image

Inakuwaje unafanya ngono na aliyeathirika na usipate UKIMWI?

Watu wengi wamekuwa na mawazo kuwa ili nipate ukimwi ninatakiwa nishiriki ngono zembe na aliyeathirika mara ngapi? Majibu ya swali hili ni mafupi tu, ni kuwa unaweza kuathirika kwa ngono zembe ya siku moja tu ndani ya dakika chache. Lakini jambo la kuzing

Inakuwaje unafanya ngono na aliyeathirika na usipate UKIMWI?

Njia ambazo virusi huingia mwilini:

Kabala ya kuingia ndani zaidi kwenye somo letu, kwanza tujuwe namna ambavyo virusi vya ukimwi vinavyoingia ndani ya miili yetu. Mara tu virusi vinapokutana na mwili wa mtu unaanza kutafuta njia za kuingilia mwilini hadi kufikia kwenye damu. Njia hizo ni kupitia kwenye majeraha, michubuko, matundu yaliyo wazi kwenye vidonda, upele, majibu ama sehemu za mwili zilizo wazi kupitia mikato kama mtu alikatwa na kitu cha ncha kali, ama alichomwa kwa sindano ama kitu cha ncha kali.

 

Michubuko inaweza kuwa kwenye sehemu za siri yaani uke na uume kutokana na kufanya tendo la ndoa, ama michubuko inaweza kuwa kwenye maeneo mengine ya mwili kutokana na majeraha, mikato ama mikwaruzo. Majeraha na vidonda huweza kupatikana kwenye mdomo ama maeneo mengine ya mwili kutokana na majeraha ama mikato na mikwaruzo. Pia wakati wa kunyoa sehemu za siri huwenda mtu akajikata hivyo kusababisha majeraha madogomadogo.

 

Nini hutokea baada ya virusi kuipata njia ya kuingia mwilini?

Kitu cha kwanza virusi huhitaji kuingia kwenye damu. Vinapofika kwenye damu vinatafuta seli zinazofahamika kwa jina la CD4. Katika damu aina zisizopunguwatatu za seli. Kuna seli hai nyekundu za damu, kuna seli hai nyeupe za dam na pia kuna seli sahani. Seli hai nyekundu kaziyake kuu ni kusafirisha hewa ya okksijeni kwenda maeneo mengine ya mwili. Kazi kuu ya seli hai nyeupe ni kulinda mwili na kukinga dhidi ya vijidudu vya maradhi kwa kuviuwa vijidudu hivi.

 

Sasa virusi vya virusi vya ukimwi vinapoingia kwenye damu moja kwa moja hutafuta seli hai nyeupe inayofahamika kwa jina la CD4 na kuingia ndani. Lengo lake ni kweda kuzaliana humo. Hivyo virusi vinapoingia kwenye seli hizi vinaanza kuzaliana na vikijaa kwenye seli seli hupasuka na kumwaga maelfu ya virusi kwenye damu, kisha mchakato huendelea kwenye seli nyingine. Kwa njia hii virusi vinajaa mwilini na kuathiri seli nyingi Zaidi na kila seli inapojaa virusi hupasuka na kufa. Kadiri seli zinapokufa ndipo kinga ya mwili hupunguwa na hatimaye kupata upungufu wa kinga mwilini.

 

Sasa inakuwaje inakuwaje mtu anashiriki tendo la ndoa na mtu aliyeathirikabila ya kuathirika?

Ok, sasa turudi kwenye swali letu la msingi. Bila shaka umejifunza hapo juu njia ambazo virusi huingia mwilini. Wapo watu wengi walioishi miaka kadhaa na waathirika bila ya wao kuathirika na hali wanazaa watoto n ahata hawatumii kinga. Unadhani ni kitu gani hapa hutokea. Zifuatazo ni baadhi tu ya sababu:-

 

 

 

Je nawezaje kuzuia kutopata michubuko wakati wa tendola ndoa?

Hili ni swali zuri, ila kabla ya kulijuwa uzuri wa swali hili, nakupa swali jingine. Je kuna umuhimu gani wa kujizuia kutopata michubuko wakati wat endo la ndoa? Kwa ufupi wa majawabu ni kuwa, michubuko ndio njia ambazo virusi huweza kuingia mwilii, sasa kama hatuna michubuko si rahisi kwa virusi kuingia mwilini. Sasa wacha tuone njia ambazo unaweza kutumia kuzuia michubuko wakati wat endo la ndoa:-

 

 

 

 

Inakuwaje idadi ya virusi ikawa 0 kwenye damu na mtu akawa ni muathirika?

