Mafunzo ya database mySQl database somo la 11

huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database klwa kutumia MySQL na hili ni somo la 11. katika somo hili tutaendelea kujifunza mpangilio wa muonekano wa data kwenye database.

Katika somo lililotangulia tumejifunza amna a kupangilia taarifa za kwenye databse. Tuliona namna ya kutumia ORDER BY. Isha tukapanga data zetu kutoka kubwa kwenda ndogo na kinyume chake. Sasa katika somo hili tutatkwenda kuendelea na nnamna ya kupangilia data hizo ila kwa kutumia WHERE .

 

Kwa nini tunatumia where ?

Tunatumia WHERE endapo tuna masharti yanatakiwa yafikiwe ili data kuonekanna. Kwa mfano unataka kusoma menu zote ambazo gharama yake ni zaidi ya 1000. hapa hili tunaita ni sharti ama condition. Sasa ili sharti hili liweze kufanya kazi kwenye SQL tunatumia where.

 

1. Mfano wa kwanza

Tunahitaji kusoma data zote ambazo price yake ni sawa na  1000.

Kufanya hivyo tutatumia alama ya = mbele ya where. Hivyocommand nzima itaonekana.

SELECT * FROM `menu` WHERE price =1000 

hapo menu itakayoonekana ni ile tu ambayo proce yake ni sawa na 1000.

 

2. Mfano wa pili

Tunataka kusoma data ambazo id yake ni 3, 4, na 8. yaani data tu zenye id hizo ndizo tunataka kuziona na si nyinginezo. Hivyo tunatarajia kuwa na row tatu tu. Kufanya hivyo tutatumia OR kwa maana au. Yaani eidha id iwe 3 au id iwe 4 au id iwe 8. Na command yote itaonekana hivi

SELECT * FROM `menu` WHERE id =3 OR id =4 OR id =8;  pia unweza kuondoa nyota na kupunguza column

SELECT name, price FROM `menu` WHERE id =3 OR id =4 OR id =8;

 

3. Mafno wa tatu

Chukulia mfano kwenye menu kuna ugali mbili. Kuna ugali nyama abayo ni 1500 na kuna ugali ng’onda ambaypo ji 1000. sasa mimi nataka kusoma ile ambayo ni ugali nyama ya 1500. kumbuka zote ni ugali na kwenye menu zitanasomeka hivyo hivyo. Ili kuona ya ugali 1500 tu tunatakiwa tutumie AND yaani tuselect ugali lakini kwa ulazima kuwa na id yake iwe 1. ambapo kwenye menu yetu id 1 ni ugali hivyo itakuwa hivi:-

SELECT * FROM menu WHERE name = 'ugali' AND id =1

 

Kuna jambo hapa unatakiwa ulijuwe. Tunapotumia string (sting ni mkusanyiko wa herufi na namba, rejea mafunzo ya php) value inatakiwa ikae ndani ya alama za kufnga na funguwa semi ‘’ kama ulivyo kwenye mfano 'ugali'.

 

4. Tofauti ya AND na OR. 

Unapotumia AND maana yake ni lazima masharti yafikiwe ili data kuonekana. Ila unapotumia OR hata shart moja likifikiwa data zitaonekana. Kwa mfano kwenye mfano namba 2 hapo hata kama kusingekuwa na id 3 data zingeonekana lakini kama tungetumia AND endapo id tatu isingekuwepo kwenye database yetu data zote zisingesoma.

 

5. Mfano wa nne

Tunahitaji kusoma menu ambazo tu majina yake yameanziwa na herufi u. chukulia mfano kuna orodha ya majina ya vyakula 50 kwenye hoteli moja kubwa sana. Sasa nataku kuona vyakula vinavyoanziwa na herufi u tu, hapo nikiwa naamini nitaona bei ua ugali kwa haraka zaidi tofauti na kuanza kusoma kutoka kwanzo hadi mwisho.

 

Kufanya hivi tutatumia LIKE kisha tutaweka hiyo heru u kikifuatiwa na alama ya asilimia %.  na ikiwa unahitaji kufatuta menu iliyoishiwa na herufi u basi alama ya asilimia % utaiweka mwanzo mfano %u. mfano huu pia utaweza kuutumia kama unataka kusearch kitu kwenye database ambacho kinaanziwa na herufi fuani. Hivyo kulingana na mfano wetu command itakuwa hivi:-

SELECT * FROM menu WHERE name LIKE 'u%'

 

Tutajifunza zaidi somo hili tutakaposoma namna ya kutafuta kitu kwenye database. Hila unaweza kutumia mfano huu pia kutafuta kitu kama mpangilio hapo unavyouona. Mfano unataka kutafuta neno supu  utaweka ‘supu%’

 

6. Mfano wa tano

Kwa kutumia SQL pia unaweza tumia mathematical operation kama >, <, !=, == na nyinginezo. Hapa nitatumia < na >. kwa ufupi > humaanisha kubwa kuliko na < humaanisha ndogo kuliko. Hapa nitatuia mifano miwili tu ya > na < .

 

A. Tunahitaji kuona menu ambazo price zake ni kubwa kuliko 1000 hapa tutatumia > .hivyo menu itakayokuja ni ile tu ambayo price yake imezidi 1000. hivyo itakuwa hivi

SELECT *  FROM menu WHERE price >1000

 

B. Tunataka kuona menu ambazo price yake ni ndogo kuliko 900. hapa tutatumia <, hivyo menu tutakazoona ni zile tu ambazo price yake haijafika 900. hivyo itakuwa hivi:-

SELECT *FROM  menu WHERE price <900

 

Tukutane somo la 12 tutajifunza kanuni kadhaa za kihesabu kwa kutumia SQL. Tafadhali usikose somo la 12 kwani ndio somo letu la mwisho wa course hii ta mafunzo ya database kwa kutumia MySQl.

 

 

Mafunzo haya yamekujia kwa Ihsani ya bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: mafunzo@bongoclass.com

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tehama Main: Jifunze File: Download PDF Views 1183

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Mafunzo ya php level 1 somo la kwanza (1)

Karibu kwenye mafunzo ya PHP level 1 na hili ni somo la kwanza. Hapa utajifunza maana ya php, inavyofanya kazi pamoja na historia yake kwa ufupi

Soma Zaidi...
Php level 1 somo la saba (7)

Hili ni somo la saba, mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika function yako mwenyewe.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya DATABASE - MySQL somo la 7

Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML level 1 somo la 7 (HTML basic level FOR BEGINNERS)

Hii ni project ya HTML ambayo imetengenezwa kulingana na mafunzo ya HTML level1. Tunatarajia project hii kuboreshwa kadiri mafunzo yanavyozidi kusonga mbele.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya php level 1 somo la nne (4)

somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 3 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 3)

Hili n somo la tatu katka muendelezo wa mafunzo ya HTML LEVEL 2 kwa lugha ya kiswahili. Mafunzo haya yanakujia kwa Ihsani ya bongoclass

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza (basic level)

Huu ni utangalizi wa mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza level ya kwanza kwa lugha ya kiswahili. Haapa utapata msingi wa kuweza kutengeneza tovuti na blog.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya php level 1 somo la pili (2)

hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo haya ya php level 1 na hapa utajifunza namna ya kuandika faili klako la kwanza la php.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML level 1 somo la 2 (HTML basic level FOR BEGINNERS)

Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.

Soma Zaidi...
PHP level 1 somo la sita (6)

Katika somo hili la php level 1 somo la 6 utajifunza namna ya kutumia tarehe yaani function date() kwenye PHP

Soma Zaidi...