Dalili kuu za minyoo


image


Minyoo ni katika viume wanyonyaji, wanaoishi katika miili ya viumbe hai na kujipatia chakula humo. Minyoo wanaweza kuishi kwenye maeneo yenye majimaji kama kwenye maji, ndani ya viumembe hai kama mtu, ngombe, ngure na paka. Minyoo pia wanaweza kuishi kwenye udongo. Minyoo wanaweza kusababisha maradhi ndani ya mwili wa kiumbe hai. Minyoo isipotibiwa inaweza kusababisha athari zaidi kwenye afya ya mtu. Makala hii inakwenda kukuletea dalili za minyoo.


DALILI ZA MINYOO

Aina za minyoo:

Kuna aina za minyoo ziatazo 300000 na kati ya hozo 300 tu ndio ambazo husababisha maradhi kwa binadamu. Minyoo imegawanyika katika aina kadhaa kulingana na tabia zao, jinsi wanavyozaliana na maeneo wanayoishi, pia na maumbile yako. Aina hizo za minyoo ni kama:-

 

  1. Trichinosis hawa tunaweza kuwapata kutoka kwa wanyama
  2. Pinworm (thread worm) hawa ni wadogo sana na unaweza kuwapata kwa kuyala mayai yao kutoka pale yalipo. Kama utakuwa unanawa mikono mara kwa mara, kabla ya kula na huna tabia ya kula vidole ni ngumu kuwapata hawa minyoo
  3. Hookworm (roundworm) minyoo hawa husambazwa kupitia udongo na kinyesi
  4. Fluke; (flatworm) hawa wanaishi kwenye utumbo mdogo na meneo mengine. Tunaweza kuwapata kwenye vyakula na mboga zisizooshwa vyema.
  5. Tapeworm (flatworm)  unaweza kuwapata hawa kwenye maji machafu na kwenye vyakula.

 

Je ni wapi naweza kupata minyoo?

Minyoo tunaweza kuipata maeneo mengi. Na katika miili yetu pia inaweza kuingia kupitia njia nyingi. Njia kuu ni kwa kupitia mdomoni kwa njia ya chakula, ama kinywaji. Lakini pia inaweza kupitia kwenye ngozi. Hebu tuyaone maeneo ambayo monyoo ipo sana.

 

  1. Kwenye majimaji
  2. Ndani ya maji
  3. Kwenye udongo
  4. Kwenye nyama
  5. Kwenye chakula kisichopikwa kama matunda
  6. Kwenye mbog za majani

 

Ni kivipi naweza pata minyoo?

  1. kwa kugusa kitu chenye mayai ya minyoo, kisha ukapeleka mkono mdomoni bila ya kuosha
  2. Kunywa maji yenye mayai ya minyoo
  3. Kula chakula chenye mayai ya minyoo
  4. Kula udongo wenye mayai ya minyoo
  5. Unapotembea bila ya viatu maeneo machafu
  6. Unapokula vyakula visivyopikwa ama vilivyopikwa kwa uchache kama nyama ya ngurue

 

Ni ziipi dalili za minyoo?

  1. Maumivu ya tumbo
  2. Kuharisha, kutapika na kupata kichefuchefu
  3. Tumbo kujaa gesi ama kuunguruma
  4. Uchofu wa mara kwa mara
  5. Kupunguwa uzito bila ya sababu maalimu
  6. Tumbo kujaa na kuwa gumu

 

Ni vipi naweza kuepuka kupata minyoo?

  1. Osha mikono kabla ya kula ama kuingiza mdomoni
  2. Kula chakula kilichopikwa vyema
  3. Usile matunda bila ya kuosha
  4. Unapotembea kwenye ardhi chafu usitembee bila ya viatu
  5. Kama unaishi na paka ama mbwa hakikisha yupo salama
  6. Vinyesi vya wanyama kama paka, mbwa, na wanyama wafugwo wa nyama vihifadhiwe vyema.
  7. Kuwa makini na nyama ya nguruwe.

 

JE minyoo inatibika?

Ndio mimnyoo inatibika tena kwa muda mchache tu. Kama unasumbuliwa fika kituo cha afya kwa vipimo zaidi. Makala inayofata tutazungumzia kuhusu matibabu ya minyoo.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    3 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    4 Jifunze Fiqh    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Dalili za ugonjwa wa kaswende
Post hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa kaswende kwa wajawazito, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa watu wote, kwa sababu ugonjwa huu una dalili ambazo upitia kwa hatua mbalimbali kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

image Mambo ya kufanya kama una kiungulia
Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo unapaswa kufanya kama una tatizo la kiungulia. Soma Zaidi...

image Dalili za moyo kutanuka
Posti hii inahusu zaidi dalili mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza na kuonyesha kwamba moyo umetanuka. Soma Zaidi...

image Njia za kusambaa kwa ugonjwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine
Posti hii inahusu zaidi jinsi magonjwa yanavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Soma Zaidi...

image Matibabu kwa mtu mwenye kiungulia
Posti hii inahusu zaidi matibabu kwa mtu mwenye kiungulia,ni tiba ambayo mtu anapaswa kutumia kama ana tatizo la kiungulia Soma Zaidi...

image Sababu ya maumivu ya magoti.
Posti hii inahusu zaidi sababu za maumivu ambayo yanasikika kwenye magoti, huu ni ugonjwa ambao umewapata walio wengi na bado ni kilio kwa walio wengi kwa vijana na kwa wazee, Kuna wataalamu mbalimbali ambao wameweza kugundua sababu za maumivu kwenye magoti kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

image Fahamu kuhusu fangasi za ukeni
Posti hii inahusu zaidi fangasi za ukeni, hili ni tatizo kubwa ambalo linawakumba watoto, akina dada na wanawake kwa hiyo na vizuri kujua Dalili zake na kuweza kuchukua hatua mapema. Soma Zaidi...

image Vyakula vya kusaidia katika matibabu ya kiungulia
PoPosti hii inahusu zaidi vyakula ambavyo unaweza kutumia iwapo umepata tatizo la kiungulia Soma Zaidi...

image Jifunze zaidi mzunguko wa mfumo wa damu kwa binadamu
Posti hii inahusu zaidi mfumo wa mwili ambao huhusika na kusafirisha damu ,virutubisho na takamwili.mfumo huu unajumuisha damu,mishipa ya damu na moyo.moyo husukuma damu kupitia mishipa ya damu na kufika maeneo yote ya mwili. Soma Zaidi...

image Je utaweza kuambukiza HIV ukiwa unatumia PrEP?
Swali hili limeulizwa na mdau mmoja. Kuwa endapo mtu atafanya ngono zembe na akapata virusi je ataweza kuambukiza. Soma Zaidi...