Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method.
Katika somo hili utajifunza kutumia method (function) kwenye string. Tulisha jifunza kwenye aina za data kuhusu string. Hapa tutakwenda kuangalia zaidi jinsi ya kuitumia string.
Tulipokuwa tunasoma object nilikueleza kuwa object ni variable. Katika javascript karibia variable zote utakazozitengeneza zinaweza kuwa ni object. Kwa mfano var web ="bongoclass". katika mfano huu variable web hapo ni object. Hivyo variable yetu itakuwa tayari kupokea method mbalimbali zinazohusu string object.
Kujuwa idadi ya character
Kujuwa idadi ya maneno tutatumia lenth kama built in property ya string. kwabnfano katika variable yetu web hapo tutasema web.length kumaanisha kuwa variable web ni object name na length ni object property ambayo value yake nibidadi ya character.
Ukihesabu neno Bongoclass utapata kuwa lina idadi yabherufi 10. Hivyo hiyo 10 itakuwa ndio property value.
<script>
var web="Bongoclass";
document.write(web.length)
</script>
Ku retrive string
Ku retrive string ni sawa na kusema kujuwa kila character ipo nafasi gani kwenye hiyo string. Na kumbuka kuwa kuhesabu tunaanza kwenye 0. Mfano kwenye string yetu Bongoclass tunataka kuangalia je character namba 4 inawakilisha herufi gani kwenye hiyovstrong?
<script>
var web="Bongoclass";
document.write(web[4])
</script>
Kujuwa nafasi ya neno
Hapa tunataka kujuwa je neno hili kwa mara ya kwanza limetokea kwenye nafasi ya ngapi. Yaani unapita character ngapi kutoka mwanzo wa string mpaka kulikuta hilo neno kwa mara ya kwanza.
Chukulia mfano wa hii string "Haloo karibu Bongoclass upate kujifunza bure, karibu sana" sasa hapa tunataka kujuwa neno karibu kwa mara ya kwanza limeonekana kuanzia character ya ngapi. Kama utahesabu hapo utaona neno karibu kwa mara ya kwanza linapatikana kuanzia character ya 6. Endapo hilo neno halijatokea utapata jibu -1.
<script>
var web="Haloo karibu Bongoclass upate kujifunza bure, karibu sana";
document.write(web.indexOf("karibu"))
</script>
Sasa endapo unataka kujuwa nafasi ya hilo neno lililotokea mara ya mwisho hapa tutatumia lastIndexOf hii ni method ambayo itatupa majibu tunayoyataka. Angalia hiyo string yetu hapo juu neno karibu limejitokeza mara mbili. Sasa tunataka tujuwe hiyo ya mwisho limejitokeza katika nafasi ha ngapi.
<script>
var web="Haloo karibu Bongoclass upate kujifunza bure, karibu sana";
document.write(web.lastIndexOf("karibu"))
</script>
Utaona hapo jibu ni 46, inamaana kuwa kwa mara ya mwisho neno karibu limejitokeza kuanzia character ya 46.
Katika indexOf na lastIndexOf hizi huangalia neno kama lilivyo yaani KaRibu na karibu ni maneno mawili tofauti. Hivyo kama hayatafanana haiwezi kukupa majibu. Sasa endapo utahitaji kutafuta neno bila kujali uandishi kama limechanganja herufi lakjni linasomeka sawa hapa tunatumia method ya search()
Mfano we.search("karibu") hii ni sawa na hizo method mbili tulojifunza kwani majibu yake ni sawa. Sasa angalia string hii "Haloo KariBu Bongoclass upate kujifunza bure, karibu sana." utaona hapo neno KariBU lipo mwanzo na neno karibu lipo mwisho.
