Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya vitabu vya Allah (s.w). Vitabu vya Allah (s.w) vimeshushwa kupitia kwa Mitume mbali mbali.
“Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na tukaviteremsha Vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu...” (57:25).
Vitabu vya Allah (s.w) ni vingi lakini tunavyovifahamu ni vile vilivyotajwa katika Qur-an kama ifuatavyo:
Suhufi kwa Ibrahimu (a.s)
Taurati kwa Mussa (a.s)
Zaburi kwa Daud (a.s)
Injili kwa Issa (a.s)
Qur-an kwa Muhammad (s.a.w)
Lengo la kushushwa Vitabu vya Allah (s.w)Iimebainishwa wazi katika Qur-an kuwa vitabu vya Allah (s.w) vimeshushwa kupitia kwa Mitume wake ili kuwaongoza wanaadamu katika njia iliyonyooka. Njia iliyonyooka ni ile inayomuwezesha mwanaadamu kumuabudu Allah (s.w) katika kila kipengele cha maisha yake kwa kipindi chote cha uhai wake hapa ulimwenguni. Allah (s.w) amechukua ahadi ya kuwaletea watu mwongozo tangu awali pale alipowashusha wazazi wetu, Adamu (a.s) na mkewe (Hawwah) hapa ardhini kama tunavyojifunza katika Qur-an:
“Tukasema, shukeni humo nyote, na kama ukikufikieni uw ongozi utokao kw angu, basi w atakaoufuata uw ongozi wangu huo haitakuwa hofu juu yao wala haw atahuzunika.
Lakini wenye kukufuru na kuyakadhibisha maneno yetu, hao ndio watakaokuwa watu wa Motoni, humo watakaa milele”. (2:38-39).
Ahadi hii ameitekeleza Allah (s.w) kwa kuwaleta Mitume mbali mbali baada ya Adamu (a.s) na kuwashushia vitabu vyenye Uongozi na nuru. Qur-an inasisitiza:
“Hakika tuliteremsha Taurat yenye Uongozi na Nuru..” (5:44)
“Na tukawafuatishia (Mitume hao) Issa bin Maryam kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurat, na tukampa Injili iliyomo ndani yake Uongozi na nuru.” (5:46 )
“Ni mw ezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo (hii) Qur-an ili iwe Uongozi kwa watu na hoja zilizo wazi za Uongozi wa upambanui