Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Haki za Nafsi.
Haki za nafsi imekokotezwa kuanzia binafsi, familia, wazazi, n.k kama ifuatavyo;
Mtu Binafsi.
Haki za msingi ni chakula, makazi, malezi, elimu, mavazi, matibabu na kufanyia kazi vipaji na neema alizonazo inavyostahiki ikiwemo;
Haki ya Macho.
Ni kutazama yaliyoamrishwa na kuyaepusha na yaliyoharamishwa.
Rejea Quran (17:36), (41:20), (24:30-31) na (20:131).
Haki ya Masikio.
Ni kusikiliza yaliyoamrishwa na kutosikiliza yaliyoharamishwa pia.
Rejea Quran (8:22) na (6:25).
Haki ya Midomo na Ulimi.
Ni kula, kunywa na kuzungumza yaliyohalalishwa na sio yaliyoharamu.
Rejea Quran (16:114), (17:26-29), (17:53), (41:33) na (31:6).
Haki ya Mikono na Miguu.
Ni kushika na kuendea vyote vilivyoamrishwa na kuacha vilivyokatazwa.
Rejea Quran (25:72) na (31:18).
(b) Haki za Familia.
Ni kusimamia malezi, elimu, uadilifu na wajibu wa kila mmoja katika familia kwa muongozo wa Quran na Sunnah ili kuleta kufikia lengo la kuumbwa.
Rejea Quran (52:21).
(c) Haki za Watoto.
Watoto wana haki ya kupata malezi na makuzi bora kulingana na mahitaji yao kwa mujibu wa mafundisho ya Quran na Sunnah katika sehemu zifuatazo;
Haki ya Uhai.
Uhai wa mtoto ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kupitia malezi na makuzi ya wazazi.
Haki ya Nasaba.
Mtoto kupata nasaba ni haki kisheria ili kuwa mwanafamilia halali.
Rejea Quran (33:4).
Haki ya Makuzi na Malezi bora.
Makuzi na malezi bora ya mtoto ni kupata haki zake za msingi na elimu inayomuwezesha kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo.
Rejea Quran (66:6).
(d) Haki za Wazazi.
Ni kuwahurumia, kuwaheshimu, kuwafanyia wema, kuwahudumia na kuwalea ipasavyo.
Rejea Quran (31:14), (17:23-24), (4:36), (6:151), (19:14) na (19:32).
(e) Haki za Jamaa na Majirani.
Ni kutunza uhusiano na kusaidiana pale inapohitajika kwa kuzingatia mipaka.
Rejea Quran (2:215).
(f) Haki za Mayatima, Wajane na Masikini.
Ni kuwahifadhi na kuwasaidia wanapokuwa na shida na mahitaji ya kimaisha.
Rejea Quran (2:220), (4:2), (4:10), (2:262) na (2:267).
(g) Haki za Udugu wa Kiimani na za Watu wengine.
Udugu wa kiimani ni haki na bora zaidi kuliko udugu wa damu au nasaba.
Rejea Quran (49:10), (49:13), (7:172-173), (4:7) na (5:8).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Katika uislamu imekatazwa kutamani kufa hata kama utakuwa ni mtu muovu sana ama mchamungu sana.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.
Soma Zaidi...Ugawaji wa mirathi-Mume ana nusu (1/2) = 1/2 -Mama ana sudusi.
Soma Zaidi...Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine.
Soma Zaidi...Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Soma Zaidi...