image

Mafunzo ya DATABASE - MySQL database somo la 5

Huu ni muendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia software ya MySQL na hili ni somo la tano. katika somo hili utajifunza type of data yaani aina ya taarifa ambazo unaweza kuzihifadhi kwenye database yako.

TYPE OF DATA IN MySQL:

Somo hili linakwenda kukufundisha aina za taarifa ambazo unaweza kuzihifadhi kwenye database (type of data). Ili kuelewa maana ya hili somo, chukulia database kama storage yako au memori kadi. Sasa kwenye memori kadi utaweza kuhifadhi video, miziki, document na nyinginezo. Ila sasa kwa upande wa database huwezi kuhifadhi video, ama mziki au document kama pdf kama ilivyo kwenye memory card. Katika database kuna namna yake ya kuweza kuhifadhi hizi media file..

 

Hivyo ili kujuwa ni taarifa zipi sasa unaweza kuzihifadhi kwenye database? Kama video inaweza kukaa kwenye database na umejifunza kuwa blog zinatumia database vipi post ya blog itaweza kuwa na image ama video? Haya yote utajifunza katika mlolongo wa somo hili na yanayofata.

 

Aina za data kwenye MySQL database:

 1. CHAR
 2. VARCHAR
 3. BINARY
 4. VARBINARY
 5. TINYBLOB
 6. TINYTEXT
 7. TEXT
 8. MEDIUMTEXT
 9. MEDIUMBLOB
 10. LONGTEXT
 11. LONGBLOB
 12. ENUM
 13. SET
 14. BIT
 15. TINYINT
 16. BOOL
 17. BOOLEAN
 18. SMALLINT
 19. MEDIUMINT
 20. INT
 21. INTEGER
 22. BIGINT
 23. FLOAT
 24. DOUBLE
 25. DECIMAL
 26. DEC
 27. DATE
 28. DATETIME
 29. TIMESTAMP
 30. TIME
 31. YEAR

 

 

Kabla hatujaziona data hizi na jinsi zinavyofanya kazi kwanza kuna mbambo hapa tunatakiwa tuyaweke wazi. Kwanza tunatakiwa tielewe maana ya charcter, utf, text, letter, unicode, non-unicode.

 

Katika uandishi jumla ya herufi, namba na alama za kiuandishi kama emoji, visitari, vinukta , alama za koma na kadhalika, jumla ya yote haya yanaitwa character. Mfano neno “hallo bongoclass!!!” hapa kuna jumla ya mane mawili ambayo ni halo na neno bongoclass. Lakini haya maneno mawili yana jumala ya character 21 ukijumlisha na hizo funga semi na fungua na space moja. Hivyo ukisikia character zipo hivi.

 

Sasa wanaposema character set ni seti maalumu ya hizo character ambayo hutumika katika kifaa cha kielectrinic ili kupeleka taarifa kutoka kifaa kwenda kingine. Kwa mfano unapoandika code. Kwa mfano katika visimu vya batani kama mtu akikutumia emoj haitaonyesha lakini utaona kuna viduara duara na vijialama. Hii ni kwa sababu character set inayotumika kwenye simu ya batani haiwezi kutafasiri baadhi ya character zilizotoka kwenye simu ya smart phone.

 

Hizi set zipo nyingi ila standard ambayo hukubali angalau character karibia zote, ila si zote ni UTF-8. hiki ni kifupisho cha maneno Unicode (or Universal Coded Character Set) Transformation Format – 8-bit.

 

AINA ZA DATA KATIKA MySQL

Aina hizi zimegawanyika katika makundi mengi hapa nitafafanua kwa uchache katika makundi matatu, ambayo ni namba, text, na tarehe.

 

1. Kundi la Text

Kundi hili linabeba data kama VARCHAR. Huu ni mkusanyiko wa character kuanzia 0 hadi 255. pia kuna VARCHAR yaani variable character hii hubeba character kuanzia 0 mpaka 65535. BINARY hii ni sawa na CHAR ila utofauti hii inakuwa na binary string. VARBINARY nayo ni sawa na VARCHAR ila hii hukusanya binary string. Kisha kuna TINYBLOB hii hukusanya taarifa za media file kama picha. Yenyewe inachukuwa character 255. media file haitahifadhiwa kama kwenye memori card ila utaiona kama vile ni mkusanyiko wa character ambazo zipo katika binary.

