Sababu za mfuko wa kizazi kushindwa kisinyaa.

Sababu za mfuko wa kizazi kushindwa kisinyaa.

Posti hii inahusu zaidi sababu za mfuko wa kizazi kushindwa kisinyaa, ni sababu ambazo utokea kwa akina Mama wengi kadri ya wataalamu wametafuta asilimia kuwa asilimia sabini ya wanawake mifuko yao ya kizazi kushindwa kisinyaa.

Sababu ya mifuko ya kizazi kushindwa kisinyaa.

1. Kwa kawaida Mama akimaliza kujifungua hatua inayofuata ni kutoa kondo la nyuma  na kutoa dawa ya oxytocin Ili kuweza kusaidia  kusinyaa kwa mfuko wa kizazi wanawake wengine  mfuko wa kizazi  hausinyai kwa sababu mbalimbali kama tutakavyoziona hapo chini na mfuko wa kizazi usiposinyaa usababisha kutokwa kwa damu nyingi na kusababisha upungufu wa damu kwa akina Mama au kama hakuna matibabu kifo kinaweza kutokea.

 

 

2. Sababu ya mfuko wa kizazi kushindwa kisinyaa usababishwa na uchungu kuwa wa mda mrefu na mtoto hatoki tumboni, hali hii usababisha mfuko wa kizazi kuendelea kutaanuka sana na kusababisha kutosinyaa baada ya Mama kujifungua. Kwa hiyo wakunga na wahudumu wengine ni vizuri kuona dalili za mapema Ili kuweza kunisaidia Mama pale uchungu unapotumia mda mrefu kuliko kawaida.

 

3.  Kushindwa kumhudumia Mama vizuri hasa pale anapojifungua na kumchoma dawa ya oxytocin Ili kusaidia uterus iweze kusinyaa.

Kwa wakati mwingine hii sindano usahaulika au kuchomwa vibaya hali inayosababisha mfuko wa uzazi kushindwa kisinyaa na kusababisha kuendelea kuwepo kwa damu baada ya kujifungua.kwa hiyo wauguzi na wahudumu wanapaswa kujiandaa mapema Ili kuweza kuwasaidia akina Mama waweze kujifungua salama bila kutokwa na damu nyingi.

 

 

4.  Kutanuka kwa uterus.

Kwa wakati mwingine Kuna tatizo la kutanuka kwa mfuko wa uzazi hasa hasa kwa wanawake wenye matumbo makubwa wako kwenye hatari ya kupata tatizo hili kwa sababu mfuko wa uzazi unakuwa umetanuka sana hali inayosababisha mfuko wa uzazi kujirudisha kistaarabu baada ya kujifungua na kusababisha kuvuja kwa damu nyingi.

 

5. Pia sababu nyingine ni kwa akina Mama wenye tatizo na kutokwa na damu uweza kujirudia rudia kila wakati wa kujifungua kwa hiyo Mama akipata mara ya kwanza , ya pili na pengine kwa mimba zake zote.

 

6. Pia Akina Mama wenye shinikizo la damu na protein kwenye mkojo ambapo kwa kitaalamu huitwa pe eclampsia na pia wanawake wenye kifafa nao wako kwenye hatari.

 

7. Kwa hiyo baada ya kujua sababu za mfuko wa kizazi kushindwa kusinyaa ni vizuri kabisa kwa wahudumu wa afya kuweza kusaidia Ili akina Mama waweze kujifungua salama na kuepukana na vifo vya akina Mama wakati wa kujifungua.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 3131

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Dalili za kasoro ya moyo ya kuzaliwa kwa watu wazima

Ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao (kasoro ya moyo ya kuzaliwa) ni hali isiyo ya kawaida katika muundo wa moyo wako unaozaliwa nao. utu uzima. Ingawa maendeleo ya kimatibabu yameboreshwa, watu wazima wengi walio na ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa wanaweza wasip

Soma Zaidi...
Hiv n kweli majivu hutoa mimb ya siku moja hadi wiki moja

Inashangaza sana, wakati wengine wanahangaika kutafutavijauzito kwa gharama yoyote ile, kuna wengine wanataka kutoa ujauzito kwa gharama yeyote ile. Unadhani njia za kienyeji sa kutoa mimba ni salama?

Soma Zaidi...
Madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji

Post hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji, ni madhara madogo madogo ambayo utokea kwa watumiaji wa matatizo ya kupumua.

Soma Zaidi...
Habari Mimi ni mjamzito was miezi Tisa sasa nimeanza kutokwa na maji kidogo kidogo ukeni bila uchungu na no mimba yangu ya kwanza he Kuna shida?

Ujauzito husababisha mabadiliko mengi mwilini, ikiwepo ongezeko la Majimaji ukeni ifikapo tarehe za kukaribia kujifunguwa. Majimaji haya ni muhimu kwa afya ya mtoto aliye tumboni.

Soma Zaidi...
MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Maumivu wakati wa tendo la ndoa kitaalamu huitwa dyspareunia.

Soma Zaidi...
Tofauti za ute kwa mwanamke

Posti hii inahusu zaidi tofauti mbalimbali za uke, kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo mbalimbali kwenye mwili wa binadamu kuna tofauti mbalimbali za ute kutegemea na hali iliyopo.

Soma Zaidi...