Vipimo vya virusi vya ukimwi vipo vya aina nyingi. Kuna ambavyo hupima idadi ya virusi kwenye damu na kuna ambavyo hupima antibody zinazotolewa na virusi. Kitaalamu idadi ya virusi kwenye damu hufahamika kama viral load. Sasa hutokea wakati kwa yule anayetumia dawa za VVU ikafikia idadi ya virusi kwenye damu yake inawa ni sifuri. 

 

Hii hutokea kama ametuma dawa kwa muda mrefu usiopunguwa miezi 6, na akawa anafuata masharti yote. Sasa endapo atadumu na hali hii kwa muda wa miezi 6 hawezi kumuambukiza mtu. Sasa lamda tuone hali hii inatokeaje. Kawaida kama mtu ameanza mapema kutumia ARV basi dawa hizi huzuia uzalishaji wa virusi hivi ama hupunguza visizaliane ama hupunguza visisathiri seli nyingine. Kama mtu atatumia vema dawa virusi vinakwenda kujificha maeneo mengine ya mwili na vinaondoka kwenye damu, na hapa ndipo hufikia mtu anawa hana kabisa virusi kwenye damu.

 

Sasa kwa kuwa virusi hivi bado vipo mwilini ila vimejificha tuu, vitaendelea kuzalisha kemikali zinazofahamika kama antibody, kemikali hizi ndizo hutuonyehsa kuwa bado vipo mwilini ila vimejificha. Endao mtu ataacha kutumia dawa vitarudi tena kwa kasi kubwa na kwa nguvu mpya na kuathiri wili kwa haraka Zaidi. Ikifikia hali hii mtu huambiwa kitaalamu ana viral resistance yaani virusi vyeke vimetengeneza usugu.

 

 

Tukutane Makala ijayo tutakapozungumzia watu walio hatarini kupata maambukizi na dawa wanazopaswa kutumia kama tahadhari kwao.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 8695


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

TIBA YA MINYOO AU DAWA YA MINYOO: praziquantel (biltricide) mebendazole (vermox, emverm) na albendazole (albenza).
TIBA YA MINYOO Moja katika sifa za minyoo ni kuwa wanatibika kwa urahisi pindi mgonjwa akipewa dawa husika. Soma Zaidi...

Yajuwe maradhi ya PID yaani uvimbe kwenye fupanyonga
Posti inazungumzia Ugonjwa kwenye fupa nyonga ambapo kitaalamu hujulikana Kama {Pelvic inflammatory (PID) ni maambukizi ya viungo vya uzazi vya mwanamke. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa UTI
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa UTI Soma Zaidi...

Dalili za ukimwi, unavyoenezwa na njia za kujikinga
Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.unasababishwa na virusi ambavyo hutokea kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali Soma Zaidi...

Namna ya kujikinga na VVU/UKIMWI
Somo hili linakwenda kukueleza namna mbalimbali za kujikinga na VVU/UKIMWI Soma Zaidi...

Dalili za maambukizi kwenye ovari
Posti hii inahusu zaidi dalili za maambukizi kwenye ovari, ni maambukizi ambayo hutokea kwenye ovari na kusababisha matatizo makubwa kama mgonjwa haujatibiwa mapema. Soma Zaidi...

Maumivu ya magoti.
Maumivu ya magoti ni malalamiko ya kawaida ambayo huathiri watu wa umri wote. Maumivu ya goti yanaweza kuwa matokeo ya jeraha, kama vile ligament iliyopasuka au cartilage iliyochanika. Soma Zaidi...

Hernia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa hernia Soma Zaidi...

Madhara ya maambukizi kwenye tumbo
Posti hii inahusu zaidi madhara ya maambukizi kwenye tumbo,hasa pale ambapo mgonjwa hakutibiwa Soma Zaidi...

YAMINYOO NA ATHARI ZAO KIAF
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Sababu za maumivu ya tumbo kwa chini uapande wa kushoto
Zijuwe sababu kuu zinazokufanya ukahisi maumivu makali ya tumbo kwa chini upande wa kushoto Soma Zaidi...

Njia za kutibu saratani
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za matibabu ya ugonjwa wa saratani,ni ugonjwa ambao unaweza kupona ikiwa umegundulika mapema katika hatua za mwanzo na kama ugonjwa huu umefikia hatua za mwisho Tiba yake huwa ni kupunguza makali ya ugonjwa. Soma Zaidi...