Ijue dawa ya sulphadoxine na pyrimethamine (sp)

Post hii inahusu zaidi dawa ya Sp , kirefu cha dawa hii ni sulphadoxine na pyrimethamine hii dawa ilitumika kutibu malaria kwa kipindi fulani lakini sasa hivi imebaki kutumiwa na wajawazito kama kinga ya kuwazuia kupata malaria.

Ijue dawa ya  Sp.

1. Kama tulivyotangulia kusema kwamba ni dawa ambayo ina majina mawili ambayo ni sulphadoxine na pyrimethamine ambayo uunda dawa hii ya Sp, dawa hii iko kwenye mfumo wa vidonge ambapo kila sehemu ina milligrams zake ambapo sulphadoxine ina milligrams miatano na pyrimethamine ina miilgram ishirini na tano jumla kuu ufanya miligramu mia tano ishirini na tano.

 

2. Dawa hii utumika sana kwa wanawake wajawazito na haipendekezwi kama mojawapo ya dawa za kutibu malaria kwa sasa, ila kwa wajawazito ikitokea wakapata malaria ingawa wanatumia sp matibabu yao wanapaswa kuwaona wataalamu wa afya ili wawaeleze cha kufanya.

 

3. Kwa akina Mama wajawazito wanapaswa kutumia vidonge hivi vya sp pindi wanapogundua kwamba ni wajawazito kwa sababu vidonge hivi vikimezwa uenda moja kwa moja mpaka kwenye sehemu ya mwanzo ya kondo la nyuma na kuweza kuzuia wadudu wanaosababisha malaria kutoingia kwenye kondo la nyuma na kusababisha madhara mbalimbali kama vile mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, mtoto kutokuwa na afya nzuri akiwa tumboni, au mimba kutoka.

 

4. Kwa hiyo akina mama wanapaswa kujua kabisa kwamba hizi dawa ni za muhimu sana wakati wa ujauzito kwa sababu bila matumizi ya dawa hizi madhara makubwa yanaweza kutokea ambayo usababisha kukosa mtoto, au mimba kutoka, mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, haya matatizo utokea kwa sababu ya kuwepo kwa wadudu wa malaria kwenye kondo la nyuma na kusababisha uharibifu kwenye sehemu hiyo.

 

5. Akina mama wote wanapaswa kutumia dawa hizi isipokuwa wale wenye aleji na sulphur , au wanaotumia dawa ambazo kwa kitaalamu huitwa cotrimoxazole au wale wamama ambao wamegundulika na malaria kwa hiyo wanapaswa kufuata kawaida ya matibabu ya ugonjwa wa malaria kadri ya wataalamu wa afya.

 

6. Kwa hiyo akina mama wenye imani potovu kuhusu dawa hizi wanapaswa kujua kwamba dawa hizi ni za muhimu sana na kutotumia dawa hizi ni hatari sana hasa kwa afya ya mtoto.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/15/Thursday - 12:07:12 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1703


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-