 

TINYTEXT hii hukusanya text zenye character mpaka 255. TEXT hii hukusanya taarifa mpaka character 65535. BLOB hii nayo hukusanya media file mpaka character 65535. MEDIUMTEXT hukusanya taarifa mpaka character 16, 777, 215. MEDIUMBLOB hii hukusanya BLOB mpaka character 4,294,967,295. ENUM hukusanya character mpaka 65535. yenyewe inabeba orodha ya vitu, yaani vitu vinakaa katika machaguo maalumu.  Set yenyewe ni kama ENUM ila inakuwa na machaguo 64.

 

2. Kundi la namba

Hapa kuna BIT hii hubeba character mapka 64. lakini TINYINT hhubeba character mpaka 255. BOOL hii hubeba zero na nonzero. BOOLEAN ni sawa na BOOL. Zenyewe kukiwa na 0 maana yake false na kukiwa na isiyokuwa zero maana yake tue. Kisha kuna SMALLINT hubeba kuanzia 0 mapaka 65535.

 

Pia kuna MEDIUMTEXT hii hubeba character kuanzia 0 mpaka 16777215. INTEGER ni sawa na INT. BIGINT hubeba character mpaka mabilioni huko. FLOAT hubeba desimali na zile za vipeo zinaitwa power. Kuna DOUBLE inafanana na FLOAT. Pia kuna DEC ambayo ni sawa na DECIMAL.

 

3. Kundi la tarehe na saa

Hapa kuna DATE ambayo inahusu tarehe tu kuanzia mwaka 1000 mapak mwaka 9999. kisha kuna DATETIME hii hubeba tarehe na saa kwa pamoja. Kisha kuna TIMESTAMP saa na tarehe huhifadhiwa katika mfumo wa sekunde kuanzia mwaka 1970. kisha kuna TIME mabyo huonyesha time tu. Na ya mwisho ni YEAR anbayo huonyesha mwaka tu wenye character 4.

 

Data hizi zinaweza kupunguwa amba kuongezeka kulingana na software iliyotumika. Unaweza kukuta baadhi ya data za hapa hazipo kwenye software ntingine. .

 

Unawez akujiuliza asa hizi aina za data nitazitumia vipi. Usijali somo linalofata tutakwenda kutengeneza table yaani majedwali kwa ajili ya kuwekea taarifa kwenye database. Kufanya hivyo itatubidi tujuwe aina ya data ambazo tutaziweka kwenye majedwali hayo.

 

 

Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: mafunzo@bongoclass.com

            

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/18/Thursday - 08:57:03 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 916


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 2 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 1 somo la 2 for beginner (html full course for beginners)
Somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2. Katika somo hili utajifunza maana ya HTML pamoja na historia yake fupi. Soma Zaidi...

Mafunzo ya Database MySQL DATABASE somo la 2
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 4 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 4)
Karibu tena katika somo la nne la mafunzo ya HTML level2 html full course for beginners. Katika somo hili utajifunza kuhusu attributes na namna zinavyofanya kazi Soma Zaidi...

Mafunzo ya php level 1 somo la tatu (3)
hili ni somo la tatu katika masomo ya php level 1. Hapa utajifunza zaidi kuhusu variable na namna ya kuitengeneza. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 3 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi. Soma Zaidi...

Php level 1 somo la saba (7)
Hili ni somo la saba, mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika function yako mwenyewe. Soma Zaidi...

Utangulizi wa Android App Development
Haya ni mafunzo ya muda mfupi katika kujifunza hasa ujuzi wa kutengeneza Android App hata kama haujui kitu kuhusiana na Android Development Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 6 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 6)
Katika somo hili la 6 mafunzo ya HTML level 2, tutajfunza namna ya kugawa ukurasa wa wavuti wa html. Soma Zaidi...

Mafunzo ya DATABASE - MySQL somo la 7
Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 1 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 1)
hili ni somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2 html full course for beginners. Katika somo hili tutaangalia utangulizi juu ya HTML na pia utajifunza faida za HTML. Soma Zaidi...

Mafunzo ya database MySQL somo la 3
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza. Soma Zaidi...