Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo ya DTP au DPT ambayo Inazuia magonjwa ya Donda Koo, Pepopunda na kifaduro.
Kazi ya chanjo ya DTP.
1. Aina hii ya chanjo uzuia Magonjwa mengi miongoni mwao ni kifaduro, Pepopunda na Dondakoo haya ni baadhi ya magonjwa ambayo uzuiwa na Aina hii ya chanjo, tunaona kwamba hii chanjo Ina nguvu sana hasa kwa watoto kwa hiyo akina Mama na walezi wanapaswa kuhimizwa kuwapeleka watoto kwenye chanjo Ili waweze kuepuka haya magonjwa hatarishi kwa watoto.
2. Kwa kuwa hii chanjo ina mchanganyiko na ukinga magonjwa mbalimbali kama vile Pepopunda ambayo usaidia au kuzuia kukakamaa kwa misuli kwa sababu misuli ikikajamaa usababisha maumivu makali kwa mtoto, kwa hiyo mtoto akipata chanjo ya Pepopunda misuli inakuwa kwenye hali ya kawaida na mtoto anaweza kuishi vizuri tu na kuendelea na maisha yake kama kawaida, kwa hiyo akina Mama na walezi wanapaswa kuwapeleka watoto wao Ili kupata chanjo ya kuzuia Pepopunda Ili kuepuka matatizo kwa mtoto.
3. Chanjo hii Inazuia na kifaduro, kwa sababu kifaduro uharibifu mfumo wa hewa na kusababisha kikohozi kwa mtoto kwa ambacho uchukua wiki nne mpaka nane tunaona hii ni hatari kwa mtoto kupata kikohozi kwa mda mrefu wa Aina hii, kwa hiyo hii chanjo utolewa pia kwa watoto na wachanga na wanawake wenye mimba Ili kuweza kuwakinga dhidi ya matatizo makubwa yanayoweza kujitokeza kama mtoto hajapata chanjo ya namna hii kwa hiyo tunapaswa kuhimiza akina Mama na walezi wahakikishe kuwa watoto wao wanapata chanjo ya Aina hii.
4. Pia chanjo hii isipotolewa inaweza kusababisha maambukizi kwenye Koo la hewa na kusababisha mgonjwa hashindwe kupumua na hatimaye na kifo kinaweza kutokea, kwa hiyo ugonjwa huu unaitwa Donda Koo. Kwa hiyo tunapaswa kuwapatia watoto wetu chanjo ya namna hii Ili kuepuka madhara makubwa zaidi.
5. Mtoto Upata chanjo hii akiwa na miezi sita baada ya kuzaliwa na baadae kila baada ya wiki nne mpaka pale anapofikisha miezi mitatu, kwa hiyo siku hizi zinapaswa kuzingatiwa kwa akina Mama na kwa walezi wa watoto.
6. Kwa sababu hii chanjo utolewa kwa watoto inaweza kuleta matokeo kwa mtoto ambayo yanaweza kumfanya mama akawa na wasiwasi juu ya mtoto kama vile kidonda kidogo kwenye sehemu ambayo wamepitishia dawa, wakati mwingine sehemu hiyo inaweza kuwa nyekundu,au sehemu hiyo inaweza kuvimba kwa hiyo mama inabidi hasiogope Bali ajue ni kawaida kwa mtoto mdogo kuwa hivyo baada ya kupata Aina hii ya chanjo.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inahusu njia na namna ya kumhudumia aliyeingiwa na nyoka. Nyoka ni kiumbe ambacho Kina sumu kali na mtu akifinywa na nyoka asipohudumiwa anaweza kupata ulemavu au kupoteza maisha
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kuyatunza macho
Soma Zaidi...Kupanda kwa msukumo wa damu ni ktendo ambapo moyo husukuma damu kwa nguvu kuliko kawaida ambapo hupelekea matatizo mengi kwenye mwili
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu magonjwa ya vidonda vya tumbo, ni hatari inayotokea kwa mtu ambaye haujatibiwa vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa mifupa mwilini, mifupa ni mojawapo ya tushy zilizounganika na ufanya kazi kubwa kwenye mwili.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi za vitamin B na makundi take
Soma Zaidi...Post hii inahusu umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa mama wajawazito na wanaonyonyesha. Ni hatua ya kupima Mama akiwa mjamzito na wakati wa kunyonyesha ili kuepuka hatari ya kumwambikiza mtoto
Soma Zaidi...Hii posti inahusu zaidi sifa za mkojo usio wa kawaida,ukiona mkojo wa namna hii unapaswa kwenda hospitalini kwa matibabu au vipimo vya zaidi.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mambo yanayosaidia kuboresha afya
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe, ni kipindi ambacho ni kutoka utotoni kwendea ujana.
Soma Zaidi...