Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria ama syntax za kuandika javascript. Hii itakuwezesha kuelwa zaidi code za javascript.
Katika somo hili utajifunza kanuni za kuandika code za javascript ama javascript statement.Lamda kwanza nianze kukujuza maana ya hili neno statement. Ni kuwa kwenye program ya kikompyuta kuna code amabazo ni maelekezo ambayo kompyuta hupewa ili kufanya jambo fulani. Sasa hizi code ama haya maelekezo ndio huitwa statement.
Katika somo hili utajifunza kanuni za kuandika hizi statement. Kanuni hizi zitaweza kukuongoza kwa ufupi uweze kugunduwa kama kwenye code zako kuna tatizo. Na kama lipo nini kimesababisha. Hivyo tutajifunza syntax ya javascript.
Kabla hujasonga mbele zaidi na somo hili, nikujuze kuwa javascript statement inaweza kuwa na vitu hivi Values, Operators, Expressions, Keywords, na Comments. Value ni thamani ambazo zinaweza kuwa ni thamani za variable, operator ni alama za kihesabu kama + kumaanisha jumlisha, Expression ni mkusanyiko wa variable, value na operator, na comment hapa ni sehemu ambayo programmer ama mtu anayeandika hizo code kuweka kumbukumbu zake, ili baadaye aweze kukumbuka.
Kanuni za kuandika javascript:
Matumizi ya semicolon (;)
Weka alama hii ya semicoloni mwishoni mwa ststement yako. kwa mfano:
Mfano: 1
<!DOCTYPE html>
<html>
<body>
<p id="demo"></p>
<script>
let x, y, z;
x = 5;
y = 6;
z = x + y;
document.getElementById("demo").innerHTML =
"The value of z is " + z + ".";
</script>
</body>
</html>
Hapo juu utaona mwishoni mwa kila msitari kuna alama ya semicolon. Pia unaweza kuunganisha statement nyingi katika msitari mmoja na kutenganisha kwa semicoloni.
Mfano 2
<!DOCTYPE html>
<html>
<body>
<p id="demo"></p>
<script>
let x, y, z; x = 5; y = 6; z = x + y; document.getElementById("demo").innerHTML = "The value of z is " + z + ".";
</script>
</body>
</html>
Matokeo ya statement ya kwanza, na ya pili ni sawa, ijapokuwa hii ya pili ina mistari kidogo ya code, ni kwa saabu imeunganishwa pamoja na kutengenishwa kwa alama ya semicolon kwa kila statement.
Kuruka nafasi wakati wa uandishi (White Space):
Ni kuwa wakati unaandika huwa tunaruka nafasi, huwenda zikawa nyingi ama moja. Sasa katika javascript nafasi ambayo itahisabika kwenye code ni moja tu, hizo ambazo umeongeza javascript hazita zitambuwa na hasita athiri matokeo ya code zako.
Hivyo unaweza kuruka nafasi kadiri uwezavyo, ili kuweza kuboresha muonekano wa code zako. Angalia mifano ya code hizo hapo chini majibu yake ni sawa.
Mfano 3
<!DOCTYPE html>
<html>
<body>
<p id="demo"></p>
<script>
document.getElementById("demo").innerHTML = "haloo javascript";
</script>
</body>
</html>
Mfano wa 4
<!DOCTYPE html>
<html>
<body>
<p id="demo"></p>
<script>
document.getElementById ("demo"). innerHTML = "haloo javascript";
</script>
</body>
</html>
Urefu wa msitari wa code
urefu wa msitari wa code hauwezi kuathiri matokeo ya code. Hata hivyo inashauriwa usizindi character 80. Inashauriwa pia kupunguz">...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowKsomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku dili na html form kwenye javascript. Javascript inaweza kufanya mengi kwenye html form.
Soma Zaidi...Katika project hii utakwenda kufunza jinsi utakavyoweza kutengeneza keyboard ya online kwa kutumia javascript
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa maandishi (text) wakati wa ku out put matokeo ya code
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript.
Soma Zaidi...Hii ni game ambayo utafikiria namba, ambayo inatakiwa iwe sawa na namba ambayo game imeiweka.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu javascript events. Event ni neno la Kiingereza lenye maana tukio wingi wake events kumaanisha matukio. Natumia ni kila ambacho kinatokea kwenye javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika variable. Hapa utajifunza sheria zinazohusu variable katika javascript
Soma Zaidi...