Katika somo hili utajifunza kuhusu Kotlin library. Pia tutakwenda kutengeneza library yetu wenyewe kwa ajili ya kufanya mazoezi zaidi.
Library ni nini?
Library ni mkusanyiko wa maelekezo ya programu, yaani ni yale maelekezo ambayo huamuru kompyuta kuyafuata. Kotlin yenyewe ina library zake. Kwa mfano, wakati tunajifunza kuhusu mahesabu, tulitumia library ya math ambapo tuli import kwa kutumia `import kotlin.math`.
Hizi library zipo nyingi na kila moja ina matumizi yake mengi tu. Kwa muda wako, unaweza kuzifuatilia Kotlin library kwenye tovuti yao ya jetbrain, link nimeitoa kwenye somo la kwanza.
Jinsi ya kutengeneza library yako mwenyewe.
Ili uweze kutengeneza library, kwanza utatengeneza faili nyingine kisha utalipa jina unalolotaka. Kwa mfano, tutatengeneza faili tutaiita `hesabu.kt`.
Ndani ya hilo file mstari wa kwanz akabisa tutatengeneza package name. Kwa mfano library yetu itakuwa kwenye package ya mylib. Hivyo tutaandika hivi package com.mylib.hesabu
Utaona hapo nmeanza keyword package ikafuatiwa na jina la hiyopackage ambalo ni com.mylib.hesabu baada ya hapo utaanza kuandika code zako library.
Sasa, chukulia tunataka library yetu ya hesabu iweze kufanya mambo kama kutafuta eneo la pembe tatu, eneo la mraba, na eneo la trapeza. Tutatumia kanuni za darasa la 5 shule ya msingi. Eneo la pembetatu ni (kimo * kitako) / 2, eneo la mtatili ni (urefu * upana), na eneo la trapeza ni ((a + b) * h / 2).
Sasa, kanuni hizi kila moja wapo hapo, tutazitengenezea function yake ili kuweza kufanya kazi husika. Kisha weka code kwenye faili letu tuloliita hesabu.kt .
package com.mylib.hesabu
fun pembeTatu(kimo: Int, kitako: Int): Double {
return (kimo * kitako) / 2.0
}
fun eneoMraba(urefu: Int, upana: Int): Int {
return urefu * upana
}
fun eneoTrapeza(a: Int, b: Int, h: Int): Double {
...Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ambavyo class moja inaweza kuriti method na properties kutoka kwenye class nyingine.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza tofauti wa library na package
Soma Zaidi...Katika soomo hili utakwenda kujifunza kuhusu class, maana yake, na jinsi ya kuitengeneza
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu while loop na do while loop zinavyofanya kazi katika Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu when case na jinsi inavyofanya kazi kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu nadharia ya package, kazi zake, aina zake na jinsi zinavyotumika
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza maana na features za object oriented Programming
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu set data type pamoja na method ambazo hufanya kazi kwenye set.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kuingia ndani zaidi kwenye somo la function. Hapa tutakwenda kuona aina za function.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza method zinazofanya kazi kwenye list data type kwenye Kotlin.
Soma Zaidi...