Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa Ugonjwa wa fangasi,ni sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha fangasi.
1. Mabadiliko ya homoni yaani vichocheo.
Kuna wakati mwingine vichocheo vya mwili usababisha kuwepo kwa fangasi ukeni hasa wakati wa uchevushaji wa mayai,uja uzito, uzazi wa mpango na kukoma kwa hedhi, kutokana na hali hizo usababisha kuwepo kwa fangasi.
2. Kuwepo kwa upungufu wa kinga mwilini.
Kwa kawaida kinga ya mwili ikipungua kila ugonjwa unakuwepo kwa hiyo watu wale wenye magonjwa ya kupunguza kinga ya mwili wako kwenye hatari Kupata fangasi za ukeni ,kama vile wenye kansa, Ukimwi na magonjwa makubwa makubwa wako kwenye hatari ya kupata tatizo la fangasi ukeni.
3. Wenye ugonjwa wa kisukari.
Kwa kawaida walio na Ugonjwa wa kisukari wana sukari nyingi mwilini kwa hiyo na fangasi wanapenda sana sukari na pia wenye kisukari hasa cha mda mrefu wanakuwa katika hatari ya kupungua kwa kinga ya mwili.
4. Kuwepo kwenye mazingira ya joto.
Kwa kawaida watu wanaopenda kuvaa nguo zinazoingiza joto hasa za siri wako kwenye hatari ya kupata tatizo la fangasi ukeni, kwa hiyo ni vizuri kuvaa nguo ambazo haziruhusu joto kuingia kwenye shehemu za siri.
5. Matumizi ya kondomu na mbegu za kiume.
Kwa wale wote wanaotumia sana kondomu wakati wa kujamiiana wako katika hatari ya kupata fangasi ukeni.
6. Walio na vidonda kwenye sehemu za siri.
Kwa sababu ya kuwepo kwa wa aina ya uwazi kwenye sehemu za siri kama vile vidonda ni rahisi sana kuingiwa na fangasi kwenye sehemu za siri.
7. Kutumia sabuni wakati wa kujitawadha
Kwa kawaida kama mtu anajitawadha na sababu anaua bakteria wazuri na kusababisha kuwepo kwa fangasi ukeni
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
KubaleheΓΒ ni wakati mwili wa mtoto unapoanza kubadilika na kuwa wa mtu mzima (balehe) hivi karibuni. Kubalehe ambao huanza kabla ya umri wa miaka 8 kwa wasichana na kabla ya umri wa miaka 9 kwa wavulana.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi chanzo cha mvurugiko wa hedhi, Kuna kipindi hedhi uvurugika kabisa, pengine unaweza kupata hedhi mara mbili kwa mwezi au kukosa au pengine siku kuwa zaidi ya tano mpaka Saba au kuwa chache, hali hii utokea kwa sababu mbalimbali tut
Soma Zaidi...Majimaji yanayitoka kwenye uke yanafungamana na taarifa nyingi kuhusu afya vya mwanamke. Ujauzito, maradhi, mabadiliko ya homoni na zaidi.
Soma Zaidi...Je wewe ni mwanmake unayepata shida kufika kileleni? (Kukojoa wakati wa tendo lwa ndoa). Post hii itakujibu baadhi ya maswali yako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi saratani zinazowashambulia watoto. Hizi ni aina mbalimbali za saratani ambazo upenda kuwasumbua watoto ambao ni chini ya umri wa miaka mitano na uleta madhara katika kipindi cha makuzi yao.
Soma Zaidi...