Madhara ya kutotoa huduma kwa Mama anayevuja damu baada ya kujifungua

Posti hii inahusu zaidi Madara ya kutomsaidia mama anayetokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.

Madhara ya kutokwa dama baada ya kujifungua.

1. Kwanza kabisa tunafahamu kwamba mwili wa binadamu umejengwa na damu, damu ikipungua madhara mengi yanaweza kutokea, pia kwa akina Mama wakiwa na mimba usababisha damu kupungua kwa sababu ya matumizi ya Mama na mtoto. Kwa hiyo wakati wa kujifungua Mama upoteza damu na damu ikipotea zaidi usababisha madhara makubwa kama vile,

 

2. Kuwepo kwa upungufu wa damu ambapo kwa kitaalamu huitwa Anemia.

Kwa hiyo ikitokea Mama akapoteza damu nyingi anaweza kupata upungufu wa damu mwilini ni vizuri kabisa hali hii ikitokea Mama anapaswa kuongezewa damu haraka Ili kuepuka tatizo hili la upungufu wa damu. Kwa hiyo wahudumu wa afya wanapaswa kufahamu hilo na kuacha uzembe ambao usababisha kupoteza damu.

 

3. Mama akipoteza damu anaweza kuzimia na kuishiwa madini mwilini.

Kwa kawaida tunajua madini mbalimbali yapo kwenye damu ambayo usambazwa kutoka sehemu mbalimbali za mwili na kuweza kuupatia mwili nguvu.kwa hiyo damu ilipungua usababisha nguvu kuisha mwilini hali inayoweza kusababisha mama kuzimia baada ya kupungukiwa kwa kiwango kikubwa cha damu.

 

4. Kifo kinaweza kutokea ikiwa Mama hajahudumiwa ipasavyo.

Kwa wakati mwingine kama Mama ana matatizo ya kutokwa na damu kwa mda mrefu bila msaada wowote, mama anaweza kufariki.

Kwa hiyo wauguzi na wahudumu wa afya wanapaswa kufahamu hilo na kuhakikisha kuwa Mama anapata dawa zote na huduma zote ili kuweza kuokoa maisha ya Mama na mtoto.

 

5. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kuhakikisha kuwa ikiwa Mama ataonyesha dalili yoyote ya kutokwa kwa damu anapaswa kuhudumiwa kwa nguvu zote ili kuokoa maisha yake na pia kwa wale wenye sababu zinazoeleweka wanapaswa kutibiwa mapema ipasavyo



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/17/Tuesday - 09:39:22 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 774


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-