Kazi ya protin na vyakula vya protini mwilini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya kazi ya protin na vyakula vya protini mwilini

KAZI ZAPROTINI NA VYAKULA VYA PROTINI MWILINI

Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini. Kazi za protini mwilini:- Kujenga mwili; Kupona kwa vidonda na majeraha Kutengeneza antibody (kinga za mwili) Kutengeneza hemoglobin (chembechembe zaseli nyekundu za damu) Kutengeneza enzymes zinatumika katika kumeng;enya chakula Kutengeneza homoni Kuthibiti kichakati na shughuli za ndani ya seli Huhusika katika kutengeneza tishu (nyama na misuli) ndani ya mwili Nywele, kope, nyusi, vinyweleo na kucha hutokana na rotini  

 

1. Kujenga mwili; protini huhusika katika kujenga mwili, na uponaji wa vidonda na majeraha. Mwili kukua vyema na kujengenka vyema protini inahitajika katika kuhakikisha hili linafanyika. Ulaji wa protini ya kutosheleza uanaweza kuufanya mwili uwe katika umbo jema na lililojengeka vyema. Endapo mwili utapata majeraha protini itahusika katika kuziba majeraha na vidonda katika eneo husika. Kama wanavyosema mwili haujengwi kwa matofali, lakini unaweza kusema kuwa protini ndio tofali la kuujenga mwili.  

 

2. Hutumika katika kutengeneza antibodies; hizi ni chembechembe za protini zinazopatikana kwenye damu. Chembechembe hini ni muhiu sana katika mfumo wa kinga. Hizi huweza kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi ya maradhi na watutu waletao maradhi. Protini inahitajika ili kutengenezwa kwa chembechembe hizi kufanyike. Hivyo unaweza kusema kuwa protini ni muhumu katika mfumo wa kinga mwilini.  

 

3.Utengenezwaji wa hemoglobin; hemoglobin ni aina za protini, na hii huhusika katika usafirishaji wa hewa ya oksijen na kabondioxide ndani ya miili yetu. Hemoglobin ni chembechembe ambazo ninakazi ya kuchukuwa hewa ya okijeni baada ya mtu kuivuta na kuipeleka kwenye moyp ambapo husambazwa, kwenda maeneo mengine. Kisha hemoglobinhukusanya hewa chafu nyenye kabondaiyokasaidi na kuipeleka kwenye mapafu. Ijapokuwa hemoglobin ni chembehembe za protini lakini pia imetokana na madini ya chuma. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuathiri mfumo wa damu.  

 

4. Utangenezwaji wa enzymes. Hizi ni chembechembe zinazotambulika kama biological catalyst, yaani ni vichochezi vya kuchochoea michakato ya kikemikali iendelee kufanyika ndani ya miili etu. Enzymes huchukuwa nafasi kubwa katika kumenge’enya chakula katika hutau zote na katika maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Enzmes zinaweza kupatikana mdomoni, tumboni na katika utumbo mdogo. Umeng’enywaji wa chakula ili tupate vurutubisho enzymes hutumika.  

 

5. Utengenezwaji wa homoni; ili mwili uweze kutengeneza homoni unahitaji protini. Homoni ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika kufanya kazi nyingi na tata mwilini. Utengenezwaji wa mayai kwa wanawake na mbegu za uzazi kwa wanaume unahitaji homon. Urekebishwaji wa sukari pia unahitaji homoni. Ilijasho liweze kutoka homoni huhusika katika kurekebisha joto mwilini. Homoni zinakazi nyingi sana mwilini. Lakini jambo la msingi kufahamu hapa ni kuwa homoni hutengenezwa kwa protini.  

 

6. Utengenezwaji wa nywele na vinyweleo na kope pia hutokana na protini. Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa protini ni matofali ya kuijenga miili yetu na hii ndio maana yake. Hata nywele zetu kama hatutapata protini ya kutosha katu huwezi kuna na nywele nzuru, na zenye afya ya kutosheleza. Nywele zinaweza kuwa katika hali isiyo ya kawiada ka hutapata protini ya kutosha. 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Huduma Main: Afya File: Download PDF Views 2647

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 web hosting    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Njia za kukabiliana na presha ya kushuka

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kushuka

Soma Zaidi...
Kwanini mtu alie ng'atwa na nyoka hairuhusiwi kumpa pombe?

Swali languKwanini mtu alie ng'atwa na nyoka hairuhusiwi kumpa pombe?

Soma Zaidi...
Huduma ya kwanza kwa aliye ungua na Moto.

Posti hii inazungumzia kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyeungua na Moto.

Soma Zaidi...
Huduma ya kanza kwa mgonjwa mwenye jeraha la kawaida kwenye ubongo

Posti hii inahusu zaidi huduma ya kwanza ya mgonjwa mwenye jeraha la kawaida kwenye ubongo, ni Tiba ambayo utolewa kulingana na dalili za jeraha la kawaida kwenye ubongo kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...
Huduma ya kwanza kwa mwenye uchafu kwenye sikio.

Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kqa mgonjwa aliyeingiliwa na kitu au uchafu kwenye sikio.

Soma Zaidi...
Ukiwa unalima sana unaweza kukonda

Unadhanivkufanya kazi kunaweza kukusababishia maradhi ama mwili kudhoofu, ama kukonda. Umeshawahivkujiuliza wanao nenepa huwa hawafanyi kazi?

Soma Zaidi...
Vyakula vya madini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya madini mwilini

Soma Zaidi...
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA

Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.

Soma Zaidi...
Viwango vitatu vya kuungua.

Posti hii inahusu zaidi viwango vitatu vya kuungua. Ili tuweze kujua mtu ameunguaje Kuna viwango vitatu vya kujua kiasi na namna mtu alivyoungua

Soma Zaidi...
Malengo ya kutibu ukoma

Posti hii inahusu zaidi malengo ya kutibu ukoma, ni malengo ambayo yamewekwa na wizara ya afya ili kuweza kutokomeza ukoma kwenye jamii

Soma Zaidi...