Post hii inahusu zaidi dawa ya streptomycin ni dawa mojawapo ya kupambana na bakteria hasa wanaoshambulia mfumo wa hewa.
1. Streptomycin ni mojawapo wa dawa ya kupambana na bakteria hasa bakteria ambao ushambulia mfumo wa hewa , bakteria hao kwa kitaamu huiitwa mycobacterium ni bakteria ambao ueneza kifua kikuu kwa kutumia dawa hii pamoja na dawa nyingine kifua kikuu uweza kutibika kwa kufuata kanuni na utaratibu wa matibabu.
2. Dawa hii ya streptomycin inafanya kazi kwa kupitia kwenye mzunguko wa damu na ikifika kwa bakteria inashambulia Ganda la juu ambalo kwa kitaamu huiitwa cell wall na kuingia kwa Ganda la ndani kwa kitaamu huiitwa cell membrane na kujibanza kwenye protein kwa hiyo uzuia protini ya bakteria kuendelea kuzalishwa na kuzuia kuendelea kukua na kusababisha kuharibu kwa bakteria na ugonjwa hauwezi kuendelea kuwepo tena, na mafanikio ya kupona utokea kulingana na udumifu na maelekezo katika matumizi ya dawa.
3. Katika kufanya kazi dawa hii upitia sehemu mbalimbali na kuweza kufanikisha uponyaji kwa hiyo dawa hiyo inapoingia mwilini na ikishasambaa uweza kupitia kwenye maji maji mbalimbali kwenye mwili ambayo Kwa kitaamu huiitwa extracellular fluids, na inapiita kwenye plasenta au kwa lugha nyepesi kwenye kondo la nyuma kama mama ana mimba, pia zinaweza kupitia hata kwenye maziwa ya mama kama ananyonyesha na kwenda kwenye maji maji ambayo yamo kwenye ubongo kwa kitaamu huiitwa cerebral Spinal fluids.
4. Kwa hiyo kama mama ana mimba anaweza kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi ya kifua kikuu,na kama mama ananyonyesha pia anaweza kumsaidia mtoto asipate kama hajapata kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hii wanaweza kusaidia hata vichanga na wanaonyonya .
5. Kwa matumizi ya dawa hii Kuna wale ambao hawapaswi kutumia dawa hii kwa mfano wenye aleji na streptomycin,wale wenye upungufu wa damu hawapaswi kutumia, watoto chini ya miezi miwili hawapaswi kutumia na wale wenye matatizo ya Figo wanapaswa kutumia dawa hii kwa kiwango kidogo na kwa wakati mwingine wanawapunguzia dozi.
6. Pia dawa hii nayo Ina mahudhi madogo madogo kama maumivu ya kichwa, kuwepo kwa ndoto za kutisha kwa baadhi ya wagonjwa au pengine mgonjwa anaweza kuwa na magonjwa ya akili kama vile kuwa mkimya sana au pengine kuchangamka sana ila ni kwa watu wachache mno, kwa sababu dawa hii upitia kwenye mmengenyo wa chakula Kuna hatari ya kupata kichefuchefu na kutapika, kuharisha pia utokea kukiambatatana na maumivu ya tumbo.
7. Kwa watumiaji wa mda mrefu wanaweza kuwa na matatizo ya macho au kuona kwa shida na pia mwili unaweza kuwa na vi upele pamoja na kujikuna kwa mda mrefu na pia dawa hizi zina tabia ya kupunguza damu mwilini wakati wa kutumia ni vizuri kuwa makini kwa wale wenye tatizo la upungufu wa damu wakati wa kutumia dawa hizi, kwa hiyo maudhi haya madogo madogo yakizidi na kuwa kama ugonjwa ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya Ili kubadilishiwaa dawa au kutoa huduma yoyote inayofaa.
8. Vile vile dawa hizi uweza kuingiliana na dawa nyingine na kumaliza nguvu dawa hizo na kufanya uponyaji kuwa wa shida, kwa hiyo kwa watumiaji wa penicillin na cephalosporin , dawa hii ya streptomycin uweza kumaliza nguvu dawa hizo na kufanya uponyaji wa kutumia penicillin na cephalosporin kushindwa kufanikiwa, kwa hiyo ni vizuri kuongea na mgonjwa ipasavyo Ili kuweza kuwa na uhakika wa dawa anazozitimia na kuweza kuwepo kwa tiba ya kweli na inayofaa.
9. Kwa hiyo katika matibabu au kutumia dawa hii ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya na sio kutumia dawa hii kiholela kwa sababu Zina matokeo mengine ni ya kuhitaji uangalizi na pia dawa hii uingiliana na dawa nyingine ni vizuri kabisa kabla ya kutumia dawa hii kuwaona wataalamu wa afya Ili kuweza kutumia dawa kwa umakinu Zaidi na kuepuka matatizo ambayo yanaweza kutokea.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi dawa ya amoxline .jinsi inavyofanya kazi mwilini.pamoja na matumizi yake.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za Doxorubicin and Daunorubicin katika kupambana na kansa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna au njia ya kufanya Ili kuweza kutumia tiba hii ya jino, kwa sababu ya mchanganyiko ambao umekwisha kuwepo kwa hiyo unachumua mchanganyiko unafanya kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Zipo dawa nyingi ambazo hufahamika katika kutibu fangasi kwenye mdomo ama kinywa. Miongoni mwa dawa hizo hapa nitakuletea baadhi yao. kama wewe pia unasumbuliwa na fangasi wa mdomo basi post hii itakusaidi sana.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya ALU ila kwa jina jingine huitwa dawa ya mseto,ni aina ya dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria ya kawaida.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi za dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria kali, ni dawa ambayo inatumika sana kutibu Malaria kali.
Soma Zaidi...DAWA YA MAPUNYEMatibabu ya mapunye inategemea ni wapi mapunjye yapo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya cardiac glycoside katika matibabu ya magonjwa ya moyo,dawa maalum ambayo imo kwenye kundi hili la cardiac glycoside ni digoxin, ni dawa muhimu ambayo utumika kwenye mfumo wa vidonge mara nyingi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mgawanyiko wa tiba ya kifua kikuu, kwa kawaida tiba hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Soma Zaidi...