunataka kuona name tu na si data zote. Hapo ukibofya Go ukurasa utakaokuja ni wa name tu. Kwa kufanya hivi utaweza kuchaguwa chochote kwa mfano:
Pia unaweza kuchaguwa viwili ama vitatu. Yaani kwa mfano ninahitaji kuonyesha name na price tu sitaki kuona maelezo meengi. Kufanya hivi utatengenisha kwa kutumia koma (,) ila neno la mwisho halitakiwi kuwa na koma.
Sasa tuseme tunataka kusoma name na price tu yaani utaona majina ya menu na gharama zake. Kufanya hivi tutatumia command hii:-
SELECT name, price FROM `menu`; ukibpfya Go utaoona rodha ya majina ya menu na gharama tu. Kwa kufanya hivi utaweza kubadili chohote hapo ama hata ukitaka kuta vyote mfano SELECT name, price, description FROM `menu`;
Taarifa zako zitajipanga kulingana na ulivyoandika wewe hizi command na sio kulingana na mpangilio wake kwenye database. Mfano kwenye database kilichoanza ni id kisha name kisha description kisha price. Sasa sisi tunataka kupangilia ianze gharama kisha id kisha description kisha name. Weka command hii SELECT price, id, description, name FROM `menu`; ukibofya go hapo data zitajipanga hivyohivyo kama ulivyoandika.
3. Kulimit kiasi cha taarifa
Hii ina maana kuwa chukulia mfano table yako ina orodha ya row 1000 za data na wewe huna huo muda wa kusoma zote. Hivyo utahitaji lamda kusoma kwanza 20 za mwano ama ishirini za mwisho. Kufanya hivi tutatumia LIMIT kisha tutaweka idadi ya row unazotaka kuzisoma kwa mfano kama 4 utaweka LIMIT 4.
Mfano tunataka kusoma name na price ila tunataka zionekane row 20 hpata tutaweka command hii:-
SELECT name, price FROM `menu` LIMIT 4 hapo ukibofya Go utaletewa orodha ya row nne tu. Unaweza kutumia mfano huu kwa command nyingine. Mfano
SELECT name FROM `menu` LIMIT 6;
SELECT price FROM `menu` LIMIT 7;
SELECT * FROM `menu` LIMIT 8;
Katika somo linalofata tutajifunza namna ya kupangilia hizo orodha za data. Mfano unataka zijipange kutoka yenye price kubwa kwenda ndogo, ama zijipange kutoka A to Z ama zijipage random. Command tutakayokuja kuitumia ni ORDER BY hivyo nakusihi usikose somo la 10.
NB: course hii itakusanya masomo 12 tu, kabla ya kuingia course ya pili. Level hii hatutakuwa na project. Ila natumai tutakuwa pamoja level ya pili ambapo utapata fursa ya kufanya project nasi:
Mafunzo haya yamekujia kwa Ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email: mafunzo@bongoclass.com
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.
Soma Zaidi...Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...Somo la 10 mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza kuhusu condition statement.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia software ya MySQL na hili ni somo la tano. katika somo hili utajifunza type of data yaani aina ya taarifa ambazo unaweza kuzihifadhi kwenye database yako.
Soma Zaidi...Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza.
Soma Zaidi...Karibu tena katika somo la nne la mafunzo ya HTML level2 html full course for beginners. Katika somo hili utajifunza kuhusu attributes na namna zinavyofanya kazi
Soma Zaidi...Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi.
Soma Zaidi...Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya muda mfupi katika kujifunza hasa ujuzi wa kutengeneza Android App hata kama haujui kitu kuhusiana na Android Development
Soma Zaidi...hili ni somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2 html full course for beginners. Katika somo hili tutaangalia utangulizi juu ya HTML na pia utajifunza faida za HTML.
Soma Zaidi...