Katika somo hili la php level 1 somo la 6 utajifunza namna ya kutumia tarehe yaani function date() kwenye PHP
SOMO LA SITA
PHP FUNCTIONS KUONYESHA TAREHE NA SAA:
Kwa kutumia php unaweza kuonyesha saa muda wowote kwa kutumia mistari michache ya code.
Katika php function inayotumika kwa ajili yakuonyesha tarehe na saa ni date(). kwa kutumia function hii una hiyari uonyesha tarehetu, ama siku tu, ama saa tu …. Katika php function inakupasa utambuwe haya:-
1.Y humaanisha mwaka yaani Year
2.m humaanisha mwezi yaani Month
3.d humaanisha siku yaani date
4.l humaanisha siku katka wiki
5.h humaanisha saa yaani hour
6.m humaanisha dakika yaani minute
7.S humaanisha sekunde yaani second
8.a humaanisha Ante meridiem (Am) na Post meridiem (Pm)
wacha tuone mifano hapo chini:-
1.Mfano wa kwanza
<?php
echo "today is", "<br><br>",
date("Y/m/d/l");
?>
Hii itakupa mwaka, mwezi, tarehe na siku katika wiki.
Kama unataka kuonyesha mwaka pekee, utaweka Y tu kwenye function
2.Mfano 2
<?php
echo "today is", "<br><br>",
date("Y");
?>
Hii itakupa mwaka tu
3.Mfano
<?php
echo "today is", "<br><br>",
date("m");
?>
Hii itakupa mwez tu
4.Mfano
<?php
echo "today is", "<br><br>",
date("d");
?>
Hii itakupa tarehe ya leo
5.Mfano
<?php
echo "today is", "<br><br>",
date("l");
?>
Hii itakupa jila la siku ya wiki ya leo kama ni juma tatu, ama jumanne ama vinginevyo
6.Mfano
<?php
echo "the time is " .
date("h:i:sa");
?>
Hii itakupa saa, dakika, sekunde na kama Am ama Pm.
Ukitaka kuonyesha saa tupu utaweza kufanya kama ilivyofanywa juu kwenye tarehe.
7.Mfano
<?php
echo "the time is " .
date("h");
?>
Hii itaonyesha saa tu.
SAA KWA ZONE
Changamoto utakayoipata kwenye php function iliyotumika hapo juu utaona kuwa masaa hayaposawa na ilvyo saa yako. Hii ni kutokana na kuwa time zone iliyotumika ni tofauti. Hivyo basi itakupasa kujuwa time zote yako ili uweze kupata saa sahihi. Kufanya hivi tutatumia function hii date_default_timezone_set()
Ili kuweka timezone, kwanza uweke region au bara kwa mfano tanzania ipo Africa kisha weka alama / kisha weka time zone. Kwa mfano Tanzania ipo kwenye timezone ya Nairobi hivyo utaandika Africa/Nairobi
8.Mfano
<?php
date_default_timezone_set("Africa/Nairobi");
echo "the time is " . date("h:i:sa");
?>
Hii itaonyesha saa kulingana na timezone ya East Africa, ambayo inachukuliwa nairobi.
COPYRIGHT KWENYE TOVUTI
Hivi umesha tembelea tovuti na blog, halafu chini utaona mwaka ilipoanzishwa mpaka mwaka wa sasa. Nikijuze kuwa ule mwaka wa sasa hubadilika automatiki, na hakuna haja ya kubadili, haya utayafanya kwa kutumia php. Mfano
9.Mfano
©: 2018 - <?php echo date("Y");
?>
Hii itakupa matokeo ©: 2018 - 2021
Tutajifunza zaidi kuhusu kalenda katika masomo yatakayofata.
Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo la 10 mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza kuhusu condition statement.
Soma Zaidi...Hii ni tafiti ambayo itakushangaza, kwa namna ambavyo matumizi ya AI yalivyo na athari kwenye uwezo wa kufikiri
Soma Zaidi...Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.
Soma Zaidi...Katika somo hili la 6 mafunzo ya HTML level 2, tutajfunza namna ya kugawa ukurasa wa wavuti wa html.
Soma Zaidi...Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 10. katika somo hili tutakwenda kuendelea namna ya kupangilia muonekano wa data zako kwenye database.
Soma Zaidi...Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi.
Soma Zaidi...Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array.
Soma Zaidi...Somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2. Katika somo hili utajifunza maana ya HTML pamoja na historia yake fupi.
Soma Zaidi...hili ni somo la sita katika mfululizo wa mafunzo ya HTML level 1. Katika somo hili tutajifunza mambo makuu matatu ambayo ni kuweka menyu, kuweka background color na kufanya faili lako liwe responsive.
Soma Zaidi...