Posti hii inahusu dawa ya salbutamol na kazi yake ya kutibu ugonjwa wa Asthma, ni dawa mojawapo ambayo imetumia na watu wengi na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo zifuatazo ni kazi ya Dawa hii ya salbutamol katika kutibu Asthma.
Kazi za Dawa ya sulbutamol.
1. Sulbutamol ni dawa ambayo usaida katika kutibu Asthma na matatizo yote yanayohusiana na mfumo wa hewa, ufanya kazi yake kwa kwa wagonjwa wenye matatizo ya kubanwa kifua na Asthma, ufanya kazi hiyo kwa kuifanya mishipa au misuli ya kwenye mfumo wa hewa kulainika na kufanya hewa kupita kwa urahisi, tukumbuke kwamba kama mgonjwa amebakwa na kifua misuli ya kwenye kifua mara nyingi huwa imebana na kumfanya mgonjwa kuumia na kupumua kwa shida kwa hiyo kwa kutumia sulbutamol misuli ya mgonjwa ulainika naye upumua kawaida.
2. Pia hii dawa uwezo kuwa kwenye mifumo mbalimbali , inaweza kuwa kwenye hali ya vidonge, au kwenye mfumo wa maji ambayo utumiwa sana na watoto, na pengine inaweza kutumiwa kwa kumpulizia mgonjwa kama anaumwa kupitia mdomoni au kwa maelezo zaidi wataalamu wa afya ndio wanaweza kukupatia utaratibu kadri ya hali halisi ya mgonjwa.
3. Dawa hii uweza kutumiwa ila si kwa watu wote hasa wale walio na Mzio au akeji na dawa hii hawapaswi kuitumia na mtu akitumia dawa hii hapaswi kutumia dawa yoyote ya maumivu hasa hasa Asprin. Na pia dawa hii inapaswa kutumiwa kwa uangalifu kwa watu wenye matatizo ya moyo na presha kwa sababu dawa inaweza kupandisha presha juu na mapigo ya moyo yanaweza kwenda kwa mbio, kwa hiyo kabla ya kutumia dawa hii mgonjwa anapaswa kupima presha kwanza na mapigo ya moyo ili tusije kuleta matatizo mengine zaidi.
4.Tunapotumia dawa hii tunategemea kupata maudhi madogo madogo kama vile mapigo ya moyo kwenda kwa mbio, maumivu ya kichwa, kupata usingizi kwa shida na pengine presha kubwa juu hii ni kwa sababu ya mishipa ya damu ambayo imeingiliwa na dawa usababisha mishipa ya damu kupitisha damu kwa haraka zaidi, kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hii wakiona hayo yote wasishangae ni sehemu ya kawaida ya matokeo ya dawa.
5 . Kwa upande wa watoto wadogo wanapaswa kupewa 0.1mg kila baada ya maasaa manne na kwa watu wazima wafuate utaratibu wa daktari na kwa wanawake wenye mimba inabidi wapewe kwa njia ya kuvuta tu kwa sababu njia nyingine zinapelekea kuwepo kwa matatizo ya moyo hasa kwa akina mama. Kwa hiyo dawa hii ni ya muhimu sana na imewasaidia watu wengi na tusitumie kiholela Bali tusikilize ushauri wa daktari na wataalamu wengine wa afya.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Post hii inahusu zaidi dawa zinazofanya kazi ya kupunguza maumivu kwa kawaida dawa hizi ufanya kazi kwa kupitia kwenye mfumo wa fahamu.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukuletea dawa za kutibu ugonjwa wa macho
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya ALU kama Dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ,ni dawa ambayo utumiwa na watu wengi kwa matibabu ya ugonjwa wa Malaria.
Soma Zaidi...Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya macrolide ni mojawapo ya dawa ya kutibu au kupambana na bakteria na upambana na bakteria wafuatao streptococcus pyogenes, staphylococcus aureus na haihusiki na haemophilia influenza ambao usababisha maambukizi kwenye mfumo w
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya isoniazid katika mapambano na kifua kikuu, tunafahamu kabisa kwamba kifua kikuu ni hatari katika jamii kwa hiyo dawa ya isoniazid ni mkombozi katika mapambano na kifua kikuu.
Soma Zaidi...Dawa za vidonda vya tumbo na tiba zake zinapatikana hapa. Soma makala hii kwa ufanisi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya paracetamol katika kutuliza maumivu, ni Aina ya dawa ambayo utumiwa sana katika kutuliza maumivu kwa wagonjwa.
Soma Zaidi...