Kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao
KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Akaunti kuhakiwa inamaana kuna mtu amelogin kwenye akaunti yako bila ya ruhusa yako ama bila ya kumpatia neno la siri. Facebook imeweka njia kadhaa kuhakikisha kuwa akaunti za watu zipo salama muda wowote.
Two-factor authentication ni katika njia mujarabu ambazo facebook wameweka ili kulinda akaunti za watumiaji wake. Kwa kutumia njia hii hata kama mtu anaijuwa password yako (neno la siri) hataweza kuingia kwenye akaunti yako ya facebook mpaka awe na laini yako ambayo namba yeke umeisajili facebook.
Njia hii inaongeza tabaka lingine la usalama wa akaunti yako ya facebook. Baada ya kuingiza neno la siri kwenye akaunti yako ya facebook, facebook watakutumia code (namba sita) kwenye laini yako ulioisajili facebook. Namba hizo utaziingiza kwenye kibox na ndipo utaruhusiwa kuingia kwenye akaunti.
Kuanza kutumia njia hii ingia kwenye setting, kisha security and login kisha Two-Factor Authentication. Utatakiwa kuingiza namba ya simu na maelekezo machache yatafuata. Utalogout kisha utalogin tena ili kuthibitisha huduma kama ipo tayari.
Njia hii itasaidia sana kwa wale ambao tayari password zao kuna watu wanazifahamu. Hata kama mtu anaijua password TROJAN) yako katu hataweza kuingia kwenye akaunti yako mpaka awe na laini yako. Karibia mitandao mingi inatumia njia hii ikiwemo google, linkedin, github na mingine mingi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 web hosting 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Utunzaji wa betri la kifaa chako
Posti hii inakwenda kukupa elimu kuhusu utunzaji wa betri la kifaa chako
Soma Zaidi...UTUNZAJI WA BETRY YA KIFAA CHAKO
Namna ya kutunza betri yako iweze kudumu kwa muda mrefu
Soma Zaidi...Njia za kujilinda na malware
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujilinda na malware
Soma Zaidi...Kipi kingine utafanya ukiwa Facebook
Somo hili linakwenda kukueleza Mambo mengne unayoweza kuyafanya ukiwa Facebook
Soma Zaidi...KIPI KINGINE UTAFANYA UKIWA FACEBOOK: matumizi mengine ya facebook
Facebook ni mtandao wa kwanza wa kijamii (social media) unaotembelewa na watu wengi.
Soma Zaidi...