Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array.
SOMO LA 9
PHP ARRAY
Array ni kama variable, tofauti hii ni kuwa inahifathi thamani ya data nyingi ndani ya variable moja. Yaani variable moja hapa itabeba thamani nyingi tofauti na tulivyosoma hapo nyuma. Cheki mifano hapo chini:-
Array sikuzote inaaznia kuhesabu kuanzia 0 na kuendelea. Unaweza kuchaguwa list katika array ipi unataka kuionyesha na ipi hutaki utafanya hivi kwa kuiondoa namba ya array hiyo ama kuiweka.
Mfano:
$masomo = array("hisabati", "sayansi", "maarifa", "kiswahili", "uraina", "kiingereza");
echo "ninasoma" . $masomo [0] . "," . $masomo[1] . "," . $masomo[3]. "," . $masomo[4]. "," . $masomo[5]. "," . ".";
Hii itakupa matokeo
ninasomahisabati,sayansi,uraina,kiingereza,.
Hapo kwa kutumia variabl ilitakiwa tuweke kila kimoja hapo na variable yake. Mfano hapo tungepata variable 5, yaani
$masomo = “sayansi”;
$masomo = “kiswahili”;
Na kuendelea. Hivyo kwa kutumia array tumeweza kupunguza kazi. Kwa kutumia array unaweza kuwa na list ya vitu hata 1000 kwenye array moja na ukakiweka kila kimoja unapotaka kwa kuangalia index namba ya ke kwa kuanzia 0.
KANUNI YA KUTENGENEZA ARRAY:
Kutengeneza array tunatumia function ya array (); kisha ndani yake ndipo zitafata hizo string ambazo kila moja hutenganishwa kwa kutumia , koma. String ya kwanz akatika array ndio array ya kwanza kuhesabiwa ambayo itakuwa ni namba 0, na inayofata itapewa namba 1.
Kuesabu jumla ya array
Kufanya hivi tutatumia function ya count() mfano.
$masomo = array("hisabati", "sayansi", "maarifa", "kiswahili", "uraina", "kiingereza");
echo count($masomo);
?>
Hii itakupa jibu 6, ina maana ndani yake kuna array sita ambazo zimeanza kuhesabiwa kutoka 0,1,2,3,4,5. hapa unapata jumla ya sita.
Pia unaweza kuonyesha array zote bila hata ya juzitajia nmba zao kama ilivyo kwenye mfano wa kwanza.
$masomo = array("hisabati", "sayansi", "maarifa", "kiswahili", "uraina", "kiingereza");
$arrlength = count($masomo);
for ($a = 0; $a < $arrlength; $a++){
echo $masomo [$a];
}
?>
Hii itakuletea matokeo
Hisabatisayansimaarifakiswahiliurainakiingereza
Tutajifunza zaidi juu ya kufanya hivi katika muendelezo wa masomo haya.
Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Karibu tena katika somo la nne la mafunzo ya HTML level2 html full course for beginners. Katika somo hili utajifunza kuhusu attributes na namna zinavyofanya kazi
Soma Zaidi...Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 10. katika somo hili tutakwenda kuendelea namna ya kupangilia muonekano wa data zako kwenye database.
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya HTML kwa wanaoanza level ya kwanza, na hili ni somo la kwanza katika masomo 8 yatakayokujia katika mtiririko wa course hii.
Soma Zaidi...huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database klwa kutumia MySQL na hili ni somo la 11. katika somo hili tutaendelea kujifunza mpangilio wa muonekano wa data kwenye database.
Soma Zaidi...Hii ni tafiti ambayo itakushangaza, kwa namna ambavyo matumizi ya AI yalivyo na athari kwenye uwezo wa kufikiri
Soma Zaidi...Katika somo hilivutajifunza namna ya kutumia HTML form. Namna ya kuookea taarifa kutoka kwenye madodoso ya html form.
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya muda mfupi katika kujifunza hasa ujuzi wa kutengeneza Android App hata kama haujui kitu kuhusiana na Android Development
Soma Zaidi...somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia.
Soma Zaidi...hili ni somo la sita katika mfululizo wa mafunzo ya HTML level 1. Katika somo hili tutajifunza mambo makuu matatu ambayo ni kuweka menyu, kuweka background color na kufanya faili lako liwe responsive.
Soma Zaidi...