12.Nyanya
Tomato tumezoea huliwa katika mboga, ila pia unaweza kuila bichi ila sio jambo zuri hususan uangalizi unahitajika. Tomato zimetaja na wataalamu wa Afya kuwa na faida nyingi. Tomato huweza kupunguza hatari ya kupata saratani na pia hupunguza athari za kisukari.
Ndani ya tomato kuna aina za carotenoid kama vile: lutein na lycopene. Hizi husaidia katika kuimarisha afya ya macho. Au kupunguza athari zinazotokana na mwanga zisidhuru macho. Tomato ni katika matunda ambayo yauwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi. Pia huweza kuuwa seli za saratani.
Tomato zina vitamini C kwa wingi. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vitamini hivi vina kazi kubwa ya kulinda mwili na maradhi mbalimbali. Pia vitamini hivi vinakazi ya kuzuia utengenezwaji wa seli bila ya mpangilio yaani seli za saratani.
Tomato huweza kupunguza presha kwa wale wenye tatizo la kupanda kwa presha yaani shinikizo la damu. Wataalamu wanaeleza kuwa kutumia kudhibiti kiwango cha sodium yaani madini ya sodiam hali hii husaidia katika kurekebisha shinikizi la damu.
13.kitunguu saumu. Watu wamekuwa wakitumia kiungo hiki kwa kupikia toka enzi za mababu. Halikadhalika kiungo hiki kimekuwa kikitumika kama dawa kwa karne nyingu, maeneo mengi duniani. Utafiki unaonesha kuwa katika kitunguu saumu kuna ‘allicin’ hii husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga katika kupambana na maradhi mbalimbali. Tumia kiungo hiki kwa kupikia. Pia unaweza kutafuna punje zake. Watu wenye maradhi mablimbali wamekuwa wakitumia kiungo hiki na kuona mafanikio.
14.Pilipili kali. Watu wengi wamekuwa wakiacha kutumia pilipili etu kwa sababu ya ukali wake. Ila itambulike kuwa ijapokuwa ni kali lakini ila faida nyingi sana kwa afya ya mtu. Pilipili pia ina vitamini c ndani yake kwa kiasi. Vitamini hivi ni muhimu sana katika mfumo mzima wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na wadudu shambulizi.
15.Karoti. Watu wengi wanafahamu kuwa karoti ni mujarabu katika maatizo ya macho. Karoti huimarisha afya ya macho yako. Tafiti zinaonyesha kuwa karoti husaidia kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo. Kariti ni kiungo safi kwa mboga ni ni dawa iliyo nzuri. Unaweza kutumia karoti kwa kutafuna, kutengeneza juisi, kachumbari iliyochanganywa na kabichi n.k
16.Tangaizi. Kiungo hiki mara mara nyingi hutumika kwenye chai. Pia hutumiwa kwenye mchuzi japo sio kawaida. Tangaizi hutibu maradhi mengi lakini ni mujarabu sana kwa tatizo la nguvu za kiume. Tutaizungumza vizuri tangaizi kwenye post zetu zijazo.
Tangaizi husaidia katika kuhakikisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula unafanya kazi kwa ufanisi. Husaidia katika uzalishaji wa mate pamoja na nyongo. Huongeza metablolic ndani ya utumbo. Pia tafiti zinaashiria kuwa tangawizi huweza kusaidia kukinga mwili na saratani ya utumbo.
Tangawizi husaidia katika kupunguza stress ikitumika kama kiungo cha chai, pia husaidia katika kusukuma chakula vizuri ndani ya tumbo, hupunguza tatizo la kutokwa na damu za pua. Pia tangawizi kuondoa maumivu na husaidia katika kuimarisha afya ya moyo.
Tangawizi ina 17.86 g of carbohydrate, 3.6 g of dietary fiber, 3.57 g of protein, 14 mg of sodium, 1.15 g of iron, 7.7 mg of vitamin C, na 33 mg of potassium