Katika kutokomeza zinaa katika jamii, Uislamu hauanzii na kutoa adhabu kali ya kuwachapa wazinifu viboko 100 mbele ya hadhara au kuwapiga mawe mpaka wafe, bali umeanza na kukataza kuikurubia zinaa Qur'an (17:32) na kuweka mazingira yatakayopelekea kutoikurubia zinaa kwa kutoa maelekezo mbali mbali ya hijabu kama inavyodhihiri katika aya zifuatazo:
βWaambie Waislamu wanaume wainamishe macho yao (wasiangalie kwa jicho la matamanio), na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao; bila shaka Mwenyezi Mungu Anazo habari za (yote) wanayoyafanya." (24:30)
"Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika (navyo ni uso na vitanga vya mikono - na wengine wanasema na nyayo). Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa wanaume zao, au baba zao, au baba za waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenziwao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, (watumwa wao), au wafuasi wanaume wasio na matamanio (kwa wanawake) au watoto ambao hawajajua mambo yaliyohusu uke. Wala was ipige miguu yao ili yajulikane wanayoyaficha katika mapambo yao. Na tubieni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waislamu ili mpate kufaulu." (24:31)
"Enyi wake wa Mtume, nyinyi si kama yeyote tu katika wanawake wengine. (Nyinyi wakeze Mtume). Kama mnataka (kufanya jambo la ) kumcha Mwenyezi Mungu, basi msiregeze sauti (zenu mnaposema na wanaume) ili asitamani mtu mwenye ugonjwa moyoni mwake (kufanya mabaya na nyiye) na semeni maneno mazuri."
"Na kaeni majumbani mwenu, wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahili na simamisheni Sala na toeni Zaka, na Mtiini Mwenyezi Mungu na mtume Wake. Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi watu wa nyumba (ya Mtume), na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa." (33:32-3 3)
"Ewe Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya Hivyo kutapelekea upesi wajulikane (kuwa ni watu wa hishima ili) wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu." (33:59)
Kutokana na aya hizi tunapata maelekezo yafuatayo juu ya hijabu:
(i)Ili kuepukana na zinaa wanaume na wanawake wameamrishwa kuinamisha macho yao. Kui namisha macho ni msemo wenye maana ya kutowaangalia wanawake (kwa upande wa wanaume) au wanaume (kwa upande wa wanawake) kwa jicho la matamanio. Mara nyingi jicho la matamanio limekuwa ndio chanzo cha fitna baina ya mume na mke wasio maharimu, yaani walio ajinabi (wanaoweza kuoana).
(ii)Wanaume na wanawake pia wamehimizwa katika aya hizi kuwa wafanye jitihada za makusudi za kulinda tupu zao. Kulinda tupu ni kufanya jitihada za makusudi kujiepusha na maasia yote yanayosababishwa na utupu. Hili ni pamoja na kujiepusha na zinaa, ubasha, usagaji na kuchezea tupu ili kukidhi matashi ya ngono. Kukidhi matashi ya ngono ni halali tu ndani ya ndoa tena kwa kuliendea tendo hilo kama alivyoliruhusu Allah (s.w). Ubasha ni tendo ovu na haramu hata kwa mtu na mkewe. Wanawake ambao kimaumbile na kisaikolojia ni kivutio (attractive) cha wanaume wamepewa maelekezo zaidi ya Hijabu katika aya za (24:31), (33:32-33) na (33:59) kama ifuatavyo:
(iii)Wavae nguo inayofunika mwili mzima isipokuwa tu uso na viganja vya mikono (wengine wanasema na nyayo za miguu).
(iv)Wavae Shungi (jalabibi) iliyoshuka vizuri kiasi cha kufunika kifua mpaka kutovuni.
(v)Wavae vazi pana linaloshuka vizuri bila ya kubana kiasi cha kuonesha makunjo ya mwili.
(vi)Vazi la baibui au kanzu liwe na mikono mirefu yenye 211 vifungo karibu na viganja vya mikono ili isitokee mwanya wa vazi hilo kuvuka na kuiacha mikono uchi wakati wa kufanya shughuli mbalimbali.
(vii)Pamoja na wanawake kuruhusiwa kuvaa mapambo (kinyume na wanaume), hawaruhusiwi kudhihirisha mapambo yao ila kwa wale waliotajwa katika aya (24:31).
