Madhara ya Tiba mionzi

Post hii inahusu zaidi madhara ya Tiba mionzi kwa wagonjwa wa saratani, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wanaotumia mionzi katika matibabu ya saratani.

1. Kupoteza hamu ya chakula.

Hii ni mojawapo ya madhara ambayo utokea kwa watumiaji wa mionzi kwa sababu ya kuwepo kwa dawa kwenye damu usababisha kuingilia mfumo wa  hamu ya kula kwa hiyo mgonjwa ushindwa kula, kwa hiyo mgonjwa anapaswa kula kidogo kidogo na kwa kila mara na pia anapaswa kula vyakula kama vile supu  na vyakula vingine vilaini Ili aweze kuruhusu dawa kufanya kazi maana dawa bila chakula mambo hayaendi vizuri.

 

2. Mgonjwa usikia uchovu mara kwa mara.

Kwa sababu mionzi uharibifu seli zinazosababisha saratani na vile vile zile ambazo ni nzima nazo uharibiwa na mionzi kwa hiyo  tunajua kabisa maisha yetu msingi wake ni seli kwa hiyo seli zikifa  bila kufikia mda wake na mambo mengine mwilini yanakwama ndo maana mtu uhisi uchovu kwa hiyo wanaotumia mionzi wanapaswa kupumzika kwa mda wa kutosha, kutembea walau dakika Kumi na Tano kwa siku na kunywa maji mengi, kula chakula Cha kutosha Ili kuupatia mwili nguvu.

 

3.Mabadiliko ya ngozi.

Kwa wagonjwa wanaotumia mionzi huwa na mabadiliko kwenye ngozi zao , pengine ngozi ubadilika na kuwa pinki, nyeusi, kuhisi moto kwenye ngozi, ngozi kuwa kavu, kuwasha na ngozi kuwa na upele au malengelenge kwa mgonjwa anayetumia mionzi akiona dalili kama hizi hasiogope Bali achukue dawa za kawaida zinazotumika kutibu magonjwa ya ngozi na pia apate ushauri wa daktari Ili kuweza kujua Cha kufanya maana madhara mengine kwenye ngozi huwa yanatisha na kumnyima mgonjwa amani.

 

4. Mgonjwa huisi kichefuchefu.

Kwa sababu dawa hizi za mionzi  zinaharibu seli na pia uingilia mfumo wa chakula na kumfanya mgonjwa kutaka kutapika kila kitu, kwa hiyo mgonjwa anapaswa kukaa woman Ili asitapike, pia anapaswa kula chakula kidogo kidogo kwa wakati b tofauti na pia anapaswa kujiadhari na vyakula vile ambavyo huwa havipendelei Ili kuepuka kutapika kwa kufanya hivyo mgonjwa ataweza kula chakula na dawa zitaweza kufanya kazi.

 

5. Tukumbuke kuwa mionzi huua seli zinazosababisha saratani na pamoja na zile ambazo ziko kawaida na pia mwili wa binadamu unapaswa kuwa na seli zinatosha Ila kwa sababu ya magonjwa seli zinaharibika kwa mionzi kwa hiyo wagonjwa hawa wanahitaji uangalizi wa karibu na kupewa chakula chenye virutubisho vyote Ili waendelee kuishi na pia jamii inapaswa kuwasaidia na kuwapa ushirikiano wa karibu.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Author Tarehe 2021/12/23/Thursday - 07:30:33 pm     Share On Facebook or WhatsApp Imesomwa mara 1735

Post zifazofanana:-

Yanayoathiri afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mambo yanayoathiri afya Soma Zaidi...

Utaratibu wa lishe kwa vijana
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa vijana Soma Zaidi...

Msaada kwa aliye na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
Posti hii inahusu zaidi msaada kwa aliye na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni huduma maalumu ambayo utolewa kwa mtu ambaye ana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo. Zifuatazo ni huduma maalumu kwa mwenye uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo. Soma Zaidi...

Asili ya vyakula vya madini ya zinki
Post hii inahusu zaidi asili ya madini ya zinki, hii inaonesha sehemu gani tunaaweza kupata madini ya zinki. Soma Zaidi...

Dalili za fangasi Mdomoni.
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za fangasi Mdomoni kwa watoto, vijana, watu wazima na mama wanaonyonyeshwa. Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamini na faida zake
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamini na faida zake Soma Zaidi...

Dalili za maumivu ya uti wa Mgongo
Posti hii inahusu zaidi dalili za uti wa mgongo ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uti wa Mgongo. Soma Zaidi...

Malengo ya kuwahudumia watoto chini ya miaka mitano
Posti hii inahusu malengo ya kuwahudumia watoto chini ya miaka mitano, huduma hii ilianzishwa na WHO na UNICEF mwaka 1990 ili kuweza kuzuia Magonjwa na kuwapatia watoto lishe pamoja na hayo walikuwa na malengo yafuatayo. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa kiseyeye na dalili zake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa kiseyeye na dalili zake Soma Zaidi...

Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia.
Postii inafundisha maandalizi ya mama kwa ajili ya kujifungulia hii Ni muhimu Sana kwa wale ambao hawajawahi kujingua Ni mara yao ya kwanza wanatakiwa kujua na kuelewa vifaa na mahitaji kujifungulia na kwa wale wanaohudhuria clinic huwa wanafundisha. Soma Zaidi...

Kazi ya metronidazole
Posti hii zaidi kazi ya Dawa ya metronidazole katika kutibu Minyoo, ni aina ya Dawa ambayo imetumiwa na watu wengi wakaweza kupona na kuepukana na minyoo. Zifuatazo ni baadhi ya kazi za metronidazole. Soma Zaidi...

Watu ambao hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango
Post hii inahusu zaidi watu ambao hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango, Ni watu ambao Wana matatizo mbalimbali endapo wakitumia wanaoweza kuleta madhara mbalimbali. Soma Zaidi...