Fahamu dawa ya tetracycline katika kupambana na bakteria

Post hii inahusu zaidi dawa ya tetracycline katika kupambana na bakteria,ni mojawapo ya antibiotics au anti bacteria ambayo upambana na bakteria kama tutakavyoona hapo mbeleni.

Fahamu dawa ya Tetracycline katika kupambana na bakteria.

1 . Tetracycline ni mojawapo ya dawa ambazo usaidia katika matibabu ya kupambana na bakteria ni  muunganiko wa dawa tatu zikiwemo penicillin na streptomycin na zikiungana ndio zinaitwa tetracycline, muunganiko wa dawa hizi tatu huwa na sifa sawa na zinazofanana na mara nyingi utolewa kwa kumezwa mdomoni na pia uingia kwenye mmengenyo wa chakula na baadae kupitia kwenye mzunguko wa damu  hatimaye  kupambana na bakteria sehemu yoyote walipo.

 

2. Kwa upande mwingine aina ya dawa ya Tetracycline hydrochloride uweza kupitia kwenye mishipa ya damu na kufanya kazi kama zile ambazo hazijapitia kwenye mishipa ya damu, dawa hizi za tetracycline zikifika kwenye mwili na kukutana na bakteria zinazuia kutengenezwaa kwa protini ndani ya bakteria kitendo ambacho ufanya bakteria huyo kushindwa kuishi kwa sababu hawezi kuishi bila kuwepo kwa protein hiyo.

 

3. Kwa kawaida dawa hizi za tetracycline utibu magonjwa mbalimbali kama vile Chlamydia, kaswende na kisonono kwenye watu walio na aleji na penicillin kwa kawaida dawa ambayo imependekezwa kutibu kaswende na kisonono ni benzyl penicillin lakini Kuna watu wenye magonjwa haya kaswende na kisonono na Wana aleji na penicillin kwa hiyo dawa yao ni tetracycline ambayo na yenyewe utibu magonjwa hayo ya kaswende na kisonono,.

 

4. Dawa hii inaweza kutumiwa na watu mbalimbali ila haipaswi kutumiwa na wote wenye aleji na tetracycline , watoto chini ya miaka minane nao hawapaswi kutumia kwa sababu Ina tabia y kuharibu meno kwa sababu uingia hata kwenye fizi,wakiona mama wenye mimba changa hawapaswi kutumia dawa hii na kwa wale wanaonyonyesha hawaruhusiwi kutumia dawa hii mpaka waache kumnyonyesha hapo wanaweza kutumia dawa hii.

 

5. Pia Kuna wale wenye matatizo ya Figo, matatizo ya moyo na pia kwa wenye matatizo ya sukari yote ya kupanda na kushuka wanapaswa kutumia dawa hii ila wawe chini ya uangalizi ikiwa mtu Hana uangalizi asitumie dawa hii kwa sababu Ina tabia ya kuongeza tatizo au ikiwezekana watumie dawa za antibiotics nyingine tofauti na hizo.

 

6. Pia dawa hii uingiliana na dawa nyingine na kumaliza dawa nyingine  nguvu kwa mfano kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa ule wenye homoni au kichocheo cha estrogen, dawa hizi za tetracycline umaliza nguvu estrogen na mama anaweza kubeba mimba huku anatumia njia ya uzazi wa mpango kwa hiyo basi kwa watumiaji wa uzazi wa mpango ni vizuri kabisa kupata ushauri wa wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa hii Ili kuepukana na mimba zisizotarajiwa .

 

7. Pia kwa wale watumiaji wa madawa ya kupunguza asidi mwilini hasa we ye vidonda vya tumbo pia dawa hizi uingiliana sana na kalsium pamoja na magnesium na pia kwa watumiaji wa dawa za kuongeza madini ya chuma na wenyewe dawa hizi uingiliana na dawa za tetracycline kwa hiyo kabla ya kutumia dawa hii ya tetracycline ni vizuri kabisa kupata ushauri wa wataalamu wa afya Ili kuepuka madhara zaidi au kwa wakati mwingine unaweza kutumia dawa nyingine na unatumia tetracycline unakuwa unafanya kazi Bure.

 

8. Vile vile na dawa hizi za tetracycline huwa na maudhi madogo madogo kama vile kuongeza spidi ya majimaji yaliyo kwenye ubongo na kusababisha kizunguzungu na pengine kuona maruwe ruwe, kwa sababu dawa hii uweza kupitia kwenye mmengenyo wa chakula mgonjwa uweza kuhisi kichefuchefu na kutapika, maambukizi kwenye Koo na pia mgonjwa anaweza kuwa na miwasho pamoja na kujikuna pia kwa watumiaji wa mda mrefu wanaweza kuwa na matatizo katika kuona.

 

9. Haya ni baadhi ya maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kutokea ikiwa maudhi haya yamepita kiasi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya Ili kuweza kutafuta tiba na kuepuka matatizo zaidi, pia dawa hizi zibatibu magonjwa mengi na kwa wakati mwingine zinapatikana kwenye maduka au famasi zetu ni vizuri, ila kwa sababu Zina maudhi mengi na zinaingiliana na dawa nyingi ambazo watu wanazozitumia mara kwa mara kwa mfano uzazi wa mpango na vidonda vya tumbo ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa hii.

 

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 3478

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

mpenzi wangu nimeshiriki nae tendo la ndoa akiwa siku zake za hatar kwa siku 3 lakin hajashika mimba tatizo linaweza kuwa ni nini?

Kupata ujauzito hufungamana na mambo mengi ikiwepo afya vya wawili yaani me na mume na mengineyo. Unaweza kushiriki sikuvhatari na usiupate mimba. Postivhii ibakwendavkukufahamisha undani wa jambo hili.

Soma Zaidi...
Mimi Nina tatizo kila nkishika mimba huwa zinatoka tu ni mara 5 Sasa nifanyaje?

Mimba inaweza kutoka kutokana na maradhi, majeraha ama misukosuko mimgine. Kutoka kwa mimva haimaanishi ndio mwisho wa kizazi.

Soma Zaidi...
Kazi na mdalasini katika kutibu matatizo ya homoni.

Posti hii inahusu zaidi kazi ya mdalasini katika matibabu ya homoni kwa wanawake.

Soma Zaidi...
Njia za kufanya ili kuepukana na tatizo la kutokwa na majimaji kwenye uume

Posti hii inahusu zaidi njia ambazo mtu anapaswa kutumia ili kuweza kupunguza tatizo hili kisiweze kutokea na pia kama jamii ikishirikiana kwa pamoja tunaweza kuepusha kwa kufanya yafuatayo.

Soma Zaidi...
Mimi nilipima na kipimo mwenyewe nkakuta mistari miwili iliokoza lkn nikifanya tendo nakua naumia sana tatizo ni Nini docta

Je anapatwa maumivu 😭 makali wakati wa tendo la ndoa ama ukiwa katika hedhi? Soma makala hii hadi mwisho

Soma Zaidi...
UTI na ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa UTI kwa wajawazito

Soma Zaidi...
Utaratibu kwa wajawazito na wanaonyonshesha wakiwa na virusi vya ukimwi na ukimwi

Je kuna madhara kwa mwenye virusi vya ukimwi kunyonyesha ama kubeba mimba, na nini afyanye kama ameshabeba mimba ama kama ananyonyesha

Soma Zaidi...