Kutoa zakat
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
4.3. Kutoa Zakat.
Umuhimu wa Zakat na Sadakat katika Uislamu.
Zakat ni nguzo ya tatu ya Uislamu.
Baada ya shahada mbili na kusimamisha swala nguzo muhimu sana katika uislamu ni kutoa zakat kama ilivyoainishwa katika hadithi.
Kutoa zakat na Sadaka ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Kutoa zaka na vile tulivyoruzukiwa katika mali na huduma au misaada mbali mbali ni wajibu kwa waislamu wanaovimudu.
Rejea Quran (14:31) na (2:254).
Kutoa Zakat ndio kitambulisho cha Uislamu na Ucha-Mungu wa mtu.
Muislamu akiacha au kukataa kutoa zakat kwa makusudi ni ishara ya kuritadi na kutoka katika Uislamu.
Rejea Quran (9:11) na (2:2-3).
Kutoa Zakat na sadaka ni sababu ya mtu kufaulu Duniani na Akhera.
Miongoni mwa sifa za waumini na wacha-Mungu ni kutoa katika vile walivyoruzukiwa na muumba wao.
Rejea Quran (2:2-3), (23:1-4), (22:34-45) na (2:262,274).
Kutotoa Zakat na Sadaka ni sababu ya kuangamia mtu Duniani na Akhera.
Kutotoa katika vile tulivyoruzukiwa hupelekea mtu kustahiki adhabu hapa Duniani na Akhera pia.
Rejea Quran (9:34-35), (92:8-10) na (3:180).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 ai web app 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Mafungu ya urithi katika uislamu
Hspa utajifunza viwango maalumu vya kutithi mirathi ys kiislamu.
Soma Zaidi...Taasisi za Kifedha Katika Mfumo wa Uchumi wa Kiislamu
- Ni taasisi za kifedha zinazohusika na kuhifadhi akiba na mali za watu zenye thamani kubwa kama dhahabu, n.
Soma Zaidi...