(v)Kuwaombea dua wazazi.
(v)Kuwaombea dua wazazi.
(vi)Kuwasaidia wenye shida.
(vii)Kutotumia mali kwa ubadhirifu.
(viii)Kujitaabisha katika kutafuta maisha ili kuwahudumia wazazi ipasavyo.
(ix)Kujiepusha na ubakhili.
(x)Kutowauwa watoto kwa kuhofia umasikini.
(xi)Kujiepusha na zinaa kwani ni njia mbaya na ni uchafu.
(xii)Kujiepusha na kula mali za yatima.
(xiii)Kuchunga ahadi.
(xiv)Kutimiza vipimo wakati wa kupima na kutumia mizani iliyo sawa au kipimo kilicho sawa.
(xv) Kutofuata mambo usiyo na ilimu nayo,yaani kutofuata mambo kwa kibubusa
2. An-Nuur (24:1-31,58-63)pamoja na (7:26),(33:32,59)
(i)Kujiepusha na zinaa.
(ii)Tusifunge ndoa na wenza waovu.
(iii)Kujiepusha kuwasingizia uovu waumini.
(iv)Ni tabia njema kuwa mwenye kufanya toba mara kwa mara.
(v)Tujiepushe na tuhuma mpaka tupate ushahidi. (vi)Kujitahidi kuwadhania vyema waumini.
(vii)Kujiepusha na kutangaza habari mbaya za watu. (viii)Kujiepusha na maovu na machafu (ni amali za shetani).
(ix)Kujiepusha na jazba na viapo.
(x)Kushikamana na kusamehe.
(xi)Tusiingie majumba ya watu mpaka tupate ruhusa (tupige hodi).
(xii)Tukiambiwa turudi tusingie basi turudi. Hakuna kupiga hodi kwenye majumba ya Ummah.
(xiii)Kujiepusha na kutazama yale yaliyokatazwa na sheria ya Allah (s.w).
(xiv)Kujiepusha na zinaa na kulinda tupu zetu.
(xv)Kujisitiri kisheria na kuchunga mipaka ya mahusiano, sauti na mavazi.
(xvi)Wanawake wakae na kujituliza majumbani kwao, wasitoke ila kwa dharura muhimu.
(xvii)Kujitakasa kutokana na uovu na machafu.
3. Luqmaan (31:12-19)
(i)Kuwa na Hikma
(ii)Kumshukuru Allah (s.w).
(iii)Kutoa nasaha njema kwa watoto.
(iv)Kutomshirikisha Allah (s.w), kwani ni dhambi kubwa.
(v)Kuwafanyia wema (Ihsaan) wazazi wetu.
(vi)Kutowatii wazazi kama wakitupeleka vibaya (wakitupelekea kumshirikisha Allah) lakini kukaa nao kwa wema.
(vii)Kushika njia ya waja wema wanaoelekea kwa Allah. (viii)Kuwa na tahadhari katika kila jambo.
(ix)Kuwa na yakini kuwa Allah (s.w), ndiye Mwenye kuruzuku na Mwenye kumlipa mja kile anachostahiki.
(x)Kusimamisha swala.
(xi)Kuamrisha mema.
(xii)Kukataza mabaya.
(xiii)Kuwa na subira katika yale yatakayotusibu. (xiv)Kutowatizama watu kwa dharau.
(xv)Kutotembea katika ardhi kwa maringo. (xvi)Kujiepusha na majivuno na kujifaharisha. (xvii)Kushika mwendo wa kati na kati.
(xviii)Kutopaza sauti, kujiepusha na tabia ya kupiga kelele.
4. Al-Ahqaaf (46:15-18)
(i) Kuwafanyia wema wazazi/walezi.
(ii)Kumuomba Allah (s.w) atupe kizazi chema. (iii)Kufanya toba mara kwa mara.
(iv)Kuwashukuru wazazi kwa kuwatii na kuwaombea dua na msamaha kwa Allah(s.w).
(v)Kufuatilia kwa makini usia mwema wanaotupa wazazi.
(vi )Kutowaka ri pia wazazi/walezi wetu au kuwafanyia mambo mabaya.
5. Al-Hujurat (49:1-13) pamoja na (24:27-29),(33:53), (4:86)
(i)Kutotanguliza maneno/kauli mbele ya kauli ya Allah (s.w) na Mtume wake yaani tusifuate matashi yetu kinyume na maamrisho/matazo ya Allah(s.w) na mtume wake
(ii)Tusipaze sauti zetu juu ya sauti za viongozi wetu.
(iii)Kutowaita watu madirishani au kusema nao mad irishan i.
(iv)Kufanyia uchunguzi taarifa yoyote kabla ya kuifanyia kazi.
(v)Kupatanisha ndugu na jamaa kwa uadilifu.
(vi)Kuunganisha udugu wa Kiislamu.
(vii)Kujiepusha na dharau na kujiona (kujikweza). (viii)Kutoitana majina mabaya.
(ix)Tusitukanane kwa makabila, rangi, taifa au vyeo n.k.
(x)Kujiepusha na kuwadhania watu dhana mbaya.
(xi)Kujiepusha na kupeleleza habari za watu. (xii)Kujiepusha na kusengenya.
(xiii)Kumcha Allah (s.w) ukweli wa kumcha).
(xiv)Kupiga hodi majumba ya watu kabla ya kuingia na kuwatolea salamu wenyeji.
(xv)Tunapokaribishwa majumbani mwa watu tushughulike
na kile kilichotupeleka na tukimaliza tutawanyike. (xvi)Tukiongea na wanawake ambao si maharim zetu
tuongee nao nyuma ya Pazia.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 666
Sponsored links
👉1
kitabu cha Simulizi
👉2
Madrasa kiganjani
👉3
Simulizi za Hadithi Audio
👉4
Kitabu cha Afya
👉5
Kitau cha Fiqh
👉6
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
MAANA NA HUKUMU YA TAJWIDI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...
Kwa namna gani Allah huwasiliana na wanadamu kwa kupitia ndoto.
Ndoto za kweli ni moja kati ya njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu. Soma Zaidi...
mafunzo ya TAWHID, maarifa na imani ya dini ya kiislamu
YALIYOMO1. Soma Zaidi...
Athari za kumuamini mwenyezi Mungu katika maisha ya kila siku
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Lengo la maisha ya mwanadamu
Soma Zaidi...
Ni lipi lengo la Elimu katika yislamu?
Ni lipi lengo kuu la Elimu katika uislamu (Edk form 1 Dhanaya Elimu) Soma Zaidi...
Kumuamini mwenyezi Mungu..
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
KUAMINI MALAIKA
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...
Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah
Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe). Soma Zaidi...
Elimu ya mwingozo na elimu ya mazingira katika uislamu
Mahusiano kati ya elimu ya mwongizo na elimu ya mazingira katika uislamu. Soma Zaidi...