Maadili na malezi ya jamii
3. Maadili na malezi ya jamii
Qur-an, vile vile inatufunza mahusiano tunayotakiwa tuwe nayo ili kuondoa chuki na uadui na kupandikiza mapenzi miongoni mwa wanajamii kama tunavyojifunza katika sura zifuatazo:
Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu. Na (ameagiza) kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee, (naye yuko) pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa hishima (kabisa). Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa (njia ya kuwaonea) huruma na useme: "Mola wangu! Warehemu (wazee wangu) kama walivyonilea katika utoto." Mola wenu anajua sana yaliyo nyoyoni mwenu. Kama mkiwa wema (kwa wazee wenu daima; lakini mara moja mbili hivi mkapotea, basi atakusameheni) kwani Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wenye kurejea (kwake). (17:23-25)
Na umpe jamaa (yako) haki yake, na maskini na msafiri aliyeharibikiwa, wala usitawanye (mali yako) kwa ubadhirifu. Hakika watumiao kwa ubadhirifu ni ndugu wa mashetani (wanamfuata Shetani). Na Shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake. (1 7:26-2 7)
Na kama unajipurukusha nao (sasa hivi kwa kuwa huna kitu) lakini unatafuta rehema ya Mola wako (riziki) unayoitumai, basi sema nao maneno laini (ya kuwapa waadi ya kuwa ukipata utawapa). Wala usifanye mkono wako (kama) uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa (ukifanya hivyo) na kufilisika (ukiukunjua ovyo ovyo). (17:28-29)
Hakika Mola wako humkunjulia rikizi amtakaye na humdhikishia (amtakaye). Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona; (anajua yupi anayestahiki utajiri na yupi anayestahiki ufakiri). (17:30)
"Wala msiwaue watoto wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi ndio tunaowaruzuku wao na nyinyi (pia). Kwa yakini kuwauwa ni khatia kubwa. Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo (zinaa) ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa). (17:31-32)
Wala msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha (kuuliwa) isipokuwa kwa haki. Na mwenye kuuawa kwa kudhulumiwa, basi tumempa nguvu mrithi wake. Basi (mrithi ) asifanye fujo katika kuua (kwa ajili ya huyo mtu wake aliyeuliwa). Hakika yeye atasaidiwa (na sharia maadam anayo haki). (17:33)
Wala msiyakaribie (msiyaguse) mali ya yatima, isipokuwa kwa njia iliyo bora mpaka afike baleghe yake (huyo yatima akabidhiwe mwenyewe). Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa (Siku ya Kiama). Na timizeni kipimo mpimapo; na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na bora mwishoni (kwake). (17:34-35)
Wala usifuate usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo; hivyo vyote vitaulizwa. Wala usitembee (usende) katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala huwezi kufikia urefu wa milima. (Basi unajivuna nini). (1 7:36-3 7)
Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza mbele ya Mola wako.(1 7:38)
Haya ni katika yale aliyokufunulia Mola wako katika hikima (zake). Wala usimueke pamoja na Mwenyezi Mungu, Mungu mwengine, usije kutupwa katika Jahanamu hali ya kuwa mwenye kulaumiwa (na) mwenye kufukuzwa (huku na huku). (1 7:39)
Aya hizi zinatufundisha kuwa ili tuweze kuishi vizuri katika jamii hatuna budi kushikamana na maamrisho kadhaa yaliyoainishwa na kujiepusha na makatazo kadhaa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)
Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu
Faradhi kwa maiti ya muislamu (edk form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kujiepusha na kukaribia zinaa
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...KAZI ZA MALAIKA
Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi.
Soma Zaidi...Mambo muhimu anayofanyiwa muislamu kabla ya kufa
Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s.
Soma Zaidi...