Katika somo hili tutakwenda kuzungumzia kuhusu parameter kwenye Kotlin function. Pia tutakwenda kuona mambo mengine yanayohusu function
Prameter zinatakiwa zifuate utaratibu:
Unapoweka parameter unaziweka kwenye mpangilio, hivyo hata wakati wa kuweka argument unatakiwa ufuate utaratibu huo huo. Mfano kama function ina parameter 2 ya umri na jinsia, basi wakati wa kuweka argument ifuate utaratibu ho huo. Pia unatakiwa kuzingatia na aina zake za data. Kama parameter inahitaji namba wewe unaweka string hapa utasababisha error.
fun haloo(umri: Int, jinsia: String) {
println("umri wako ni miaka $umri na jinsia yako ni $jinsia")
}
fun main() {
println("Andika umri wako: ")
val umri = readLine()!!.toInt()
println("Andika jinsia yako: ")
val jinsia = readLine()!!
haloo(umri, jinsia)
}
Sasa hapo kama utachanganya mpangilio wa aprameter aina za data utaishia kupata error
Unaweza kuwa na default parameter
Default parameter ni parameter ambayo inakuwa umeshawekwa, hivyo mtumiaji wa program hana haja ya kujaza kitu. Kwa mfano katika program yetu ya hapo juu tunakwenda kuongeza parameter nyingine ambayo itaonyesha makazi. Tutaweka Tanzania kama default parameter
Ili uweze kuandika default parameter utaiweka ndani ya mabano {} utai declare kwa alama ya ( = ). Mfano {makazi = ‘Tanzania’}
fun haloo(umri: Int, jinsia: String, makazi: String = "Tanzania") {
println("umri wako ni miaka $umri na jinsia yako ni $jinsia unaishi $makazi")
}
fun main() {
println("Andika umri wako: ")
val umri = readLine()!!.toInt()
println("Andika jinsia yako: ")
val jinsia = readLine()!!
haloo(umri, jinsia)
}
Pia unaweza kuweka parameter ambayo sio lazima ijazwe hivyo inakuwa ni optional. Parameter hii inaweza kuwa ni default parameter. Na endapo hutakuwa na default parameter yenyewe itabeba value null kumaanisha haina kitu. Kwa mfano hapo tunataka kuongeza parameter ya kuweka jina la mkoa. Hiyo ttaifanya sio lazima ijazwe yaani option.
Ili kuweka optional parameter tutaiweka jina lake kisha utaweka aina yake ya data ikifuatiwa na alama ya ? mfano [String? mkoa]
fun haloo(umri: Int, jinsia: String, mkoa: String?) {
println("umri wako ni miaka $umri na jinsia yako ni $jinsia unaishi $mkoa")
}
fun main() {
print("Andika umri wako: ")
val umri = readLine()!!.toInt()
print("Andika jinsia yako: ")
val jinsia = readLine()!!
print("Andika Mkoa unaoishi: ")
val mkoa = readLine()
haloo(umri, jinsia, mkoa)
}
Hapo kwenye parameter ya unapoishi sikujaza kitu kivyo haikileta chochote, lakini ukijaza italeta, ni kwa sababu parameter ya mkoa ni option sio lazima kujazwa.
Required parameter
Pia parameter inaweza kuwa required kuwa ni lazima kujazwa na kama haitajazwa program haiwezi kuendelea kufanya kazi. Kwenye KKotlin parameter zote ni required tofauti na lugha n">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya function, jinsi ya kuandika function na kuweka parameter kwenye function
Soma Zaidi...Somo hili linaeleza msingi wa database, kwa nini tunazitumia, aina za database, na utangulizi wa MySQL. Pia tutaona jinsi Kotlin inaweza kuunganishwa na MySQL kwa ajili ya kutekeleza CRUD operations (Create, Read, Update, Delete).
Soma Zaidi...Katika somo hili unakwenda kujifunza kuhusu sheria na kanuni za undishi wa code za Kotlin yaani syntax za kotlin.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu operator na aina zake.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu nadharia ya package, kazi zake, aina zake na jinsi zinavyotumika
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu Kotlin library. Pia tutakwenda kutengeneza library yetu wenyewe kwa ajili ya kufanya mazoezi zaidi.
Soma Zaidi...Katika soomo hili utakwenda kujifunza kuhusu class, maana yake, na jinsi ya kuitengeneza
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu dhana ya module. Hata ivyo tutakwenda kuisoma zaidi kwenye android App
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza tofauti wa library na package
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu set data type pamoja na method ambazo hufanya kazi kwenye set.
Soma Zaidi...