Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini

Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)

-    Sanda ya mwanamke ina vipande vitano; 

 

    -    Taratibu za kutayarisha sanda na kukafini:

  1. Majamvi mawili yatatandikwa moja baada ya nyingine.
  2. Kikatwe kitambaa cha ukubwa wa shuka ya kujifunga kiunoni (shuka/gagulo) na iwekwe juu ya majamvi mawili ili ije kutumika kumfungia kiunoni.

 

  1. Kisha ikatwe kanzu (blause) isiyoshonwa vizuri kwa kukunja kitambaa na kukitoboa katikati kwa ajili ya kuingizia kichwa cha maiti (kumvalisha) na kisha kushikiza pembeni kwa uzi mfano wa kanzu kata mikono na kuwekwa juu ya gagulo sehemu ya chini (kiunoni) na itakuwa juu ya majamvi 2 sehemu ya juu (kifuani).

 

  1.  Kitambaa (ukaya/shungi) ya kutosha kuweza kufunika kichwa na uso kitaingizwa ndani ya shingo ya kanzu na kunyooshwa kwa juu.

 

  1. Maiti itaanza kuvalishwa kanzu, kisha kufungwa shuka (gagulo) juu yake. Kisha maiti itawekewa pamba viungo vyote vya sijda na kuziba sehemu za matundu kama ilivyokuwa kuwa kwa maiti mwanamume. Kisha maiti itatizwa (itafungwa) na majamvi mawili, moja baada ya jingine kwa kuanza kunjo la kushoto na kumalizia la kulia juu yake, na kisha kufungwa na kamba tatu juu yake- kichwani, tumboni na miguuni na kuwa tayari kuingizwa kwenye jeneza na kuswaliwa.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 11141

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu

Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume.

Soma Zaidi...
Nguzo za kufunga ramadhani

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Nguzo za swala.

Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali.

Soma Zaidi...