Sifa za malaika
Sifa za malaika
Ni viumbe watiifu wasiomuasi Allah(SW)
Malaika ni viumbe watiifu kwa Allah(SW). Wakipewa amri ya kumuadhibu mtu muovu, hawagomi wala kumuonea huruma mtu huyo.Enyi mlioamini! Ziokoeni nafsi zenu na nafsi za watu wenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Juu yake kuna Malaika w akali wenye nguvu.Haw amuasi Allah(SW) katika yale anayowaamuru, na wanatekeleza vile walivyoamrishwa.(66:6)
Wana elimu ya kutosha kutekeleza majukumu yao
Malaika wana elimu inayowawezesha kutekeleza majukumu yao bila ya kubabaisha. Elimu waliyopewa malaika ni sehemu ndogo sana katika ujuzi wa Allah(SW). Na wenyewe walikiri mbele ya Allah(SW)Wakasema: Utukufu ni wako! Hatuna elimu ila ile uliyotufundisha, bila shaka wewe ndiye mjuzi na mwenye hekima(2:32)
Malaika hawana jinsia ya kike wala ya kiume. Qurβan inawakosoa watu wanaodhani kuwa malaika ni wanawake. In a h oji:
Na wamewafanya malaika ambao ni waja wa Mwingi wa Rehma kuwa ni wanawake. Je wameshuhudia kuumbwa kwao(43:19).
Ni viumbe wenye mbawa
βSifa zote njema ni za Allah, Muumba wa mbingu na ardhi. Aliyewafanya malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, na tatu tatu, na nne nne. Huzid is ha katika kuumba apendavyo. Bila shaka Allah ni mwenye uweza juu ya kila kituβ. (35:1)
Huweza kujimithilisha umbile la mwanadamu
Malaika huweza kujimithilisha kuwa kama wanadamu. Hufanya hivyo pale wanapotumwa na Allah(SW)kuleta ujumbe kwa watu maalumu. Kwa mfano, Bibi Maryam, mama yake nabii Isa(a.s), alijiwa na malaika katika umbo mithili ya mwanaume.Na mtaje katika kitabu, Maryam, alipojitenga na watu wake katika upande wa mashariki.
Tukampelekea Muhuisha sharia Yetu(Jibril) akajimithilisha kwake kwa sura ya binaadamu aliye kamilifu. (19:16-1 7)
Lengo la kuumbwa malaika
Lengo la kuumbwa malaika ni kumtumikia Allah(SW). Katika kutekeleza lengo la kuumbwa kwao, malaika hawana hiyari katika kutekeleza amri za Allah(SW), hufanya mambo yote vile anavyotaka Allah(SW).
..Hawamuasi Allah(SW) katika yale anayowaamuru, na w anatekeleza vile w alivyoamrishw a.(66:6)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Dua za Mitume na Manabii π2 ai web app π3 Madrasa kiganjani π4 Bongolite - Game zone - Play free game π5 Simulizi za Hadithi Audio π6 web hosting
Post zinazofanana:
Mtazamo wa makafiri juu ya dini
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na maumbile yake
Kuwa ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na umbile la mwanadamu.
Soma Zaidi...Mambo muhimu anayofanyiwa muislamu kabla ya kufa
Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mafundisho ya Mitume
Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s.
Soma Zaidi...