picha

KUAMINI SIKU YA MALIPO

KUAMINI SIKU YA MALIPO

KUAMINI SIKU YA MALIPO




Kuamini siku ya Malipo ni miongoni mwa Nguzo Muhimu katika Nguzo za Iman ya Kiislamu. Kwa hakika ndiyo Msingi wa nguzo nyinginezo za Iman. Mtu hawezi kuwa muumini wa kweli mpaka awe na yakini kuwa pana maisha mengine baada ya kufa. Katika sehemu mbalimbali katika Qur’an Allah (s.w) ameiambatanisha nguzo hii ya “Kuamini Akhera” na “Kumuamini Allah” ambayo ni nguzo ya kwanza.
Allah (s.w) anatuambia:“…Na mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali (na haki) (4:136)
Pia anasema:"Bila shaka mnao mfano mwema (ruwaza nzuri) kwa mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa Mwenye kumwogopa Mwenyezi mungu na Siku ya Mwisho, na kumtaja Mwenyezimungu sana” (33 :21)


“Sio wema (peke yake tu) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi, bali wema hasa ( ni wale) wanaomwamini Allah na Siku ya Mwisho…” (2:177)
Muislamu wa kweli anaamini kuwa maisha haya ya duniani ni maisha yana mwisho, yatakoma na kuna siku nyingine ambayo hakuna siku baada ya siku hiyo, kisha yanakuja maisha ya pili ambayo ndiyo maisha halisi ya kweli ya nyumba ya Akhera.



Kupatikana kwa siku hiyo ambayo hakuna siku baada ya siku hiyo, kutakuja baada ya Ulimwengu wote kutoweka na kubaki ufalme wa Allah (s.w) tu yeye peke yake, Aliye dhati ya kweli.
Malaika, Milima, Majini, Binaadamu, maji na kila kilicho na uhai kitatoweka kipende kisipende. Allah anatutanabahisha hili kwa kusema:“ Kila aliye juu ya ardhi atakufa na atasalia Mola wako Mwenye Utukufu (wa kweli) usio na mahitaji na fadhila kamili” (55:26 – 27)



Baada ya kila kilicho hai kutoweka na kubaki Ufalme wa Allah (s.w) kama Alivyokuwa kabla ya kuumba chochote, hapo Allah atawafufua viumbe na kuwakusanya kwake wote ili apate kuwalipa kwa lile walilolifanya katika ardhi hii, wapate Pepo kama walikuwa watiifu kamili kwa Mola wao au wastahili Moto kwa kuwa walishika miungu mingine badala ya Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao. Maisha hayo ndiyo maisha halisi na yenye kudumu daima! Allah (s.w) anatubainishia kuwa:“Kwani hawaelewi kuwa wao watafufuliwa? Ndani ya Siku tukufu, Siku watasimama watu kwa amri ya Bwana wa viumbe vyote? (83: 4-6).
Pia anasema:“Makafiri wanadai kuwa hawatafufuliwa!, (sema Kwanini msifufuliwe?!) Naapa kwa Mola wangu Wallah!: Mtafufuliwa na kisha wallah! Mtaelezwa mlichokifanya duniani, hayo kwa Allah ni sahali (64:7)
Muislamu wa kweli anaamini kuwa Qiyama kitasimama na kila mja atalipwa kwa kila tendo alilolifanya, dogo au kubwa kama Allah (s.w) anavyotubainishia katika Qur’an


“Basi atakayefanya (jambo lolote) la kheri lenye uzito mfano wa Dharra (Atom) ataliona jaza yake. Na atakayefanya (jambo lolote) la shari lenye uzito mfano w a Dh a rra (A tom) a ta lion a jaz a y ake ”. (99: 7 - 8)
Pia Allah (s.w) anamkumbusha Mtume (s.a.w) juu ya wasia wa Mzee Luqmaan kwa kijana wake ambao kwa hakika ndio wasia bora wa kila mzazi kumpa kijana wake, anasema:



“Ewe mw anangu, jambo lolote lililo na uzito wa chembe ya Hardal (au ndogo kuliko hiyo) ikiwa katikati ya jabali, au juu mbinguni au chini ardhini Allah Atalileta (amlipe aliyelifanya) Hakika Allah ni mwingi wa habari na mwenye ujuzi (hasa)” (31: 16)




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views 2830

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 ai web app     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Ni lipi lengo la Elimu katika yislamu?

Ni lipi lengo kuu la Elimu katika uislamu (Edk form 1 Dhanaya Elimu)

Soma Zaidi...
Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu

Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu).

Soma Zaidi...
Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)

"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu

Soma Zaidi...
Kujiepusha na kula mali ya Yatima

Waumini wanawajibika kuwatunzia mayatima mali zao na kuwakabidhi wanapofikia baleghe yao baada ya kuwajaribu na kuthibitisha kuwa wanao uwezo wa kutunza mali zao - Rejea Qur-an (4:5-6).

Soma Zaidi...
KAZI ZA MALAIKA

Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi.

Soma Zaidi...