<script>
var web="Haloo KariBu Bongoclass upate kujifunza bure, karibu sana.";
document.write(web.search("karibu"))
</script>
Utaona hapo umepata jibu 47 kwa maana karibu ya kwanza imeonekana haipo sawa na neno lililopo kwenye method yetu. Ili kufanya karibu ya kwanza itambulike tutatumia alama za back lash yaani /. Mfano search(/karibu/i) kisha tutaweka i kumaanisha insensitivity higyobkuifanya isijali uandishi ila izingatie kuwa neno linasomeka sawa.
<script>
var web="Haloo KariBu Bongoclass upate kujifunza bure, karibu sana.";
document.write(web.search(/karibu/i))
</script>
Tofauti kuu iliyopo kati ya indexOf na lastIndexOf na search ni kuwa hii ya search inakubali matumizi yavregular expression. Regular expression ni javascript expression ambayo inakuwa na paten maalumu. Inaweza kuwa na special character, herufi, namba, symbol na space character.
Kunyofoa maneno
Hapa tutakwenda kujifunza namna ya kunyofoa maneno kwenye string ka namna tunavyotaka.
Kwa mfano una string hii hapa "Bonhoclass ni tovuti inayokua fursa ya kujifunza elimu ya TEHEMA" sasa tunataka kunyofoa herufi kuanzia character ya 13 hadi ya 20 ili tupate nono jipya ambalo litatengenezwa kupitia character hizo.
Kufanya hivyo tutatumia method inayoitwa slice(). Itakachofanya hapo ni kukusanya hizo character na kupata neno moja. Kwa mujibubwa character yetu hapo tutapata tovuti
<script>
var web="Bonhoclass ni tovuti inayokua fursa ya kujifunza elimu ya TEHEMA";
document.write(web.slice(13, 20))
</script>
Pia method ya slice inaweza kuchukuwa negative hivyo kuanza kuhesabu kutoka mwisho kujabmwanzo. Kwa mfano hapo kwenye string yetu neno tovuti tutalipata kwenye -50 hadi -44 kama ukihesabu kutoka mwisho.
<script>
var web="Bonhoclass ni tovuti inayokua fursa ya kujifunza elimu ya TEHEMA";
document.write(web.slice(-50, -44))
</script>
...
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: JavaScript Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 260
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Simulizi za Hadithi Audio
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Madrasa kiganjani
Game 3: Mchezo wa kufikiria namba kwa kutumia javascript
Hii ni game ambayo utafikiria namba, ambayo inatakiwa iwe sawa na namba ambayo game imeiweka. Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 8: Aina za data zinazotumika kwenye javascript
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za data ambazo hutumika kwenye javascript Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 5: Jinsi ya kupangilia maandishi wakati wa ku output kwenye javascript
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa maandishi (text) wakati wa ku out put matokeo ya code Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 14: Jifunze kuhusu event kwenye javascript
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu javascript events. Event ni neno la Kiingereza lenye maana tukio wingi wake events kumaanisha matukio. Natumia ni kila ambacho kinatokea kwenye javascript. Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 15: Jinsi ya kukusanya user input
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript. Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 18: Jinsi ya kutumia switch case kwenye javascript
Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement. Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 10: Jinsi ya kuandika object na matumizi yake kwenye javascript
Ksomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika. Soma Zaidi...
Game 2: Jinsi ya kutengeneza tic toc game ya single player kwa kutumia javascript, html na css
Katika post hii utakwenda kujifunza kutengeneza game ya tic toc ya mchezaji mmoja na kompyuta yaani single player Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 7: Jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript. Katika somo hili tutakwenda kutumia mahesabu. Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 4: Jinsi ya kuandika variable kwenye javascript
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika variable. Hapa utajifunza sheria zinazohusu variable katika javascript Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 16: Jinsi ya kutumia html form kwenye javascript
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku dili na html form kwenye javascript. Javascript inaweza kufanya mengi kwenye html form. Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 23: Jinsi ya kutengeneza calculator yaani kikokotoo cha hesabu kwa kutumia javascript
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza kutumia javascript kutengeneza kikokotoo cha hesabu yaani calculator Soma Zaidi...