Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho.
SOMO LA NANE
Katika somo lililotangulia tumejifunz namna ya kubadili jina kwenye table pia tukaona kuongeza column. Sasa katika somo hili hasa ndipo tunakwenda kuweka data kwenye table yetu, yaani kuweka data kwenye database. Katika somo hili tunakwenda kutumia ile table tulioiita post.
1. Kuweka data kwenye table kwa kutumia MySQL
Kama tulivyofanya kwenye masomo yaliyotangulia kuwa tunatumia MySQl kisha tunatumia SQL statement hivyohivyo ndivyo tutakavyofanya kwenye somo hili.Ili kuweka taarifa kwenye database yako fuata hatuwa zifuata:-
Fanya hivi kuweka posta zaidi na kwenye menu weka menu inayoitwa afya.
2. Kuweka data kwenye table kwa kutumia SQL
Sasa tunakwenda kuongeza data kwenye table yetu menu. Tujaalie tunataka kuweka menu ya afya kwenye blog yetu sasa tunakwenda kuongeza menu ya afya.
Kwanza tuedit table ya menu nayo iwena unique kama tulivyofanya kwenye post. Hivyo ingia kwenye structure, kwenye id bofya change, angalia kwenye Null kama kuna tiki ondoa, angalia kwenye A_I kama hakuna tiki weka, kisha save.
Kwenye id nenda pembeni ya change bofya more, kisha unique kisha kwenye kaujumbe utakaokuja bofya OK.
Kisha edit na hiyo title ingia change kwenye null ondoa tiki kisha save. Baada ya hapo table yetu tutakuwa tumeiandaa vyema kwa ajili ya kutumia SQL kwa urahisi kabisa. Sasa ili uweze kuweka data kwa kutumia SQl fuata hatuwa hizi:-
3. Kuedit na kufuta data kwenye table
Kuedit data kwenye MySQl rahisi sana. Kwanza bofya hiyo table mfano post. Kisha bofya browser utaona data zako.utaone katika kila row yako ya data kuna neno edit na delete. Unachotakiwa kufanya ni kubofya edit ama delete. Ukibofya delete maana yake unafuta. Na ukibofya edit maana yake utaedit.ukimaliza kuedit bofya neno GO na hapo data yako itakuwa imebadilika.
Pia MySQL inakupa fursa ya kuedit humohumo huku tunaita inline edit. Unachotakiwa kufanya kama unataka kuedit column ya conten bofya hapo, kwenye data yenyewe ya kontente yaani maandishi ambayo umesha andika. Baada ya hapo utaona kamsitari ka kuonesha sasa unaweza kuedit. Hakuna haja ya kusave ukiodoka tu hapo itasave automatik. Ama unaweza pia kubofya pembeni ambapo hapana maandishi itasave yenyewe automatiki.
4. Kufuta ama kuedit kwa kutumia SQL
Kwa kutumia SQL pia unaweza kufuta data kwenye database ama kuedit. Ila jambo hili tutajifunza katika masomo yanayofuata kwa sasa tuendelee kutumia MySQL interface kufanya haya.
Somo linalofuata tutajifunza namna ya kusoma data kwenye database. Kazi yako kwa sasa kablya ya kuingia somo lijalo ni kuhakikisha kuwa umeweka data nyingi zaidi kwenye table zako. Unaweza kupost posta 5 kwenye dabke ya post na menu hivyo hivyoo ama zaidi ya hapo.
Mafunzo haya yamekujia kwa Ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email: mafunzo@bongoclass.com
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowMafunzo ya php level 1 somo ka 12 mwisho wa mafunzo. Hapa utaona project ambazo unaweza kufanya kutokana na mafunzo haya.
Soma Zaidi...Hili ni somo la saba, mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika function yako mwenyewe.
Soma Zaidi...Hili n somo la tatu katka muendelezo wa mafunzo ya HTML LEVEL 2 kwa lugha ya kiswahili. Mafunzo haya yanakujia kwa Ihsani ya bongoclass
Soma Zaidi...Hili ni somo la mwisho mafunzo ya HTML level 2 (html full course for beginners)
Soma Zaidi...Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 6. Katika somo hili tutakwenda kuona jinsi ya kutengeneza table kwa kutumia MySQL na kwa kutuma SQL.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza utofauti kati ya php constant na variable. Na hili ni somo la nane katika mfululizo wa masomo haya ya php level 1.
Soma Zaidi...Somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2. Katika somo hili utajifunza maana ya HTML pamoja na historia yake fupi.
Soma Zaidi...Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...Huu ni utangalizi wa mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza level ya kwanza kwa lugha ya kiswahili. Haapa utapata msingi wa kuweza kutengeneza tovuti na blog.
Soma Zaidi...