Katika somo hili tutakwenda kujifunza jinsi ya kushughulika na string kwenye Kotlin.
Tulisha jifunza kuhusu string katika somo la aina za data. Pia tulijifunza mambo kadhaa khusu string kama interpolation na concatnate. Katika somo hili tutaingia ndani zaidi.
String indexing
Katika programming unaweza kuitumia character yeyote kwenye string husika. Kwa mfano katika string bongoclass hapo naweza kusoma herufi moja moja. Tunapohesabu index ya string tunaanza na 0. Hivyo katika string Bongoclass kama tunataka kusoma herufi ya mwanzo tu hapo tutatumia index ya 0
Mfano:
fun main() {
val text = "Bongoclass"
print(text[0])
}
Hapo utaona imeleta B
fun main() {
val text = "Bongoclass"
print(text[6])
}
Hapa itakuletea l
Sas kwa mfano unataka kujuwa kwenye string yetu ya bongoclass neno class linapatikana kuandia index ya ngapi. Kufanya hivi tutatumia indexOf .
fun main() {
val text = "bongoclass"
print(text.indexOf("class"))
}
Hapo itakupa jibu 5 kumaanisha kuwa neno class kwenye string ya bongoclass hupatikana kuandia index ya 5, kumbuka tunahesabu index kuanzi 0.
Kujuwa idadi y character kwenye string (string length)
Kwa mfabo tunataka kujuwa katika string bongoclass kuna character ngapi. Hapo tutatumia length property.
Mfano:
fun main() {
val text = "Bongoclass"
print(text.length)
}
Hapo itakuletea jibu 10 kumaanisha kuwa kuna character 10.
Kubadili string kuwa katika herufi kubwa na ndogo
Kama unataka kubadili string case kutoka herufi kubwa kwenye ndogo utatumia lowercase() na kama unataka kubadili kutoka ndogo kuwa kubwa utatumia uppercase()
Mfano:
fun main() {
val text = "bongoclass"
val text2 = "BONGOCLASS"
println(text.uppercase())
print(text2.lowercase())
}
Kulinganisha string mbili:
Wakati mwingine utahitaji kulinganisha string mwili. Kama zipo sawa. Kufanya hivi utatumia compareTo. Ikiwa itakupa jibu 0 ujuwe zipo sawa, na ikikupa jibu tofauti ujuwe hazipo sawa.
Mfano:
fun main() {
val text = "bongoclass"
val text2 = "bongoclass"
print(text compareTo text2)
}
Hiyo itakupa">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu namna ambavyo program inaweza kufanya maamuzi kulingana na mashart fulani.ama namna ambavyo program inaweza ku run code zaii ya mara moja kulingana na mashart. Hapa tutazingumzia flow of control statement
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza kuhusu method na properties za Kotlin zinazofanya kazi kwenye namba.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu break na continue kwenye Kotlin loop za for loop na while loop.
Soma Zaidi...Katika somo hili unakwenda kujifunza kuhusu sheria na kanuni za undishi wa code za Kotlin yaani syntax za kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu while loop na do while loop zinavyofanya kazi katika Kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kuandika variable kweye Kotlin. pia utakwenda kujifunza kuhusu concatnation na interpolation
Soma Zaidi...Katika soomo hili utakwenda kujifunza kuhusu class, maana yake, na jinsi ya kuitengeneza
Soma Zaidi...Jinsi ya kuchukuwa user input kwenye Kotlin kwa ajili ya kuongeza user interaction kwenye program.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kuingia ndani zaidi kwenye somo la function. Hapa tutakwenda kuona aina za function.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza maana na features za object oriented Programming
Soma Zaidi...