Zijue sababu za kutobeba mimba

Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinamfanya mama au dada kutobeba mimba. Kwa hiyo tutaziona hapo chini kama ifuatavyo.

Zijue sababu za kutobeba mimba kwa akina Mama au dada.

1. Kwanza kabisa kwa wakati huu Kuna changamoto kubwa ya akina dada au mama kushindwa kubeba mimba hii ni kwa sababu mbalimbali ambazo tutaweza kuziona hapo mbeleni sababu nyingine ni nje ya uwezo wa akina dada na sababu nyingine ni wenyewe wanaosababisha kwa kushindwa kutibu magonjwa mbalimbali, kutoa mimba mara Kwa mara na matumizi ya mda mrefu ya vidonge na sindano za kuzuia kubeba mimba.

 

2. Kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na uvimbe kwenye kizazi ambao usababishwa na vitu mbalimbali kwa hiyo hata kama mimba ikitungwa haitaweza kukua kwa sababu ya kuwepo kwa uvimbe mpaka uvimbe utolewe ndipo mama anaweza kubeba mimba.

 

3. Kuwepo kwa hormones imbalance.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na kiwango kidogo cha aina Moja ya homoni na homoni nyingine inakuwa kubwa hali ambayo usababisha mimba kushindwa kushika kwa Sababu Ili mimba itingwe kiwango chote cha homoni kinapaswa kuwa sawa.

 

4. Kuwepo kwa uvimbe kwenye mayai.

Kuna wakati mwingine uvimbe kwenye mayai usababisha mayai kushindwa kukua na kuweza kupevuka au pengine mayai yanakosa njia ya kupanda mpaka kwenye follapian tube kwa ajili ya kuchevushwa kwa hiyo ni vigumu sana kubeba mimba.

 

5. Kukosa Ute wa uzazi.

Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa Ute wa uzazi usababisha mayai kusafiri kutoka kwenye ovaries mpaka kwenye follapian tube, kama hakuna ute wa uzazi ni vigumu sana kubeba mimba.

 

6. Kizazi kushuka.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo tatizo la kizazi kushuka au kizazi kutokuwa kwenye hali yake hali ambayo usababisha kutokushika kwa mimba.

 

7. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kupata ushauri wa daktari kama Kuna tatizo lolote lile likijitokeza Ili kuweza kuhakikisha kila mama mwenye hamu ya kupata mtoto anampata.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/07/Thursday - 05:39:19 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1277


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-