image

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 3 (HTML basic level FOR BEGINNERS)

Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi.

HTML SOMO LA TATU
Karibu tena kwenye mafunzo ya HTML. Na hili ni somo la tatu. Kama bado hujalipata somo la kwanza na la pili, tumia link hapo chini kufunguwa masomo hayo. Katika somo hili la tatu tutakwenda kuelezea baadhi ya tag za HTML ambazo hutumika mara nyingi katika kuandika makala.

 

Katika somo lililopita tuliona maana ya tag, na namna ambavyo tag hufanya kazi. Tag zipo za kufungua ambazo huanzwa na alama hii < na zipo tag za kufunga ambazo huanzwa na alama hizi </. pia katika somo lililotangulia tuliona maana ya element katika html. Element tuliona kuwa ni mkusanyiko wa tag na maudhui yaliyo ndani ya tag kwa mfano <p> hello </p> katika code hii kuna tag ya kufungua ambayo ni <p> na kuna maudhui ambayo ni “hello” pia kuna tag ya kufunga ambayo ni </p> kwa pamoja tunapata element.

 


Tag zipo nyingi sana ambazo tunazitumia katika uandishi. Kama unavyotumia microsoft katika kuandika basi kula unachokifanya pale kuna tag yake. Kwa mfano unapopigia msitari, kuna tag ya kufanya hivyo. N.k

 

TAG 25 MUHIMU KATIKA UANDISHI
1.<h1> kwa ajili ya heading. Tag hizi huanzia <h1> hadi <h6>
2.<p> kwa ajili ya kuandika paragraph
3.<b> kwa ajili ya kubold
4.<u> kwa ajili ya kupigia msitari
5.<hr> kupiga msitari kwenye faili, bila ya kupigia herufi maalumu
6.<i> kwa ajili ya kufanya italic
7.<sup> kwa ajili ya kuandika vipeo na vipeuo
8.<sub> kuandika kama vipeua vile vya chini kama unavyoandika alama za kiemikali
9.<code> kwa ajili ya kuandika code text
10.<tt> kwa ajili ya kuandika tipewriter text
11.<small> kwa ajili ya kuandika maandishi madogo
12.<em> kwa ajili ya kuwekea mkazo maandishi (hufanana na kubold)
13.<strong>Kwa ajili ya kusisitiza zaidi (hufanana na kubold)
14.<mark>Kwa ajili ya kumark maandishi
15.<s>kwa ajili ya kukata maneno
16.<q> kwa ajili ya kunukuu maneno yaani kukata msitari na kuanza mpya
17.<br> kubreak line yaani unakata msitari na kuanza kuandika msitari mpya. Mfan wake ni kama unavyotumia batani ya enter kwenye keyboard za simu ama kompyuta wakati wa kuandika.
18.nbsp kwa ajili ya kuruka nafasi ama
19.<a> kwa ajili ya kuweka link
20.<button> hutumika kuweka batani
21.<pre> hutumika kuandika mashairi ama kuonyesha text kama zilivyo kutoka kwenye faili la html
22.<form> kwa ajili ya kutengeneza fomu
23.<img hutumika katika kuweka image
24.<div> kufanya text block
25.<span> hutumika kugroup maandishi kwenye paragraph.

 


Unaweza kuanza kuzifanyika kazi tag hizi. Usisahau kufunga tag hizo. Katika somo linalofata tutaona namna ambavyo tag zote hizi zinavyofanya kazi kwenye faili lako. Endelea kufuatilia somo hili. Lengo la tag hizi ni kukusaidia kuandika faili lako la html na likakuletea matokeo kama vile faili limeandikwa kwenye word processor kama microsoft word ama wps n.k

 

Unawezakuanza kuzifanyia kazi tag hizo hapo juu. Kwa kutumia mifano iliyotangaliak katika somo lililopita, chekilinki hapo juu ya masomo yaliyopita, unaweza kufany amazoezi mwenyewe bila hata ya kusubiri somo lijalo. Ningependa sana kama utashea screenshot za mazoeziyako kupitia koment.

 

Ndugu msomaji, nikupe siri ya mwanzo wa somo hili. Sababu ya kuanzisha somo hili I baada ya mafunzo ya kutengeneza Android App kwa kutumua simu. Tulishaanza hatuwa ya kwanza na tumetengeza Appp kwa kutumia link. Sasa changamoto ni kuwa somo lililotakiwa kufata ni kutengeneza App yenye ubora. Hapa ndipo ikaja haja ya angalau kujifunza HTML ili tuweze kutengeneza App nzurikwa kutumia data zetu wenyewe na kwa namna tunavyotaka.

 

Hivyo ni matarajio yangu baada ya mafunzo haya ya siku chache (basic) tutarudi tena kwenye darasa letu la kutengeneza App kwa kutumia simu. Kisha somo hili litaweza kuendelea (advanced) baada ya kuonekana haja zaidi. Kwa wale walio na haja ya kutengeneza website zao ama blog, tutaendelea kuwa pamoja nao katika mafunzo haya.

 

Mafunzo haya yamekujia kwa hisani ya:-
Bongoclass.com
Web: www.bongoclass.com
Email: mafunzo@bongoclass.com

 

 

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 929


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Mafunzo ya database MySQL - DATABASE somo la 6
Huu ni muendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 6. Katika somo hili tutakwenda kuona jinsi ya kutengeneza table kwa kutumia MySQL na kwa kutuma SQL. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 2 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo. Soma Zaidi...

Mafunzo ya php level 1 somo la nne (4)
somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia. Soma Zaidi...

Mafunzo ya html level 2 (html full course for beginners)
haya ni mafunzo ya HTML level 2 kwa wenye kuanza. Mafunzo haya ni muendelezo wa level 1 html. Katika course hii utajifunza mengi zaidi lu;iko level1 pia tutazidi kuboresha project yetu. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 5 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 5)
Karibu tena katika mafunzo haya ya html level 2 na hili ni somo la 5. Katika somo hili utajifunza zaidi kuhusu kuweka style kwenye html file. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 1 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Haya ni mafunzo ya HTML kwa wanaoanza level ya kwanza, na hili ni somo la kwanza katika masomo 8 yatakayokujia katika mtiririko wa course hii. Soma Zaidi...

Mafunzo ya DATABASE MYSQL na SQL somo la 1
Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo. Soma Zaidi...

PHP level 1 somo la tano (5)
Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 8 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Katika somo hili la 8 mafunzo ya html level 8 utajifunza jinsi ya kuhost project ya html na kuwa live, watu wakaipitia na kusoma maudhui yake. Soma Zaidi...

Mafunzo ya database MySQL somo la 3
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza. Soma Zaidi...

PHP level 1 somo la tisa (9).
Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array. Soma Zaidi...

Mafunzo yz database MySQL database somo la 12 (final)
Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database Soma Zaidi...