Posti hii inahusu zaidi sababu za kumwosha Mgonjwa mwili mzima,ni sababu ambazo umsaidie mgonjwa ili aweze kupata nafuu mapema na kumsaidia kama tutakavyoona hapo chini
Sababu za kumwosha Mgonjwa mwili mzima.
1. Kumweka mgonjwa kwenye hali ya usafi na kumfanya ajisikie vizuri wakati akiwa kitandani na wakati Watu wanakuja kumwona.
2. Kuzuia maupele kwenye ngozi na kuufanya mwili uwe huru na kuzuia magonjwahiyo mbalimbali yanayoweza kujitokeza kwa sababu ya uchafu kwenye ngozi ya mgonjwa.
3. Kusaidia mzunguko wa damu uenda vizuri kwa sababu kama kuna uchafu umegandamana kwenye ngozi ni vigumu kwa damu kuweza kusafiri vizuri.
4. Kushusha joto la mwili kama liko juu ni kawaida kama joto la mwili liko juu ukioga kwa maji ya uvugu vugu joto la mwili linashuka kwa kiasi.
5. Kuzuia bakteria na wadudu wengine kama vile chawa za kwenye nguo ambazo uja kwa sababu ya kuwepo kwa uchafu kwa kufanya usafi wa mwili mzima mara kwa mara wadudu hao hawawezi kuonekana tena.
6. Kumfanya mgonjwa aweze kujisikia vizuri na anaweza kuonekana vizuri pia kumfanya mgonjwa awe na usingizi kwa sababu uchafu umekosesha mgonjwa usingizi akioga tu anaweza kusinzia vizuri.
7. Kwa hiyo na jamii nzima inapaswa kujua kuwa wagonjwa wetu wanapaswa kuwa wasafi mda wote kwa sababu ukimfanyia mgonjwa usafi unamsaidia kupona kwa hiyo wagonjwa wetu walioko majumbani na mahospitali hasa hasa wale ambao hawawezi kujifanyia kitu tuwaoshe kwa kufanya hivyo tunawatia matumaini na wataweza kupata nafuu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Unapokuwa na kizunguzungu unashindwa kuudhibiti mwili wako, unaweza kuanguka kabisa.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa protini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za tumbo,tumbo ni sehemu ya mwili ambayo ushughilika na kutunza chakula,
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kqa mgonjwa aliyeingiliwa na kitu au uchafu kwenye sikio.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu namna ya kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima, ni njia ambazo utumika kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima au kumwosha Mgonjwa hasa wale walio mahututi na hawawezi kuamka kitandani.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya fati na mafuta
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi jinsi moyo unavyosukuma damu, moyo ni ogani ambayo usukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyekula chakula chenye sumu, kula sumu ni kitendo Cha kula kitu chochote kama dawa,pombe, kemikali na chakula kichafu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa mifupa mwilini, mifupa ni mojawapo ya tushy zilizounganika na ufanya kazi kubwa kwenye mwili.
Soma Zaidi...