Namna ya kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni mwa Mama
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni mwa mama, zoezi hili ufanyika kila mwezi pale mama anapokuja kwenye mahudhurio kwa kufanya hivyo tunaweza kuja maendeleo ya mtoto kwa kila mwezi.
Namna ya kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni mwa mama.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kupima mapigo ya moyo ya mama, kupima urefu wa Mama, kupima joto la mwili Mama, msukumo wa damu wa Mama na upumuaji wa Mama kwa kufanya hivyo tunaweza kujua kabisa maendeleo ya mtoto kama vipimo vyote viko sawa kwa Mama na kwa mtoto patakuwa hakuna shida ila kama vipimo vya mama haviko sawa na kwa mtoto huenda pakawepo na shida kwa hiyo hatua za kutibu ufuata au Mama uenda kwa daktari kwa uchunguzi zaidi.
2. Pamoja na hayo Mama anapaswa kuangaliwa kama ana damu ya kutosha kwa kuangalia macho, viganja na kama kuna dalili yoyote ya kutokuwepo kwa damu Mama anapaswa kwenda kupima kiwango cha damu na kama ni kidogo ataweza kupewa dawa na kama ni chini ya tano atapaswa kuongezewa damu.
3. Kuangalia matiti ya Mama kama kuna aina yoyote ya uvimbe na kuangalia kama matiti yana Dalili za kuwepo kwa maji maji ambayo ni ishara ya kuwepo kwa maziwa baada ya kujifungua, kama kuna dalili za uvimbe Mama anapaswa kuangaliwa kw karibu zaidi.
4.Na pia tunapaswa kuangalia kama Upumuaji wa kwenye tumbo kama ni sawa na kwenye kifua kama ni sawa hiyo ni Dalili nzuri, na pia kuangalia kama tumbo lina makovu au kama Mama amewahi kufanyiwa upasuaji au kama kuna mstari kutoka kwenye kitovu kwenda chini ambayo ni Dalili nzuri za kuwepo kwa mimba.
5.Baada ya kuangalia hayo tunapaswa kushika shika tumbo na kuangalia jinsi mtoto alivyolala kama ametanguliza kichwa au matako, kama amelala ki upande au kama kuna mapacha , Mama anapaswa kuambiwa ulalo wa mtoto ili aweze kujiandaa vizuri wakati wa kujifungua.na kama mtoto amelala vibaya Mama anasisitizwa kuzalia hospitalini ili kuepuka madhara mengine.
6.Na pia tunapaswa kujua kama mtoto anapumua kwa kusikiliza mapigo ya mtoto kwa dakika moja na kumuuliza Mama kama mtoto anacheza kama hachezi mama anapaswa kwenda kumwona daktari mara moja ili kuangalia tatizo ni nini
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi.
Posti hii inahusu zaidi dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama ambaye anakuwa amepasuka mfuko wa kizazi.
Soma Zaidi...Sababu za ugumba kwa wanawake
Post hii inahusu zaidi sababu za ugumba kwa wanawake, ni sababu ambazo upelekea wanawake wengi kuwa wagumba ukizingatia kuwa wanazaliwa wakiwa na uwezo kabisa wa kupata watoto lakini kwa sababu mbalimbali za kimazingira wanakoswa watoto, zifuatazo ni saba
Soma Zaidi...Fahamu kuhusu mapacha wanaofanana
Post hii inahusu zaidi watoto mapacha wanaofanana,ni watoto wanaozaliwa wakiwa wanaofanana kwa sura na hata group la damu huwa ni Moja.
Soma Zaidi...tuseme nilifanya ngono jana na leo nipata period,je kuna uwezekano wa kupata mimba
Mimba inatungwa katika siku maalumu na hazizidi 10. Sio kila ukishiriki tendo unaweza pata mimba. Je unaweza kupata mimba baada ya kushiriki tendo wiki moja kabla ya kuingia hedhi?
Soma Zaidi...Je ukitokea mchubuko wakati wa ngono unaweza pata ukimwi?
Kupata Ukimwi ama HIV hufungamana na mambo mengi. Si kila anayefanya ngono zembe nabmuathiria naye lazima aathirike. Hiivsibkweli, ila tangu kuwa hali hii ni hatari kwani kupata maambukizi ni rahisi sana.
Soma Zaidi...Tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID
Posti hii inahusu zaidi tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID, tunaita tiba ya awali kwa sababu baada ya kupima na kugunduliwa kwamba una tatizo au changamoto ya PID ni vizuri kutumia tiba hiii baadae ndipo utumie dawa.
Soma Zaidi...