Namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, hizi ni njia ambazo zinapaswa kufuatwa ili kutokomeza kabisa maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa sababu nyingi zinazoweza kusababisha maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo ni uchafu ambao tunakutana nao kwenye shughuli zetu za kila siku kwa hiyo tunapaswa kufanya yafuatayo ili kuweza kuepuka madhara makubwa yatokanayo na Maambukizi
2.Kwanza kabisa tunapaswa kuepuka kunywa maji machafu na vyakula vichafu kwa hiyo tunapaswa kuchemsha maji na kuyachuja kabla ya kunywa na pia chakula kinapaswa kwa cha moto au kufunikwa vizuri kama tumemtunzia mtu ili kuepuka kupandwa na nzi ambao utua sehemu mbalimbali.
3. Tunapaswa kuishi mikono na maji safi na sabuni baada ya kutoka chooni, kabla ya kuandaa chakula , kabla ya kula na kabla ya kugusa kitu chochote ambacho kinaingia mdomoni mwa mtu kwa kufanya hivyo tunaweza kupunguza maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
4. Pia tunapaswa kuwashauri Watu wale wanaotumia madawa ya antibiotics mara kwa mara bila mpangilio na bila maelekezo kutoka kwa daktari au wataalamu wa afya wanapaswa kuacha kabisa kwa sababu nazo uleta Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo ikiwa zitatumiwa bila mpangilio
5.Na pia tunapaswa kuosha vyakula vyote tunavyozipata kutoka sokoni na pia kuelimisha jamii matumizi ya choo na kuacha kukisaidia ovyoovyo kwa kufanya hivyo tutaweza kuondoa tatizo la Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
FAIDA ZA KIAFYA ZA MINYOO: kupunguza aleji, kuchochea utungaji wa mimba, kupona kwa vidonda vya ndani
FAIDA ZA KIAFYA ZA MINYOO Wakati mwingine kuwa na aina flani ya minyoo kunaweza kuwa na faida katika afya.
Soma Zaidi...Homa ya matone (Mumps): Dalili na tiba yake.
Homa ya matone, inayojulikana kama Mumps, ni maambukizi ya virusi yanayoathiri tezi zinazozalisha mate (salivary glands), hasa tezi zilizopo pande zote mbili za shavu (tezi za parotidi). Ugonjwa huu huambukiza kwa urahisi kupitia matone ya maji yanayotoka unapopiga chafya, kukohoa, au kuzungumza. Ingawa kwa sasa ni nadra kutokana na chanjo, bado inaweza kuwapata watu ambao hawajapata chanjo hiyo. Makala haya yanakupa uelewa wa dalili zake na jinsi ya kutoa huduma ya kwanza.
Soma Zaidi...Fangasi wa kwenye kucha: dalili zake, na kumbambana nao
Hawa ni fangasi ambao wanashambulia sana kwenye kucha za vidole vya mikonobna miguu.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ambao kwa kitaalamu huitwa Dementia ugonjwa huu uwapata wale ambao umri umekwenda lakini kwa wakati mwingine Usababishwa na vitu mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Dalili za kuvimbiwa kwa watoto.
Kuvimbiwa kwa watoto ni shida ya kawaida. Kuvimbiwa kwa watoto mara nyingi huonyeshwa na kinyesi kisicho kawaida au kinyesi ngumu na kavu.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa Saratani ya ini.
Saratani ya ini ni Saratani inayoanzia kwenye seli za ini lako.
Soma Zaidi...