Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Lengo la Kusimamisha Swala.
Lengo kuu la kusimamisha swala ni kumkinga mja na mambo machafu na maovu kwa kutekeleza kikamilifu sharti, nguzo na sunnah za swala pamoja na kuwa na khushui ndani ya swala kama ifuatavyo;
Swala inamtakasa mja kwa kuzingatia na kutekeleza sharti zake zote kikamilifu ambazo ni kuwa twahara, sitara (kujisitiri), kuchunga wakati wa swala na kuelekea Qibla.
Swala inamtakasa mja kwa kutekeleza kikamilifu nguzo na sunnah za swala kama kumsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w), kusoma Quran, kutoa ahadi ya kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w), kuomba dua na kutekeleza vitendo vyote vya swala.
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za uislamu,kutoa zakat na sadaqat (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...