Ingawa hakuna ajuaye Kiyama kitakuwa lini, kupitia Aya mbali mbali za Qur’an na Hadith kadhaa za Mtume (s.a.w) zinabainisha kwa uwazi juu ya dalili mbali mbali za kusimama kwa kiyama. Ziko Dalili kubwa na Dalili ndogo, na zipo ambazo tayari zimekwishadhihiri nyingine zinaendelea na ambazo bado kudhihiri kwake; Kama Allah Aliyetukuka anavyotubainishia:
“Kwani wanangoja jingine ila kiyama kiwajie kwa ghafla? Basi alama zake(hicho kiyama) zimekw ishakuja. Kutaw afaa w api kukumbuka wakati kitakapow ajia ? ” (47:18)
Pia anasema“Saa ya Kiyama imekaribia; na mwezi umepasuka” (54 :1)
Dalili Ndogo za Kiyama:
(i)Watu kumiliki mali na hali ya kuwa ni madhalimu wasio na uadilifu
(ii)Kuenea mno kwa riba kiasi cha kila mtu kuathiriwa nayo
(iii)Kuenea kwa kila aina ya Ulevi
(iv)Wanawake kukithiri katika kuvaa nguozinazochochea zinaa (nguo nyepesi za kuangaza , fupi na za kubana)
(v)Wanawake watawaiga wanaume katika mavazi kadhalika wanaume watawaiga wanawake katika mavazi. Leo wanaume wanavaa hereni, shanga, bangili, na mengineyo yanayojulikana kuwa mapambo ya kike.
(vi)Kuenea kwa Liwati (kujimai baina ya jinsia moja-wanaume kuwaendea wanaume wenzao na wanawake kuwaendea wanawake wenzao) Homosexuality and Lesbiansm. Jambo hili leo limehalalishwa na watu wa Magharibi, pia hapa kwetu Afrika na hasa Kenya na Afrika kusini ni halali Mwanaume kuolewa na mwanamume mwenzake! Subhaanallah!
(vii)Kuenea sana kwa zinaa na itafanyika hadharani.
(viii)Watu hawatawajali tena wazazi wao, ndugu zao najamaa zao badala yake watawathamini nakuwasaidia rafiki zao.
(ix)Watu watachukia sana kulea watoto.
(x)Unafiki utaenea sana.
(xi)Mauaji yataenea sana, kwa kutoka Taifa mojakwenda kulivamia Taifa jingine na watu baadhikuwaua wengine kwa maslahi yao binafsi
(xii)Watu wataona uzito sana kutoa sadaka
xiii)Watawala watakuwa wengi sana lakini hakuna atakayekuwa mkweli na mwadilifu
xiv)Mtu ataheshimiwa kwa shari yake na si kwa uadilifu na wema wake.
xv)Kujifaharisha kwa misikiti
xvi)Pamoja na haya yote, bado kutakuwepo na kundi dogo tu la waislamu ambalo litadumu katika njia iliyonyooka na halitatetereka kwa lolote.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Wakatibmeingibe Allah anapotaka kuwasiliana na wanadamu hutuma Malaika wake.
Soma Zaidi...Kipengele hichi kinahusu mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu.sababu za mgawanyiko wa elimu udio sahihi katika uislamu.
Soma Zaidi...Kwa kutumia akili yako unaweza kumtambua Allah bila ya shaka yeyote ile. Postbhii itakufundisha nafasi ya akilonkatika kutambuwa uwepo na Uwezo wa Allah.
Soma Zaidi...“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele).
Soma Zaidi...Kwenye mada hii tutajifunza shahada mbili,tafsiri ya shahada kstika maisha ya kila siku.
Soma Zaidi...