image

KUAMINI SIKU YA MALIPO

KUAMINI SIKU YA MALIPO

KUAMINI SIKU YA MALIPO
Kuamini siku ya Malipo ni miongoni mwa Nguzo Muhimu katika Nguzo za Iman ya Kiislamu. Kwa hakika ndiyo Msingi wa nguzo nyinginezo za Iman. Mtu hawezi kuwa muumini wa kweli mpaka awe na yakini kuwa pana maisha mengine baada ya kufa. Katika sehemu mbalimbali katika Qur’an Allah (s.w) ameiambatanisha nguzo hii ya “Kuamini Akhera” na “Kumuamini Allah” ambayo ni nguzo ya kwanza.
Allah (s.w) anatuambia:“…Na mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali (na haki) (4:136)
Pia anasema:"Bila shaka mnao mfano mwema (ruwaza nzuri) kwa mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa Mwenye kumwogopa Mwenyezi mungu na Siku ya Mwisho, na kumtaja Mwenyezimungu sana” (33 :21)


“Sio wema (peke yake tu) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi, bali wema hasa ( ni wale) wanaomwamini Allah na Siku ya Mwisho…” (2:177)
Muislamu wa kweli anaamini kuwa maisha haya ya duniani ni maisha yana mwisho, yatakoma na kuna siku nyingine ambayo hakuna siku baada ya siku hiyo, kisha yanakuja maisha ya pili ambayo ndiyo maisha halisi ya kweli ya nyumba ya Akhera.Kupatikana kwa siku hiyo ambayo hakuna siku baada ya siku hiyo, kutakuja baada ya Ulimwengu wote kutoweka na kubaki ufalme wa Allah (s.w) tu yeye peke yake, Aliye dhati ya kweli.
Malaika, Milima, Majini, Binaadamu, maji na kila kilicho na uhai kitatoweka kipende kisipende. Allah anatutanabahisha hili kwa kusema:“ Kila aliye juu ya ardhi atakufa na atasalia Mola wako Mwenye Utukufu (wa kweli) usio na mahitaji na fadhila kamili” (55:26 – 27)Baada ya kila kilicho hai kutoweka na kubaki Ufalme wa Allah (s.w) kama Alivyokuwa kabla ya kuumba chochote, hapo Allah atawafufua viumbe na kuwakusanya kwake wote ili apate kuwalipa kwa lile walilolifanya katika ardhi hii, wapate Pepo kama walikuwa watiifu kamili kwa Mola wao au wastahili Moto kwa kuwa walishika miungu mingine badala ya Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao. Maisha hayo ndiyo maisha halisi na yenye kudumu daima! Allah (s.w) anatubainishia kuwa:“Kwani hawaelewi kuwa wao watafufuliwa? Ndani ya Siku tukufu, Siku watasimama watu kwa amri ya Bwana wa viumbe vyote? (83: 4-6).
Pia anasema:“Makafiri wanadai kuwa hawatafufuliwa!, (sema Kwanini msifufuliwe?!) Naapa kwa Mola wangu Wallah!: Mtafufuliwa na kisha wallah! Mtaelezwa mlichokifanya duniani, hayo kwa Allah ni sahali (64:7)
Muislamu wa kweli anaamini kuwa Qiyama kitasimama na kila mja atalipwa kwa kila tendo alilolifanya, dogo au kubwa kama Allah (s.w) anavyotubainishia katika Qur’an


“Basi atakayefanya (jambo lolote) la kheri lenye uzito mfano wa Dharra (Atom) ataliona jaza yake. Na atakayefanya (jambo lolote) la shari lenye uzito mfano w a Dh a rra (A tom) a ta lion a jaz a y ake ”. (99: 7 - 8)
Pia Allah (s.w) anamkumbusha Mtume (s.a.w) juu ya wasia wa Mzee Luqmaan kwa kijana wake ambao kwa hakika ndio wasia bora wa kila mzazi kumpa kijana wake, anasema:“Ewe mw anangu, jambo lolote lililo na uzito wa chembe ya Hardal (au ndogo kuliko hiyo) ikiwa katikati ya jabali, au juu mbinguni au chini ardhini Allah Atalileta (amlipe aliyelifanya) Hakika Allah ni mwingi wa habari na mwenye ujuzi (hasa)” (31: 16)
                   


           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 612


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Taathira ya Imani ya Malaika katika maisha ya kila siku
Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini. Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Furqaan (25:64-76)
Soma Zaidi...

Ni ipi maana ya Imani katika Uislamu, na ni zipi sifa za muumini.
Katika Uislamu imani inanguzo kuu 6.Pia muumini anatakiwa ajipambe na sifa za waumini. Posti hii itakufundisha kuhusu imani katika Uislamu. Soma Zaidi...

Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na nini? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo) Soma Zaidi...

Maadili katika surat luqman
Soma Zaidi...

Imani ya Kiislamu na ni nani muumini?
Soma Zaidi...

Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume
Soma Zaidi...

Ndoto ya Nabii Yusufu(a.s) Yatimia
Yusufu(a. Soma Zaidi...

Maswali juu ya mtazamo wa uislamu kuhusu dini
Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kuangamizwa Waovu na Kuokolewa Waumini
Baada ya kuonywa wasionyeke, Allah(s. Soma Zaidi...

Mtazamo wa kikafiri juu ya maana ya dini.
Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini. Soma Zaidi...

KUAMINI MALAIKA
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...