picha

Nguzo za uislamu

Katika kipengele hiki tutajifunza nguzo za uislamu.aina tano za nguzo za uislamu,dhana ya nguzo za uislamu,lengo na umuhimu wa nguzo za uislamu

6.NGUZO ZA UISLAMU.

6.1.Dhana ya Nguzo za Uislamu.

Rejea Hadith ifuatayo:

Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:

“Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano; Kushuhudia kuwa hapana Mola ila Allah na kushuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah, Kusimamisha Swala, Kutoa Zaka, Kufunga Ramadhani na Kuhiji Makkah kwa mwenye uwezo.” (Bukhari na Muslim).

 

Kutokana na Hadith hii, nguzo za Uislamu ni:

  1. Kutoa Shahada mbili, kwa kushuhudia kuwa hapana Mola ila Allah na kushuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah.
  2. Kusimamisha Swala.
  3. Kutoa Zakat.
  4. Kufunga mwezi wa Ramadhani.
  5. Kuhiji Makkah kwa mwenye uwezo.

 

Hadith hii inatufahamisha kuwa “Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano” na sio “Uislamu ni nguzo tano”.

 

Hii ina maana kuwa misingi ya kusimama Uislamu ni nguzo tano lakini Uislamu hauwezi kukamilika (kusimama) kwa kusimamisha nguzo tano tu.

 

-     Nguzo tano ni nyenzo za kumuandaa muislamu kuweza kumuabudu Mola wake katika kila kipengele cha maisha yake ya kila siku.

 

-     Nguzo za Uislamu ni sehemu ndogo sana katika ibada ya muislamu ya maisha yake ya kila siku, mfano; shahada ni wastani wa 0% ya umri, swala ni 7% ya muda wa siku, zaka ni 2½ % ya mali yote ya tajiri, funga ni 5% ya saa za funga kwa mwaka na hija ni 0% ya umri wa mtu.

 

-     Jumla ya ibada ya nguzo 5 za Uislamu katika maisha ya muislamu ni wastani wa 3% tu na 97% ni nje ya ibada. 

 

-     Hivyo kutekeleza nguzo tano tu ni sawa na kufanya ibada 3% ya maisha na 97% ni nje ya ibada ambalo ndio lengo la kuumbwa mwanaadamu.

 

-     Kila nguzo ya Uislamu ina lengo maalumu na umuhimu wake katika kumuandaa mja kuweza kumuabudu na kumtumikia Mola wake ipasavyo.

 

 

 

Nguzo za Uislamu zina umuhimu na malengo maalumu kama ifuatavyo:

  1. Shahada mbili.

-     Ni kiingilio (kitambulisho) cha muislamu kwa ummah wa Kiislamu anayoitoa muislamu mbele ya ummah.

 

-     Ni kutoa ahadi ya kumtii Allah (s.w) ipasavyo katika kukiendea kipengele cha maisha ya kila siku saa 24.

 

2.Kusimamisha Swala.

-     Ni nguzo ya pili na ni nguzo kuu ya Uislamu na ni amri ya Allah (s.w) kwa waislamu wote katika kuitekeleza.

 

-     Lengo kuu la kusimamisha swala ni kumtakasa mja kutokana na mambo maovu na machafu.

      Rejea Qur’an (29:45).

 

3.Zakat.

-     Ni nguzo ya tatu ya Uislamu na ni amri ya Allah (s.w) kwa waislamu matajiri kuitekeleza.

 

-     Zaka ina lengo la utakaso (kuitakasa):

         Rejea Qur’an (9:103).

 

4.Swaumu.

-     Ni nguzo ya nne ya Uislamu na ni amri ya Allah (s.w) kwa waislamu kufunga mwezi wa Ramadhani.

 

-     Swaumu ina lengo la kumuandaa mja kuwa Mcha-Mungu atakaye mtii Allah (s.w) ipasavyo katika maamrisho na makatazo yake.

Rejea Qur’an (2:183).

 

5.Hija.

-     Ni nguzo ya tano ya Uislamu na ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa waislamu wenye uwezo wa mali na afya.

 

-     Hija ina lengo la kumtayarisha mja kumpenda Allah (s.w) kuliko kitu chochote hata nafsi yake.

 

-     Inamuandaa mja kuwa askari aliyetayari kutumia mali na nafsi yake katika kupigania dini yake.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2021/12/30/Thursday - 08:50:04 am Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 6159

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 ai web app    👉4 web hosting    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa

Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii.

Soma Zaidi...
Sifa za imamu wa swala ya jamaa

Post hii inakwenda kukupa sifa za imamu wa msikitini anayepasa kuswalisha swala ya jamii.

Soma Zaidi...
Maana ya Mirathi na kurithi katika uislamu

Maana ya MirathiMirathi katika Uislamu ni kanuni na taratibu alizoziweka Allah (Sw) katika kuwagawawia na kuwarithisha familia na jamaa, mali aliyoiacha marehemu.

Soma Zaidi...
Wanaowajibika kuhijji

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kugungisha ndoa ya kiislamu hatuwa kwa hatuwa

Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa.

Soma Zaidi...