Hapa utajifunza utofauti kati ya php constant na variable. Na hili ni somo la nane katika mfululizo wa masomo haya ya php level 1.
SOMO LA 8
PHP COSTANTS
Constant ni jina linalowakilisha thamani fulani. Thamani hi haiwezi kubadilika wakti wa code kufanya kazi. Constant inaweza kuanzwa kwa herufi lakini si kwa alama ya dola $ kama ilivyo kwenye variable.
Jinsi ya kuweka constant kwenye php.
Utaanza kuweka neno define likifuatiwa na mabano mfano define() ndani ya mabano utaweka jina la constant na thamani vyote vinatakiwa viwekwe kwenye funga semi.
Mfano:-
<?php
define("tunda", "Tunda ni zao la mti linalopatikana baada ya uwa");
echo tunda;
?>
Hii itakupa matokeo:
Tunda ni zao la mti linalopatikana baada ya uwa
Constant hutumika katika kuweka data ambazo hazitakiwi kubadilika wakati wa kuchakata code. Kwa mfano password na database connection.
KUTUMIA CONSTANT KWENYE PHP FUNCTION
Unaweza kutumia constant kwenye code zako zote yaani constant moja unaweza kuitumia katika code zako bila kujali ipo wapi. Kwa urahisi ni sawa na kusema unaweza kutumia constant hata kwenye function ama kwingineko.
Mfano:-
<?php
define("salamu", "halo hujambo");
function mfano() {
echo salamu;
}
mfano();
?>
Hii itakupa matokeo
Halo hujambo
Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
haya ni mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 9. katika soo hili utajifunza namna ya kusoma ama kutumia taarifa zilizomo kwenye DATABASE.
Soma Zaidi...Karibu tena katika somo la nne la mafunzo ya HTML level2 html full course for beginners. Katika somo hili utajifunza kuhusu attributes na namna zinavyofanya kazi
Soma Zaidi...Katika somo hilivutajifunza namna ya kutumia HTML form. Namna ya kuookea taarifa kutoka kwenye madodoso ya html form.
Soma Zaidi...Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database
Soma Zaidi...Hii ni project ya HTML ambayo imetengenezwa kulingana na mafunzo ya HTML level1. Tunatarajia project hii kuboreshwa kadiri mafunzo yanavyozidi kusonga mbele.
Soma Zaidi...Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi.
Soma Zaidi...katika somo hili la tano kwenye mafunzo ya HTML level 1 utajifunza jinsi ya 1.Kuweka picha 2.Kuweka rangi 3.Kuweka linki 4.Kupangilia position na alignment ya maandishi 5.Kuongeza ukubwa wa herufi 6.Kukoment
Soma Zaidi...Katika somo hili la 6 mafunzo ya HTML level 2, tutajfunza namna ya kugawa ukurasa wa wavuti wa html.
Soma Zaidi...Karibu kwenye mafunzo ya PHP level 1 na hili ni somo la kwanza. Hapa utajifunza maana ya php, inavyofanya kazi pamoja na historia yake kwa ufupi
Soma Zaidi...