image

Maana ya Kuamini Siku ya Mwisho

Maana ya Kuamini Siku ya Mwisho

Maana ya Kuamini Siku ya Mwisho


katika Maisha ya kila siku Muumini wa kweli wa Siku ya Mwisho ni yule atakaye jitahidi kwa jitihada zake zote kufanya yafuatayo:




1. Kufanya wema kwa kadiri ya uwezo wake ili apate radhi za Allah (s.w) ili astahiki kupata makazi mema katika maisha ya akhera. Huingia katika biashara na Allah (s.w):Enyi mlioamini! Je! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo (Basi biashara yenyewe ni hii):- Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu; ikiwa mnajua (kuwa ni bora, basifanyeni).(Mkifanya haya) Atakusameheni dhambi zenu na atakuingizeni katika Mabustani yapitayo mito mbele yake na (atakupeni) maskani mazuri mazuri katika Bustani za milele: huku ndiko kufuzu kukubwa. Na (atakupeni) kingine mnachokipenda: Nayo ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi ulio karibu! Na wapashe habari njema waumini (61:10 -13).


Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waislamu nafsi zao na mali zao (watoe nafsi zao na mali zao katika kupigania dini) ili na yeye awape Pepo. Wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu; wanaua na wanauawa. Hii ndiyo ahadi aliyojilazimisha (Mwenyezi Mungu) katika Taurati na Injili na Qur ani.Na ni nani atekelezaye zaidi ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyofanya naye (Mwenye Mungu) Na huko ndiko kufuzu kukubwa (9: 111)




2. Kujiepusha na maovu kwa kadiri ya uwezo wake na kila mara kuleta Istighfar na dua, kumuomba Mola wake amuepushe na adhabu ya akhera. Katika Qur-an tunafahamishwa waja wa Rahman (Waumini wa kweli) ni wale waombao:“Mola wetu tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea.Hakika hiyo (Jahannam) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa.” (25:65-66)




3. Kuleta toba ya kweli atakapoteleza kwa kufanya jambo lolote lile kinyume na radhi ya Allah (s.w). Mwenyewe Allah (s.w) anatuamrisha “Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allah toba ya kweli, huenda Mola wenu Atakufutieni maovu yenu na kukuingizeni katika pepo zipitazo mito mbele yake, ...” (66:8) “Na ombeni msamaha kwa Mw enyezi Mungu , hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa Kurehemu.” (73:20)


Allah (s.w) ameahidi kuwasamehe wale watakao leta toba ya kweli kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri; basi hao ndio Mwenyezi Mungu ataw abadilishia maovu yao kuwa mema; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kw eli kw eli kw a Mw enyezi Mungu.(25:70-71)Kisha hakika Mola wako kwa wale waliofanya ubaya kwa ujinga, kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mema; bila shaka Mola wako baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu (16:119)Na (wewe Mtume) wanapofika wale wanaoamini Ayazetu(na hali wamekosa kidogo; wanakuja kutubia)waambie “Amani iwe juu yenu, Mola wenu amejilazimisha rehema,kwamba atakayefanya miongoni mwenu uovu kw a ujinga, Mw enyezi Mungu atamghufiria kwani yeye ni Mwingi wa Rehema. (6:54)




Sema, “Enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu; bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote; hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.” (39:53)
Kutokana na aya hizi, tunajifunza kuwa toba ya kweli itapatikana kwa kuzingatia masharti yafu atayo:




1.Mwenye kuleta toba awe amefanya kosa kwa ujinga au kwa kutelezeshwa na vishawishi vya mazingira ya kishetani bila ya kudhamiria.




2.Baada ya kutanabahi kuwa amemuasi Mola wake, Muumini wa kweli atajuta na kuilaumu nafsi yake, na kulalama kwa Mola wake, kama walivyolalama wazazi wetu, Adam (a.s) na Hawwa (r.a): “Mola wetu!Tumedhulumu nafsi zetu, na kama hutatusamehe na kuturehemu,bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye khasara.” (7:23)
Pia katika Hadithi iliyosimuliwa na Abubakar Swidiq (r.a) na kukubaliwa na Maimamu wote wa hadith, Mtume (s.a.w) ametufundisha kuleta majuto moyoni mwetu kwa kuomba:“Ewe Mw enyezi Mungu ! Hakika nim edhulum u nafsi yangu dhulmakubw a.Hapanayeyotemw enyekusamehedhambi isipokuwa wewe tu.Basi nakuomba unipatie msamaha utukaokwakonaunihurumie.HakikaweweniMsamehevu, Mrehemevu.”



3.Kuazimia moyoni kuacha maovu.



4.Iwapo makosa yake yamehusiana na kudhulumu haki za watu, itabidi awatake radhi wale aliowakosea na kuwarejeshea haki zao zile zinazorejesheka.



5.Kuzidisha kufanya amali njema kwa kuzidisha kutoa sadaqa, kuzidisha kuleta swala na funga za sunnah, na kuzidisha juhudi ya kupigania dini ya Allah kwa mali na nafsi.
Rejea Qur-an (61:10-13) na (9:111).




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 605


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu (EDK form 1: mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu Soma Zaidi...

Dhana ya ibada kwa mtazamo wa uislamu..
Mtazamo wa uislamu juu ya ibada (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maadili kati surat Al-Hujurat (49:1-13)
Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Kujielimisha kwa Ajili ya Allah (s.w).
Elimu ndiyo zana aliyotunukiwa mwanadamu ili aitumie kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Allah (s. Soma Zaidi...

Maana ya uislamu.
Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti. Soma Zaidi...

Muhtasari wa madili malezi ya jamii kama ilivyobainishwa katika Qur-an
(v)Kuwaombea dua wazazi. Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat ash-Shuura
“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele). Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Furqaan (25:64-76)
Soma Zaidi...

Mgawanyiko wa Elimu kwa mtazamo wa kikafiri
Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera. Soma Zaidi...

Athari za vita vya Uhud
Vita vya uhudi viliweza kuleta athari nyingi. Post hii itakuletea athari baadhi za vita hivyo. Soma Zaidi...

Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake
Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...