Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini.
MTAZAMO WA KIKAFIRI JUU YA DINI
Maana ya Dini kwa Mtazamo wa Makafiri
Makafiri wanatafsiri dini kuwa ni:
(i)“Imani inayohusiana na mambo ya kiroho baina ya binaadamu na Mwenyezi Mungu au njia ya kuhusiana na Mwenyezi Mungu” (Kamusi ya Kiswahili sanifu)
(ii)“Imani juu ya kuwepo Mungu Muumba aliye muweza na mwenye nguvu juu ya kila kitu, Mmiliki wa ulimwengu, ambaye amempa binaadamu roho ambayo huendelea kuishi baada ya kifo cha mwili” (Oxford Advanced Learner’s Dictionary of Current English).
Kutokana na tafsiri hii ya dini iliyonukuliwa kutoka kwenye kamusi ya Kiswahili na ya Kiingereza, tunajifunza mambo makubwa mawili:
Kwanza, kwa mtazamo wa makafiri dini inahusiana na imani ya kuwepo Allah (s.w).
Hivyo wenye dini ni wale tu wanaoamini kuwepo kwa Allah (s.w), na wale was ioamini kuwepo kwake hawana dini. Ni katika mtazamo huu V. I. Lenin katika kitabu chake “Socialism and Religion (Ujamaa na Dini) amedai:
“Everybody must be absolutely free to profess any religion he pleases or no religion whatever; i.e. to be an atheist which every socialist is as a rule...”
Tafsiri:
“Kila mtu hanabudi kuwa huru kabisa kufuata dini yoyote anayotaka au asiwe na dini kabisa, yaani awe kafiri, jambo ambalo inambidi kila mjamaa awe kama sheria...”
Pili, kwa mtazamo wa makafiri, dini inahusiana na mambo ya kiroho au ulimwengu wa kiroho tu, na haihusiani kabisa na
ulimwengu wa kimaada (wa vitu). Ni kwa mtazamo huu kwa makafiri, matendo ya wafuasi wa dini yamegawanywa katika sehemu mbili, matendo ya dini na matendo ya dunia. Katika mtazamo huu pia Waislamu hulaumiwa na makafiri kuwa wanachanganya dini na siasa, dini na uchumi; dini na utamaduni, na kadhalika.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kwenye mada hii tutajifunza shahada mbili,tafsiri ya shahada kstika maisha ya kila siku.
Soma Zaidi...Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine.
Soma Zaidi...“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele).
Soma Zaidi...Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi.
Soma Zaidi...