(viii)Wanawake hawaruhisiwi hata kudhihirisha sauti ya mapambo yao. Pia wanawake hawaruhisiwe kudhihirisha hata harufu na rangi ya vipodozi vyao. Wanaruhisiwa kujipodoa kwa mafuta na manukato butu (yasiyo na harufu kali). Ni haramu kwa wanawake kujipaka rangi za midomoni, kuchani, viganjani na kwingineko penye kud h ih irika.
(ix)Ikibidi wanawake waongee na wanaume wasio maharimu zao, wanalazimika kuzikaza sauti zao. Wanawake kulegeza sauti zao mbele ya wanaume wasio maharimu ni miongoni mwa vichocheo vya zinaa.
(x)Wanawake wamekatazwa kutoka ovyo majumbani mwao pasi na sababu za msingi. Na wakitoka kwa sababu za msingi wachunge miiko yote ya Hijabu iliyoelekezwa katika aya hizi pia wajiepushe na michanganyiko ya wanaume na wanawake isiyozingatia mipaka ya Uislamu. Ni haramu kwa mwanamume na mwanamke ajinabi kukaa faragha wakiwa wawili tu. Ikibidi wanaume na wanawake kukutana pamoja kwa ajili ya jambo la kheri wasiwe chini ya watu watatu.
Pamoja na maelekezo haya ya Hijabu, bado Uislamu umechukua hatua nyingine ya kuikinga jamii na zinaa na majanga yatokanayo kwa kuhalalisha na kuhimiza ndoa (rejea Qur'an 4:24, 5:5). Pia katika Hadithi ya 'Abdullah bin Mas'ud (r.a), Mtume (s.a.w) aliwausia vijana:
βEnyi kongamano la vijana! Na aoe yule aliye na uwezo miongoni mwenu, Hakika kuoa kunainamisha macho na asiyeweza kuoa na afunge; hakika funga hukata matamanio" (Bukhari na Muslim).
Wanawake wa Kiislamu pamoja na washauri wao (mawalii wao) wanashauriwa watoze mahari kidogo kulingana na hali ya muoaji mtarajiwa, ili kurahisisha ndoa.
Hivyo, katika majumuisho ya sehemu hii tunajifunza kuwa Uislamu unatokomeza zinaa katika jamii kwa kufuata hatua zifuatazo:
(1)Kuwakataza watu kuikurubia zinaa na kuonesha ubaya wa zinaa (Qur'an 17:32)
(2)Kutoa maeelekezo ya Hijabu kwa wanaume na wanawake ambayo yakitiiwa ipasavyo yanawawezesha watu kuepukana na zinaa.
(3)Kuhimiza ndoa ambayo ndiyo njia pekee iliyo nzuri katika kutosheleza matashi ya kimaumbile ya ngono.
(4)Kutoa adhabu kali kwa wazinifu ili iwe onyo kwao na kwa jamii nzi ma.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 530
Sponsored links
π1 Madrasa kiganjani
π2 Kitabu cha Afya
π3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
π4 Kitau cha Fiqh
π5 Simulizi za Hadithi Audio
π6 kitabu cha Simulizi
Nguzo za imani
Zifuatazo ni nguzo za imani
(EDK form 2: elimu ya dini ya kiislamu) Soma Zaidi...
Mgawanyiko wa Elimu kwa mtazamo wa kikafiri
Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera. Soma Zaidi...
Kutopupia dunia
"Ewe mwanangu! Soma Zaidi...
Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)
"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu Soma Zaidi...
KAZI ZA MALAIKA
Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi. Soma Zaidi...
Kuwafanyia Wema Wazazi
Allah (s. Soma Zaidi...
Lengo la kuumbwa Mwanadamu ni lipi?
Kwenye kipengele hichi tutajifunza lengo la kuumbwa mwaanadamuengo la kuumbwa ulimwengu na viumbe vilivyomo. Soma Zaidi...
Neema Alizotunukiwa Nabii Daudi(a.s)
Soma Zaidi...
Elimu Yenye Manufaa
Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa. Soma Zaidi...
Mambo ya lazima kufanyiwa maiti ya muislamu
Mambo ya faradhi kuhusu maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Nguzo za Imani kwa mujibu wa mafunzo ya kiislami.
Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu nguzo sita za imani katika Uislamu. Soma Zaidi...